HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

SERIKALI MKOANI MBEYA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KISHERIA ASKARI POLISI WANAOTUHUMIWA KWA WIZI WA DHAHABU CHUNYA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo katika mgodi wa dhabau wa Itumbi kata ya Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Februry 2 mwaka huu.


Na EmanuelMadafa,Mbeya

Serikali Mkoani Mbeya imeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya askari Polisi wanao tuhumiwa kuhusika  na ubebaji wa mawe ya dhahabu katika shughuli za uokoaji wa wachimbaji waliofukiwa na kifusi mwezi February mwaka huu Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Hatua hiyo inakuja  kufuatia baadhi ya wachimbaji madini wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Itumbi Kata ya Matundas Wilayani Chunya kutoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla, ambaye alifika katika eneo hilo kujionea hali halisi ya maafa hayo, ambapo inaelezwa kuwa zaidi ya wachimbaji wadogo 25  katika mgodi wa dhahabu wa Itumbi,walifukiwa na kifusi na kusababisha majeruhi na vifo vya watu wanne, mwezi February mwaka huu.

Wachimbaji hao walidai mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwa    baadhi ya askari polisi ,walishindwa kutekeleza wajibu wao katika   kufanya kazi ya uokoaji wa watu na mali zao, badala yake wao walikimbilia kubeba mawe ya dhahabu ambayo yalikuwa tayari yamechimbwa na wachimbaji hao, kisha kuyapakia kwenye gari ya polisi na kuyasafirisha mahala pasipojulikana.

 Wachimbaji hao, walimweleza Makalla kuwa askari hao ambao wanadaiwa kuwa si waadilifu, wao waliendelea na shughuli ya ubebaji wa mawe ya dhahabu ambayo yalikuwa yamechimbwa na wachimbaji na yapo nje yakisubili kuchenjuliwa ili kupatikana madini aina ya dhahabu.

 Aidha, kutokana na malalamiko hayo, Makalla aliwataka wananchi pamoja na wachimba madini hayo kuwa watulivu na wapole, kwa kuwahakikishia kwamba serikali italishughulikia suala hilo na kuwachukulia hatua baadhi ya askari watakaothibitika kuhusika na tuhuma hizo.

MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA KUWAONDOA WALIOVAMIA MAENEO YA HIFADHI


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na waanchi wa kijiji Cha Hanzya Kata ya Itagano jijini Mbeya katika kilele cha Kampeni ya Upandaji Miti Kimkoa .

Na Emanuel Madafa,Mbeya 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya.

Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la kudhibiti shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60 kwa kufuata sheria ya mita 60.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika kilele cha upandaji miti kimkoa katika eneo la chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.

Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa mazingira katika maeneo yot.

"Nikazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli za kibInadam"Alisema Makala.

Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo vya maji kwani ni muhimu kwa maisha ya kila siku.

"Serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1 kwa mwaka katika kila halmashauri mkoani humo ambapo mwezi juni mwaka huu kufanyika tathimini ya pamoja kuona zoezi hilo lilipo fikiwa"Alisema .

Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara baada ya kutembelea safu ya Mlima huo.
Wananchi wa kijiji cha Hanzya kata ya Itagano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika kilele cha Upandaji Miti Kimkoa katika SAFU ya Mlima Mbeya January 31 ,2017.
Afisa habari na Mawasiliano Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA)akichukua matukio katika tukio hilo la kilele cha upandaji miti kimkoa katika safu ya Mlima Mbeya Itagano. 
Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipanda mti katika kilele cha Upandaji kimkoa katika chanzo cha Maji Hanzya Kata ya Itagano. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kushoto akiteta jambo na Meya wa jiji la Mbeya David Mwashilindi mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika Safu ya Mlima Mbeya eneo la Chanzo cha maji cha Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya. 
Askari wa JKT Itende Mbeya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA) na baadhi ya watumishi halmashauri ya jiji la Mbeya wakiendelea na zoezi la upandaji miti katika Safu ya Mlima Mbeya katika Chanzo cha Maji Hanzya Itagano Jijini Mbeya .Picha Fahari News na JamiiMojablog. 

RC MAKALLA AISHUKURU UN KWA MISAADA NA USHIRIKIANO KWA SERIKALI YA TANZANIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa kwa misaada na ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo huduma kwa kambi za wakimbizi, Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye kauli mbiu ya Vijana - Fursa na misaada mingi katika shughuli za maendeleo Hayo ameyasema wakati wa mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake. RC Makalla amewahakikishia ushirikiano zaidi kwa mradi wa Vijana kutambua fursa na kuzitumia utakaotekelezwa Mkoa wa Mbeya mwakani. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati alipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akielezea mipango aliyonayo ya kuinua uchumi wa mkoa wake na kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekua changamoto kubwa nchini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyemtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa taarifa zilizomo kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi rasmi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kulia) nje ya jengo la ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na "Orange car" ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia: 'Elimu kwa wote" nje ya ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo jijini Mbeya.

