BASI LA SUPER FEO LILILOKUWA LINATOKEA MBEYA KWENDA SONGEA LIMETUMBUKIA MTONI ENEO LA PIPELINE INYARA LEO ASUBUHI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.




Mpaka Basi la Super Feo l inapata ajali lilikuwa na abiria 20 na basi hilo linauwezo wa kubeba abiria 53. Chanzo  cha ajali ni dereva wa basi alitaka kuovatake roli bila ya uangalifu na kakutana na roli akakimblia kulia zaidi ndipo ikapinduka mara tatu na kufikia kwenye kalvatina kutumbukia mtoni. 
Majeruhi  wametajwa kwa majina ambao ni Patriki Mwimbila  ambaye ni dereva msaidizi wa basi na amevunjika mguu majeruhi wengine ni Sakeni Mwandaneg, Fatuma Nyambi na Feliciana  Mwalongo hawa wote wamelazwa hospitali ya mkoa Mbeya. 
Waliofariki katika ajali hii ni watatu ambao ni Anastazia Ngonyani, Robett Leyman kutoka Marekani pamoja na mwanaume mmoja hajafahamika jina lake. Abiria kumi na tatu wako salama, dereva wa basi anaitwa Shafii Ngaiyo ametoroka baada ya ajali hiyo kutokea.

HABARI NA JOSEPH MWAISANGO

No comments

Powered by Blogger.