WANANCHI WA ARUMERU WAVAMIA SHAMBA LA MWEKEZAJI USIKU WA MANANE NA KUOTESHA MIGOMBA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 



 Hili ni moja ya bango lililowekwa na wananchi wa kijiji cha Nkoaranga na Poli wakidai shamba lao
 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki , Joshua Nassar akiwa ameongozana na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo kutembelea eneo hilola Shamba akiungana mkono na hatua hiyo ya wananchi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Nkoaranga na Poli wameingia katika Shamba la Karamu (Karamu Estate) usiku wa manane na kuamua kuotesha migomba kwa kile wanachodai kuchoshwa na serikali kushindwa kusikia kilio chao cha kurudisha ardhi ya mashamba makubwa yaliyomilikiwa na walowezi wakati wa ukoloni.
Shamba hilo linalodaiwa kuwa na zaidi ya Hekari 3500 lilivamiwa na wananchi hao na kuanza zoezi la kuotesha migomba kabla ya kuning'iza  mabango yenye ujumbe mbalimbali katika maeneo tofauti ya shmaba hilo.
Wakizungumza kwa sharti la kutotaja majina yao,wananchi hao walisema mashamba hayo enzi za ukoloni yalipelekea Wananchi wa Meru kuchangia fedha kwenye Vyungu na kwamba mwaka 1952 alitumwa marehemu Shujaa Japhet Kirilo kwenda umoja wa mataifa (UNO)kudai ardhi hiyo.
"Mwaka 1952 tulimtuma Shujaa wetu Kirilo kwenda umoja wa mataifa (UNO) huko New York nchini Marekani  kwenda kudai ardhi hii ya wana Meru lakini hadi leo hii mwaka 2015 maeneo mengi hayajarudi mikononi mwa wazawa."alisema mmoja wa wananchi hao.
Akizungumzia hatua hiyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari alisema: "Binafsi nikisaidiwa na Mhe. Halima Mdee,Waziri Kivuli wa Ardhi,tumepiga kelele vya kutosha Bungeni, serikali sikivu bado haijasikia kelele zetu. Pengine sasa Waziri Lukuvi na serikali hii ya CCM itasikia kilio cha wananci hawa walioamua kuingia shambani na kuotesha Migomba"alisema Nassari.
Alisema Shamba la Karamu lilikuwa likitumika kwa kilimo cha Kahawa na kwamba kwa sasa limegeuka pori huku mwekezaji akidaiwa kuuza kuni kwa wenyeji na kukodishiwa kulima bustani ndogo ndogo za mboga.
Nassari alidai kuwa hivi karibuni mwekezaji alidaiwa kumega eneo la shamba hilo na kisha kuliuza kwa chuo kikuu cha Tumaini, tawi la Makumira na kwa baadhi ya wageni kutokana na kile kinachodaiwa kumalizika kwa muda wa umiliki wa miaka 99.

Haya ni baadhi ya mabango yaliyowekwa na wananchi wa eneo hilo




Picha na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog

No comments

Powered by Blogger.