CHAMA CHA WANANCHI (CUF) CHATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 15 KUWASAIDIA WANANCHI WALIOATHIRIKA NA MVUA VISIWANI ZANZIBAR

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui (kulia), akikabidhi fedha taslimu shilingi milioni 15 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis, kusaidia watu waliopatwa na maafa yaliyotokana na mvua. Anayeshuhudia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis, akifurahi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kukabidhiwa shilingi milioni 15 na CUF kwa ajili ya kusaidia maafa ya mvua.
Katibu wa kamati ya maafa kitaifa Dkt. Khalid Salum Mohammed, akipokea fedha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa zilizotolewa na CUF Zanzibar.
Katibu wa kamati ya maafa kitaifa Dkt. Khalid Salum Mohammed, akipokea fedha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa zilizotolewa na CUF Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis, akijiandaa kukabidhi fedha taslimu shilingi milioni 15 kwa katibu wa kamati ya maafa kitaifa Dkt. Khalid Salum (kushoto), baada ya kuzipokea kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui (kulia). (Picha na Salmin Said, OMKR) 

Na: Khamis Haji, OMKR
Chama cha Wananchi CUF kimetoa shilingi milioni 15 kusaidia wananchi waliopatwa na maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonesha kwa takriban muda wa siku tatu na kuacha athari kubwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Fedha hizo zilikabidhiwa na Naibu Mkuu Mkuu wa CUF Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, katika halfa ambayo pia ilihudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, iliyofanyika huko ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, amesema chama hicho kimeguswa sana na maafa yaliyosababishwa na mvua, ambapo wananchi wengi wamekosa makaazi pamoja na kukosa huduma nyingi muhimu za kibinaadamu.
 “Baada ya kutembelea na kuona athari kubwa zilizowakabili wananchi wenzetu katika maeneo mbali mbali, CUF tumeona tuwafariji wenzetu kutokana na hicho kidogo tulichokipata”, alisema Maalim Seif.
 Naye Katibu wa Kamati ya Maafa Kitaifa, Khalid Salum Mohammed baada ya kukabidhiwa fedha hizo, amekishukuru Chama cha CUF kutokana na msaada huo ambao amesema unahitajika sana kutokana na kuwepo wananchi wengi wenye mahitaji, wakiwemo wanaotunzwa katika kambi maalum.
 Katibu Khalid alisema sehemu ya fedha hizo zitapelekwa kwenye kituo cha watoto yatima kilichopo eneo la Mwanakwerekwe mjini Zanzibar, ambacho kimeathirika kutokana na maafa hayo ya mvua.
“Tunakushukuru sana Maalim Seif na Chama cha CUF kwa jumla, fedha hizi zitasaidia sana kwa sababu hivi sasa kwa kweli tuna mahitaji mengi sana kutokana na kuwepo watu wengi wanaohitaji kusaidiwa”, alisema Khalid ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ali Juma Hamad, Mwakilishi wa jimbo la Chake Chake, Omar Ali Shehe na Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa CUF, Pavu Juma.

No comments

Powered by Blogger.