Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Juni, 2017 amemteua Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Bibi Anna Elisha Mghwira anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki alikuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Tarehe ya kuapishwa kwa wateule wote itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Juni, 2017
ACT yaibana Serikali kuhusu vyeti
By: VIJIMAMBO on May 01, 2017 / comment : 0 ACT Wazalendo, Habari
CHAMA cha ACT – Wazalendo kimeitaka Serikali kufanya uhakiki wa vyeti kwa viongozi wote wa siasa na isipofanya hivyo kitafikisha suala hilo mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu, alisema endapo Serikali haitawahakiki viongozi hao na mamlaka zinazohusika kutowachukulia hatua kwa kughushi vyeti, kitafungua mashtaka mahakamani.
“Malalamiko ya wananchi kuwa kuna viongozi wamatumia vyeti feki na wengine wakituhumiwa kuwa na shahada batili ni ya muda mrefu.
“Ikumbukwe kiongozi ni kama dereva kwa hiyo kuwaacha kwa kisingizio cha kujua kusoma na kuandika ni sawa na kuwa na dereva ‘kihiyo’ anayeendesha gari lililo na abiria waelewa,” alisema Shaibu.
Alisema kitendo cha kutowahakiki viongozi hao kinapotosha mantiki nzima ya mchakato wa uhakiki na kuweka upendeleo wa dhahiri baina ya watumishi wa umma.
“Msingi wa mchakato huu ni kuhakikisha taifa linabaki na watumishi wenye sifa.
“Waziri Kairuki hakutaka kujiuliza iwapo viongozi wa siasa watathibitika kughushi vyeti ambalo ni kosa la jinai, haitawaondolea sifa yao ya uongozi,”alisema.
Kauli hiyo imetolewa ikiwa ni siku chache tangu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, kueleza kuwa uhakiki huo haukuwahusisha viongozi wa siasa kwa kile alichodai kuwa Katiba inawataka kujua kusoma na kuandika tu.
Waziri Kairuki alitoa kauli hiyo Aprili 28 mwaka huu, wakati akikabidhi taarifa ya uhakiki wa vyeti kwa Rais Dk. John Magufuli ambako watumishi 9932 walibainika kuwa wanatumia vyeti vya udanganyifu na kutakiwa kujiondoa wenyewe kazini.
Alisema watakaokaidi watafikiswa katika vyombo vya dola.
Shaibu alisema uamuzi wa kutowahakiki viongozi wa siasa ni ushahidi wa dhahiri wa jinsi Serikali inavyohaha kuwalinda baadhi ya wateule na wanasiasa ambao wametuhumiwa na umma kwa makosa ya kughushi vyeti.
Alisema kitendo cha Rais kutangaza kuwasamehe watumishi wenye vyeti feki watakaojiondosha kazini wenyewe ni kinyume cha sheria na Katiba ya nchi kwa sababu hana mamlaka ya kufanya hivyo katia katiba.
Alisema kwa mujibu wa sheria Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu anayetuhumiwa kufanya kosa la jinai iwapo mtu huyo hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuhukumiwa.
Mamlaka pekee aliyonayo Rais ni kutoa msamaha kwa wafungwa wanaotumikia kifungo, alisema.
Hakuna tatizo la njaa nchini – Rais Magufuli
By: VIJIMAMBO on January 12, 2017 / comment : 0 ACT Wazalendo, Habari, Magufuli, Rais, Zitto Kabwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ametoa wito kwa Watanzania kupuuza baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotoa taarifa kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la njaa huku akisema kuwa anayejua njaa ni Rais.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi mkoani Simiyu Rais Magufuli amesema kuwa taarifa hizo ni uzushi huku akisema kuwa kama yeye Rais wa Tanzania yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za njaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
“Wapo wafanyabiashara wengine wachache waliokuwa wamezoea panapotokea matatizo kidogo tu ya ukame wanatumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na magazeti wanayoyaamini wao sio magazeti yote, pamoja na baadhi ya wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa, anayejua njaa ni Rais na sio gazeti fulani mimi ndiyo niliyepewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania,” alisema.
