WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 30 KUJERUHIWA BAADA YA BASI LA ABIRIA KUGONGA TRENI YA MIZIGO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Watu 4 wamefariki dunia papo hapo na wengine 30 wamejeruhiwa baada ya treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza kugongwa na basi la abiria lililofahamika kwa jina na Badikadi mkoani Morogoro. 
Taarifa za awali toka kwa mashuhuda na majeruhi wa ajali hiyo wamesema kuwa, ajali hiyo imetokea eneo la njia panda kibaoni katika kijiji cha Kibaoni, kata ya Mpakani. 

Taarifa zaidi zinasema kuwa, dereva wa basi hilo lililokuwa linatoka Kilosa kuelekea Morogoro mjini alitaka kuvuka njia ya treni bila kuwa muangalifu ndipo basi hilo lilipogonga treni hiyo ya mizigo. 

Majeruhi wote hivi sasa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Kilosa.

No comments

Powered by Blogger.