ZITTO KABWE AFUNGUKA ASEMA TUHUMA DHIDI YAKE ZICHUNGUZWE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Katika kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, mbunge wa Sengerema Bwana William Ngeleja alisema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na wafanyabiashara na taasisi za umma. Katika Maelezo yake alirudia tuhuma dhidi yangu zilizokwisha tolewa huko nyuma kwamba 
1) nilipewa fedha na kampuni ya PAP na
2) nilipewa fedha na shirika la NSSF.
Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo. Watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao. Ndio maana Bwana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo wafanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Hivyo narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja, wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza. Nikiwa mbunge ambaye maisha yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha taasisi zake, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu dhidi ya tuhuma zilizotolewa na nyingine zozote ambazo mtanzania yeyote anazo dhidi yangu.
Naunga Mkono kwa nguvu kubwa kazi inayofanywa na Baraza la Maadili. Ni kazi ambayo ilipaswa kuwa imefanyika kwa muda mrefu sana kwa kashfa mbali mbali ambazo viongozi wa umma wamepata kama vile ile ya rada, rushwa katika manunuzi ya mafuta mazito kuendesha mitambo ya Umeme, kujipatia mikopo kwenye taasisi za umma bila kulipa, kujilimbikizia Mali tofauti na kipato nk. Hivyo naiomba Sekretariat ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya Bwana Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi.
Katika kujenga Misingi Madhubuti ya uwajibikaji nchini ni lazima kila kiongozi aheshimu taasisi kama Baraza la Maadili. Baraza likiendelea kufanya kazi kama inavyofanyika sasa, vita dhidi ya ufisadi itakuwa imepiga hatua na porojo za kuzushiana mitaani zitapungua.
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Dar Es salaam, tarehe 4 Machi 2015.

No comments

Powered by Blogger.