WAFANYABIASHARA WA DALADALA MJINI SONGEA WAINGIA KWENYE MGOMO WAKISHINIKIZA KIONGOZI WA WAFANYABIASHARA KUACHILIWA HURU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mgomo wa wafanya biashara umeendelea kuchukua sura mpya baada ya wafanya biashara wa daladala mjini Songea kugoma kufanya kazi toka asubuhi kwa madai ya kuunga mkono mgomo wa wafanya biashara unaoendelea katika mikoa mabalimbali nchini ili kushinikiza serikali kumuachilia kiongozi wao Bwana Joseph Minja pamoja na kutatua madai yao ya matumizi ya mashine za EFDS pamoja na ongezeko la kodi kwa asilimia mia moja.


Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo mjini songea hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa songea ambao wamelazimika kutembea kwa miguu kwenda maeneo mbalimbali ya mji huo ambapo jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

No comments

Powered by Blogger.