Hivi karibuni kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita aliitaka serikali kutangaza balaa la njaa.
ZITTO KABWE AMTEMBELEA LEMA MAHABUSU, ATOA NENO
By: VIJIMAMBO on December 03, 2016 / comment : 0 ACT Wazalendo, Goodbless Lema, Habari, UKAWA, Zitto Kabwe
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Jana Ijumaa desemba 2/2016 nilipata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza Kuvu la Arusha. Nilimtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati Za kutafuta na kulinda Haki.
Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa Sana na ukiukwaji mkubwa wa Haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona Ni bora akae ndani Mpaka hapo Dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.
Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka Mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.
Amemshukuru Mungu Kwa kumpa Mke jasiri anayempa moyo na Ndio ngome yake Kwa sasa.
Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka Haki kutendeka Katika uendeshaji wa Nchi yetu. Siku zote Haki hushinda
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini(NCCR) na kuhamia ACT-Wazalendo, Moses Machali ahamia CCM
By: VIJIMAMBO on November 21, 2016 / comment : 0 ACT Wazalendo, CCM, CHADEMA, Habari, UKAWA
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE.
Kutoka mezani kwangu Moses Joseph Machali, Tarehe: 21/11/2016
Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake.
Mimi Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za Upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania. Watu wenye mwelekeo na dhamira ya kuijenga nchi yetu kwa maendeleo enedelevu ni jamii ya akina Magufuli, Kasim Majaliwa, nk.
Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli.
Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais kwa vitendo, kwa sababu ninaposoma Rekodi yangu ya enzi nikiwa Mbunge (Hansard) na kabla ya kuwa mbunge ni kwamba nilipinga mnoo wizi na ufisadi wa kila aina; Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa taifa (Rejeeni hotuba yangu ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, nikiwa Waziri Kivuli wa wizara hiyo ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016), vilevile bila kusahau hotuba zangu mbalimbali Bungeni na nje ya Bunge.
Kwa kushirikiana na wapinzania wenzangu enzi hizo tulishauri na kupinga ufisadi wa kila aina, tuliitaka serikali kufanya mambo yenye tija kwa taifa na sasa kila mwenye macho anaona hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona wapinzani; sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono.
Wale tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri nchini.
Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena bali ya JPM na CCM yake au yao. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Hakika huo siyo uungwana bali aina mpya ya ufisadi nchini na usaliti kwa agenda zao.
Kama kweli sisi tumeokuwa wapinzani na tulioonesha kupinga kwa nguvu zote ufisadi ulioiumiza nchi hii tulimaanisha yale tuliyoyahubiri na kuwaaminisha watu basi tunao wajibu wa kuacha tabia ya kuwa vigeugeu kwa mambo tuliyoyaamini na kuyahubiri. Kutofanya hivyo basi ni mwendelezo wa ufisadi kwa maslahi binafsi.
Ni nani asiyeona kwamba serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi mambo mengi tuliyoyapigia kelele? Au tunajifanya kutokukubali ukweli unaoishi kwa ule msingi wa upinzani wa Tanzania kwamba Tukimuunga mkono Mtawala kamwe hatutapata kuaminiwa na wapiga kura nchini na hivyo tupinge tu hata kama ni ukweli? Nadhani kinachofanyika ni mwendelezo wa kupinga hata mazuri ili kutafuta fursa ya wapinzani kukubalika kisiasa zaidi hata kwa njia na mbinu haramu kama kawaida ya siasa zilizo zoeleka hapa nchini kwa miaka mingi.
Taifa hili haliwezi kuendelea kwa kuwa na siasa za kutokukubaliana na ukweli unaoishi. Kama dhamira ya kila mtanzania ikiwemo wapinzani ni kuona nchi ina move basi hatuhitaji kuwa watu wa kupingapinga hata yaliyo mema bali kuyaunga mkono yale yaliyo mema bila kujali yanafanywa na nani bali msingi mzuri unapaswa kuwa ukweli kwa kila jambo.