MKUU WA MKOA WA MBEYA, AMOS MAKALLA APIGA MARUFUKU MIKUTANO YA OPERESHENI UKUTA ILIYOTANGAZWA NA CHADEMA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amepiga marufuku mikutano ya Operesheni Ukuta iliyotangazwa kuratibiwa na Chadema kuanzia Septemba Mosi. 

Akizungumza katika kikao cha kazi kilichoshirikisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, Makalla alitangaza kupiga marufuku mkutano wowote utakaofanyika chini ya utaratibu unaoitwa Operesheni Ukuta. 

“Bila shaka wananchi wa Mbeya wanataka amani na kazi, hivyo ni marufuku kufanyika mkutano wowote wa kisiasa unaoandaliwa kwa kushirikiana na watu wengine kutoka nje ya mkoa,” alisema Makalla aliyewahi kuwa mbunge na mweka hazina wa CCM.

Alifafanua kuwa wabunge na madiwani akiwamo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) wa Chadema wanaweza kufanya mikutano yao bila wasiwasi katika maeneo yao.

 Makalla alisema vyombo vimewekwa tayari kuwashughulikia kwa nguvu zote watakaokaidi maagizo yanayotolewa na kutoa mwito kwa vijana wa mkoa huo kuwafichua watu wenye njama zozote zikiwamo za kuwahamasisha kufanya maandamano au mikutano. 

Polisi yadai kukamata vijana 
Wakati Makalla akipiga marufuku Operesheni Ukuta, Polisi mkoani Mbeya wameeleza kuwakamata vijana wawili wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema kwa tuhuma za kuandaa na kusambaza ujumbe wa sauti wenye kauli za kutaka ofisi za CCM zichomwe moto. 

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Dhahir Kidavashari alidai kwamba vijana hao waliandaa na kusambaza ujumbe huo Julai 29 ukiwataka vijana wenzao ambao ni wanachama wa chama hicho kwenda kuchoma moto ofisi za CCM mahali walipo. 

Kidavashari alidai kwamba ujumbe huo unahamasisha vijana kufanya uhalifu huo wakati wowote kabla ya Septemba Mosi na baada ya hapo ilimradi nchi iwe kwenye machafuko. 

“Baada ya kufuatiliwa na kumkamata, mtuhumiwa wa kwanza alipekuliwa na kukutwa na simu ambazo zilitumika kusambaza ujumbe huo.Pia kupitia mtuhumiwa huyo tulifanikiwa kumpata mtuhumiwa mwingine.”

MAKALLA ATOA SIKU SABA KUONDOKA KWA MALORI YOTE YA MIZIGO JIJINI MBEYA YANAYOEGESHWA KINYUME NA TARATIBU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Amos Makalla ametoa siku saba kwa Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuyaondoa magari yote ya mizigo yanayoegeshwa pembezoni mwa Barabara kuu kinyume na utaratibu wakati kuna vibao vinaeleza ni marufuku magari ya mizigo kuegeshwa maeneo hayo." Siwezi kuendelea kuona magari yamejazana hapa kuna vibao vinakataza lakini watu hawatii, madiwani mpo, viongozi mpo, Takataka zinazagaa Watendaji Mpo, Viongozi Tupo kuanzia leo Usafi wa Jiji letu ni Sehemu ya kipaumbele na kwa kuanzia magari yote ya mizigo ndani ya wiki moja yaondoke yapelekwe eneo lililotengwa "

Hayo ameyasema jana katika kikao cha pamoja na madiwani na watendaji wa jiji la Mbeya wakati wa kujadili Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Serikali (CAG) Kuhusu ukusanyaji wa Mapato amewataka Watendaji na Madiwani kudhibiti Mapato kwa kuhakikisha Mapato yote yanakusanywa kwa njia ya (Elektroniki). Aidha amewataka madiwani kukagua miradi ili miradi hiyo iliyojengwa ieandane na Thamani ya Fedha.

Baadhi ya madiwani na watendaji wa jiji la Mbeya wakifuatilia kwa makini mkutano.
Wapili Kutoka Shoto ni Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Mh. Amos Makalla, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mh. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu) Katika picha ya pamoja baada ya Mkutano Kumalizika.