Tukio lilikuwa kama hivi:- Dereva wa Pikipiki ya miguu mitatu, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiwa amelala chini huku akiugulia maumivu baada ya kugongwa na gari ndogo aina ya Pajero i0 Mitsubishi, yenye Namba za usajili T 179 BRU.
Ajali hiyo imetokea mwishoni mwa wiki hii eneo la Samaki Mbezi Beach jijini Dar es Saalm, baada ya dereva huyo mwanamama kukata kona ghafla ya kuingia njia ndogo ili kuelekea Saluni kwa ajili ya kuseti Nywele. 
Jamaa mmoja (kulia) akianza kumuita mama huyo ili kufika eneo la tukio ili kumsaidia kijana huyo, mama akitoka Saluni.
Kijana huyo akiwa amelala chini akiugulia maumivu huku mzigo wake wa Kreti za Bia na Soda zikiwa zimevunjika baada ya kutumbukia mtaroni.
Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini
Raia wakimwangalia kijana huyo huku wakishindwa kumsaidia wakibaki kujadili kuhusu mama huyo aliyemgonga na kwenda kuingia Saluni huku watu wakishindwa kumchukulia hatua.
Kijana mmoja akijaribu kusaidia kuokota baadhi ya vinywaji ambavyo vilikuwa havijavunjika.
Mama akijielezea kujaribu kujitetea.....
Mama akielekea kuonyesha sehemu ya nyuma ya gari lake anayodai kuwa ndipo alipojigonga dereva huyo wa Pikipiki.
Ghafla alizongwa na watu, hapa akijaribu kuwaka 'eti' asisogelewe, lakini wapi watu hao walimzonga.
Hapa wakiwa tayari wamemuweka mtu kati...huku kila mmoja akiwaka kivyake kuhusu dharau za mama huyo.
Majadiliano yakiendelea...
Watu wakaiwa katika mlango wa Saluni hiyo wakimtaka mama huyo kutoka nje baada ya kukimbilia ndani.
Baada ya ajali hiyo mwanamama huyo hakuweza kuonyesha ushirikiano wala kusimama bali aliendelea na safari yake hadi katika Saluni moja iliyo karibu kabisa na eneo la tukio na kushuka garini na kisha kuingia saluni humo na kuanza kuendelea na utaratibu wa ratiba yake kuanza kusetiwa nywele.
Jambo hilo liliwaudhi sana watu mashuhuda wa tukio hilo, ambao baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto ikiwa kazini walianza kusema ya moyoni, ''Sasa wewe mwandishi unapiga picha na kuandika habari we unaona hivi ni sawa kweli wakati mgonjwa anaugulia maumivi bila hata huduma ya kwanza wala kupelekwa hospitali wakati mhusika aliyemgonga ameonekana na anaendelea na shughuli zake tu pale saluni, ameingia kuseti nywele''. alisema mama mmoja aliyeonekana kukerwa na jambo hilo.
Baada ya kusikia hivyo kamera ya Mafoto ilielekea hadi katika saluni hiyo pamoja na watu waliokuwapo eneo hilo huku wengi wao wakilalama kila mmoja akitukana kivyake, na kumkuta mama huyo akianza kuingia katika Draya kuanza kusetiwa nywele zake, na alipoitwa na mmoja wa watu hao, mama huyo alionyesha dharau na kuendelea na utaratibu wake.
Jambo hilo lilimkera kila aliyefika katika mlango wa saluni hiyo na watu kushikwa na hasira huku kila mmoja akianza kutukana na kuingia bila utaratibu katika chumba cha saluni hiyo jambo lililowafanya wafanyakazi wa saluni hiyo kuingilia kati na kumsihi mama huyo kutoka nje.
Mama huyo alipotoka nje na kuhojiwa kulikoni kugonga mtu na kumuacha kama alivyo na akaekea kuseti nywele, Mama huyo alijibu:- ''Tayari nimesha muita ndugu yangu anakuja na Tax kuja kumpeleka hospitali kwa hiyo asubiri, kwanza sikumgonga mimi, mimi nimemgusa tu baada ya kugongwa na gari ya GX 100 iliyokimbia, kwa hiyo asubiri'', alisema mama huyo
Baada ya watu hao kusikia kauli hiyo walikuja juu na kumzonga mama huyo wakitaka kumshushia kichapo, hatimaye mama huyo aliamua kukimbilia ndani ya Saluni hiyo na kufungiwa huku watu hao wakijadiliana kulichoma moto gari lake lililokuwa limeegeshwa mbele ya Saluni.
Ilielezwa kuwa baadaye alifika ndugu wa huyo mama akiwa na gari lakini tayari kijana huyo akawa tayari ameshapata msaada ya kuwahishwa hospitali.
PICHA NA SUFIANI MAFOTO
No comments:
Post a Comment