Serikali ya awamu ya tano imeonesha njia ktk mambo mengi na inastahili kuungwa mkono. Safari ni hatua na ninaamini kwamba hata yale yanayoonekana kutokufanyiwa kazi ndani ya mwaka mmoja uliopita na ambayo yalishindikana huko nyuma, bado yanaweza kuja kufanyiwa kazi huko mbeleni. Serikali ya JPM imejitahidi sana tukilinganisha na huko tuliko toka. Uongozi huu unafanana sana na ule wa akina Hayati EDAWARD MORINGE SOKOINE chini ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Daima ninaamini ktk yale ninayoyaamini pasipo kufungwa na ukada bali kuangalia ukweli ni upi. Hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la KUDHIBITI wapiga dili wa fedha na mali za umma bali tukubali kwamba wapiga dili waliozoea kupiga dili na kuziingiza fedha walizopiga ktk mzunguko kwamba siyo jambo la msingi ktk kujenga uchumi imara.
Uchumi imara hauwezi kujengwa kwa kuruhusu ubadhirifu wa fedha na mali za umma au hata za mtu mmoja mmoja. Kinachoonekana hivi sasa ni kama nchi inasukwa upya na hivyo tuwaunge mkono viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa mema wanayoyafanya na kuwashauri kurekebisha ktk yale ambayo hayajakaa vizuri. Tuachane na siasa nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku mambo hayohayo yakifanywa na CCM yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo. CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono.
Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM kwa maslahi ya taifa kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe. Kwaherini Upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.
Moses Joseph Machali
X-mbunge, Kasulu Mjini 2010-2015,
Majibu ya ACT Wazalendo kwa Ole Sendeka baada ya kutaka Zitto achunguzwe
By: VIJIMAMBO on October 29, 2016 / comment : 0 ACT Wazalendo, CCM, Habari, Zitto Kabwe
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya kiongozi wake wa chama, Zitto Kabwe kwamba ana miliki mali za kifisadi pamoja na kuhusishwa na ununuzi wa ardhi maeneo ya Kigamboni uliofanywa na NSSF kwa bei ya milioni 800 kwa ekari moja, wakati bei halisi ni milioni 25 na kwamba kitendo hicho kimeitia hasara serikali .
Tuhuma hizo zilitolewa jana na Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Christopher Ole Sendeka, ambapo alivitaka vyombo vya uchunguzi kufanya uchunguzi katika shirika hilo ili kubaini waliohusika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria, huku akimhusisha Zitto katika uchunguzi huo.
Ole Sendeka alitaka akaunti za benki za Zitto pamoja na maisha yake binafsi kuchunguzwa kama yana uhalisia na kipato chake halali.
Tuhuma hizo zimekiibua chama cha ACT, ambapo leo Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa ACT, Habibu Mchange amevitaka vyombo vya uchunguzi haraka iwezekanavyo kuchunguza mali, madeni, akaunti zote za benki pamoja na mfumo wa maisha ya Zitto.
“ACT imeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa jana na Ole sendeka dhidi ya kiongozi wa chama chetu,” amesema.
Amesema kuwa, katiba ya chama hicho huwataka viongozi wote kuweka hadharani matamko ya mali zao na madeni na kwamba Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria hivyo mali na madeni yake yako hadharani na mtandaoni.
“Tunaamini kama kuna kiongozi ambaye mali, madeni, maslahi, na akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto,” amesema.
Aidha, Mchange amedai kuwa, kilichomsukuma Sendeka kutoa tuhuma hizo kwa Zitto ni harakati zake za kuupinga muswada mpya wa habari.
“Tuhuma za ole sendeka kuna kitu nyuma yake, jitihada za zito za kupambana na mswada wa habari ndizo zilizomuibua, sababu wanataka upitishwe ili kuviua vyombo vya habari,” amesema.
Amesema ACT itaendelea kuisimamia serikali katika mambo ya bungeni kama anavyofanya mbunge na kiongozi wao wa chama.
JESHI LA POLISI LAONDOA ZUIO LA MIKUTANO YA NDANI YA VYAMA VYA SIASA
By: VIJIMAMBO on September 22, 2016 / comment : 0 ACT Wazalendo, CCM, CHADEMA, CUF, Habari, jeshi la polisi, UKAWA
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Jeshi la polisi nchini limeondoa marufuku ya mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kwa madai kwamba limeridhishwa na hali ya kiusalama iliyopo nchini.
