WATU 38 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 55 WAMEJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA NYUMBA ZAO MKOANI SHINYANGA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Sehemu ya mabaki ya nyumba zilizobomolewa na mvua kubwa iliyonyesha katuika kijiji cha Mwakata, wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga na kusababisha vifo vya watu 39 na wengine 60 kujeruhiwa, usiku wa kuamkia leo Juatano Machi 4, 2015

WATU 38 wamekufa, baada ya kuangukiwa na nyumba zao, kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, Jumanne usiku wa kuamkia leo Machi 4, 2015.


ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI



Akithibitisha taarifa hizo kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema maafa hayo yametokea katika kijiji cha Mwakata, kata ya Isaka, wilayani Kahama na kwamba watu wengine 60 wamejeruhiwa vibaya huku mifugo kadhaa, ikiwemo Ng'ombe, Mbuzi na kuku navyo vimekumbwa na maafa. Huenda idadi ya waliokufa ikaongezeka, kwani zoezi la uokoaji linaendelea licha ya changamoto ya kutokuwa na vifaa vya kutosha vya uokozi.

CHANZO: LUKAZA BLOG

No comments

Powered by Blogger.