SERIKALI YAPANIA KUMCHUKULIA HATUA SHILOLE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Serikali imeahidi kumchukulia Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Akizungumza bungeni Dodoma jana, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia

“Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,” alisema Juma Mkamia.

No comments

Powered by Blogger.