NAPE ATANGAZA RATIBA YA MIKUTANO YA CCM UTAKAOFANYIKA MKOANI DODOMA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesema vikao hivyo vilianza leo kwa sekretalieti kukutana na kujadili maandalizi ya kamati kuu (CC), Halmashauri Kuu (NEC) na mkutano mkuu huku kesho julai 8 inakutana kamati ya Usalama na maadili ndani ya Chama ambacho kitakuwa chini ya Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Jakaya  Kikwete.
Nape amesema keshokutwa Julai 9 kutakuwa na uzinduzi wa Ukumbi mpya ambako kutafanyikia Mkutano mkuu wa mwaka huu utakaofanywa na mwekiti wa CCM Jakaya Kikwete na mchana kutakuwa na kikao cha kamati kuu ya halmashauri ya taifa ya chama hicho ambacho ni moja ya vikao kuelekea mkutano mkuu.
Julai 10, kutakuwa na kikao cha NEC kitakateua jina la mgombea urais wa Zanzibar , kazi ya pili itapia irani ya taifa ya CCM itakayotumika kuombea kura na kutumiwa kwa mwaka 2015/20 na kazi ya tatu kamati hiyo itapokea majina matano yatakayokuwa yameteuliwa na NEC na kisha kuyapigia kura ili kupata majina matatu ambayo yatapigiwa kura kwenye mkutano mkuu ili kupata jina moja litakalogombea nafasi ya urais mwaka huu.  
Alisema Julai 11 itakuwa siku ya mkutano mkuu ambao unatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja na vyomba mbalimbali vya habari zikiwemo Television na Radio

No comments

Powered by Blogger.