Hata hivyo, Kamishna wa operesheni na mafunzo, Nsato Marijani amesisitiza kwamba maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa bado imezuiliwa isipokuwa kwa wabunge katika majimbo yao.
Ametoa wito kwa vyama vya siasa na wananchi wote kuheshimu sheria za nchi na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuimarisha usalama wa raia na mali zao
"Maandamano na mikutano ya hadhara imezuiliwa hadi tathmini pana zaidi ya hali ya usalama itakapofanyika," amesema Marijani.
Chanzo: Mwananchi
CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHASEMA UCHUMI WA NCHI KWA KIPINDI CHA MIEZI SITA UMEPUNGUA KWA ASILIMIA NNE
By: VIJIMAMBO on September 06, 2016 / comment : 0 ACT Wazalendo, Matukio, Zitto Kabwe
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kabwe Zitto (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho baada ya kufanyika kikao chake cha kawaida jana. Kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho, Juma Sanani na kulia ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Shaban Mambo.
Taswira meza kuu. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho, Juma Sanani , Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Shaban Mambo, Makamu Mwenyekiti Tanzania Zanzibar, Ramadhan Ramadhan na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Msafiri Mtemelwa.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA Cha ACT Wazalendo kimesema katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Dk. John Magufuli uchumi wa nchi umepungua hadi kufikia asilimia nne ukilinganisha na vipindi vingine vilivyopita.
Hayo yamebainishwa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto Dar es Salaam leo wakati akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho kuhusu hali ya nchi baada ya kikao cha kawaida kilichofanyika jana.
Kabwe alisema katika miaka 10-15 iliyopita, nchi yetu imejenga uchumi ambao umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6-7 kwa mwaka katika kipindi chote hiki. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na juhudi za nchi katika kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Alisema awamu ya tano ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi imerithi changamoto ya uchumi unaokua bila kuwafaidisha wananchi wa kawaida. Hili ndilo tulitegemea Serikali mpya ishughulike nalo.
" Kamati kuu yetu imeshtushwa na hali ya kuanza kudorora kwa shughuli za uchumi katika kipindi cha miezi kumi ya utawala wa awamu ya tano" alisema Kabwe
Akitolea mafano alisema taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake (Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba?- Desemba 2015) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari - Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%. Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%!?
Alisema shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita. Hii inamaanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama Mapinduzi iingie madarakani.
Aliongeza kuwa ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 ulikuwa ni 13.8% lakini ukuaji wa sekta hiyo katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.
"Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama ntilie wanaowauzia chakula" alisema .
Alisema kwa kuzingatia mwenendo wa hali ya uchumi katika nchi, kaamati kuu ya chama hicho wanaitaka serikali izingatie ‘’sayansi ya uchumi’’ katika kuendesha uchumi wa nchi. Uamuzi wa CCM wa kuitelekeza serikali yake kwa mwanasiasa mmoja anayedhani ndiye anayejua kila kitu na yeye kugeuka kuwa mshauri wa washauri wa uchumi badala ya washauri wa uchumi kumshauri yeye, itasambaratisha uwekezaji nchini na kuua kabisa juhudi za miaka 20 za kuvutia wawekezaji na kujenga uchumi shirikishi.
Alisema kamati hiyo inahimiza wananchi kuzingatia kuwa msingi wa uchumi wetu ni uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Msingi wa kuvutia wawekezaji ni utawala wa sheria. Juhudi za serikali ya CCM za kuua utawala wa sheria zitaua uwekezaji na kuangamiza uchumi wa nchi. Tusiruhusu CCM iue uchumi wa nchi kwa maslahi yake ya kisiasa na viongozi wake.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG

WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendesha warsha kwa njia ya mtandao pamoja na mafunzo ya ana kwa ana kwa w...
-
N a Mwandish wetu, Dar es Salaam. CHAMA cha Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN) kimeshukuru uamuzi wa serikali ya kuwapatia mafunzo maalumu ya...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Huma...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE

MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014