WAZIRI MKUU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAAFA YA MVUA SHINYANGA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mzee  Donald Lubunda ambaye  amepoteza watoto wanne katika maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha  katika  eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kuwapa pole waathirka leo
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa pole wanafamilia wa MzeeZakaria  Limbe ambao wamepoteza wototo wane katika mafa ya mvua kubwa yenye upepo na  mawe iliyonyesha katika eneo la Mwakata Machi  3 usiku. Alikwenda katika maeneo yaliyoathirika leo  kuwapa pole wananchi. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipa pole Shoma Petro  ambaye ni mmoja wa majeruhi wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa yenye upepo na mawe iliyonyesha kwenye  eneo la  Mwakata wilayani Kahama Machi 3, 2015 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kwenye hospitali a wilaya ya Kahama kuwapa pole  majeruhi waliolazwa hospitalini hapo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu, Jenista Mhagama  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dr Rufunga kukagua maeneo yalyoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana  na upepo mkali na mawe katika eneo  Mwakata wilayani Kahama usiku Machi 3, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments

Powered by Blogger.