HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKABIDHIWA VIFAA TIBA VYA UZAZI ZAIDI YA 200 NA BALOZI WA KUWAIT HAPA NCHINI

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akitazama moja ya Dawa,mara baada ya kukabidhiwa mapema leo Ikulu jijini Dar,vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 na Balozi wa Kuwait hapa nchini,Mhe,Jasem Al-Najem,vifaa hivyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 ambavyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makabidhiano ya vifaa hivyo vya uzazi yamefanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam ambapo Balozi wa Kuwait hapa Nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya nchi hiyo imetoa vifaa hivyo kama hatua ya kuendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Amesema kuwa Serikali ya Kuwait imetoa vifaa hivyo ikiwa ni awamu ya kwanza na lengo ni kutoa vifaa hivyo zaidi ya 1000 vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa wanawake wajawazito na waliojifungua katika hospitali mbalimbali nchini.

Mara baada ya kupokea msaada huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada huo ambao utasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema msaada huo utasaidia sana wanawake wajawazito na waliojifungua kupata vifaa za uzazi ambavyo vinahitajika wakati wanamke mjamzito anapojifungua na baada ya kujifungua.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitaanza kusambazwa kuanzia mwezi huu na mchakato wa kuainishwa hospitali zitakazopata msaada huo unaendelea.

Makamu wa Rais pia amesisitiza kudumishwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi ya Kuwait na Tanzania kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili.

Aidha Balozi huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serakali ya Kuwait itaendelea kusaidia Serikali ya Tanzania katika uimarishaji wa sekta ya afya na elimu nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za msingi


WAZIRI MAHIGA AFUNGUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA 69 YA UHURU WA ISRAELI, DODOMA.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 69 ya uhuru wa Taifa la Israel iliyofanyika kwenye Hoteli Morena Mjini Dodoma 
Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo ya Taifa unakipigwa kweye maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel 
Balozi wa Israeli nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Yahel Vilan akizunguza kwenye hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel iliyofanyika mjini Dodoma 
Mhe. Balozi Vilan akisisitiza jambo 
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akihutubia hadhira iliyo shiriki hafla hiyo 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani (Mwinyi kulia) akifuatilia jambo, kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima 
Picha ya pamoja 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga jana alifungua hafla ya maadhimisho ya 69ya uhuru wa Taifa la Israeli yaliyo fanyika mjini Dodoma katika Hoteli ya Morena.

Hafla hiyo ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Taifa hilo na uhusiono mzuri wa kidiplomasia  baina ya Tanzania na Israeli yaliratibiwa na Ubalozi wa Israel wenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya.  Waziri Mahiga akizungumza katika hafla hiyo aliupongeza Ubalozi wa Israel kwa uamuzi wake wa kufanyia hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wao, Makao Mkuu ya Serikali mjini Dodoma.

 Waziri Mahiga aliongeza kusema Mataifa haya mawili Tanzania na Israel yana mahusiano mazuri ya kidiplomasia, ikidhihirishwa wazi na idadi kubwa ya raia wa nchi hizi mbili kutembeleana na kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo utalii. Aidha Mahiga aliipongeza Serikali ya Israel kwa hatua kubwa ya maendeleo waliyofikia katika maeneo mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia na kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali.  

Balozi wa Israeli nchini Mhe. Yahel Vilan mwenye makazi yake Jijini Nairobi, Kenya akitoa hotuba yake alisema Ubalozi wa Israeli umechukua maamuzi ya kufanyia hafla hiyo Mjini Dodoma ikiwa nikuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma. Aliongeza kusema kuwa hafla hiyo ni ishara ya Israel kuanziasha Ubalozi wake nchini Tanzania. 

Balozi Vilan ameihakikishia serikali ya Tanzania kuwa Israel itaendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Taifa katika maeneo ya kilimo, afya, elimu, sayansi na teknolojia na usalama.Israeli ilifungua kituo cha kushughulikia masuala ya viza nchini Tanzania tarehe 3 Novemba, 2016.


Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia atumia Sikukuu ya Muungano kutangaza Utalii

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, kushoto akifurahia jambo katika Sikukuu ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa nchini humo kwa kukutanisha Watanzania wanaoishi Saudi Arabia, wazawa na viongozi mbalimbali kama sehemu ya kuitangaza vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.

Na Mwandishi Maalum, Riyadh Saud Arabia
SHEREHE za Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimetumika kama sehemu ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tukio maalum lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wan chi hiyo.

Akizungumza hivi karibuni katika sherehe hizo za Sikukuu ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji kutokana na sera zake nzuri pamoja na dhamira njema za viongozi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa Tanzania Bara pamoja na Dr Ali Mohamed Shein kwa upande wa Visiwani Zanzibar.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza wa nane kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali katika maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kusherehekea pamoja katika siku hiyo muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.
Balozi Mgaza akiwa na mgeni rasmi Prince Muhammad bin abdullahman wakikata keki ya sherehe.
Balozi Mgaza kushoto akikata keki
Balozi Mgaza akihutubia katika hafla hiyo

Alisema kutokana na sera hizo pamoja na kusimamia vyema rasilimali za utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga mbalimbali za wanyama ni sehemu thabiti ya utalii kwa wageni, wakiwamo wananchi wa Saudi Arabia.

“Nchi yetu ina mbuga za wanyama 16 ambazo zimekuwa zikitunzwa na kuhifadhiwa vema kama sehemu ya kuhakikisha kwamba rasimali hiyo inakuza uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nchi yetu ina wakaribisha wote kutembelea kujionea mambo mbalimbali yanayovutia katika utalii pamoja na kuwekeza katika sekta muhimu zikiwamo za viwanda ambazo ndio agenda kuu kwa sasa nchini mwetu,” Alisema Balozi Mgaza.

Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeadhimishwa wiki iliyopita Aprili 26 ambayo hutumiwa kama kioo cha kuangalia matunda yanayojitokeza kutokana na Muungano huo kati ya Tanzania Bara na Visiwani.

Taarifa Potofu Zinazomuhusisha Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dr Asha Rose Migiro

Ubalozi wa Tanzania London umepokea Habari inayozagaa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa instagram ikiwa na nukuu ifuatayo:


''Binafsi bado sijaona umuhimu na mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zaidi ya vingozi kujikusanyia mali na utajiri mkubwa sambamba na kung'an'gania madaraka kwa nguvu. Mfano uchaguzi uliofanyika mwaka 2015 kwa yaliyotokea Zanzibar ni miongoni mwa Athari mbaya kabisa zinazotokona na Muungano,nadhani kila Mtanzania aliyaona"

Ukurasa huo wenyewe jina la UKUTA inaihusisha nukuu hiyo na jina la Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro. 

Ubalozi wa Tanzania London unapenda kutumia fursa hii, kuwajulisha Watanzania Waishio Uingereza na Watanzania kwa ujumla kuwa Balozi Migiro ahusiki na nukuu hiyo kama inavyosambazwa.Hivyo ni wazi kuwa wanayoisambaza wana malengo ya kulichafua jina la Balozi Migiro kwa sababu wanazozijua wao. 

Ubalozi wa Tanzania London unaendelea kutoa wito kwa Watanzania Waishio Uingereza kutumia muda wao na mitandao ya kijamii kutoa mawazo chanya yatakayo imarisha Muungano wa Taifa letu na mustakabali wa maendeleo ya Nchi yetu na Watanzania wa pande zote za Muungano. 

Ubalozi wa Tanzania London 
29 Aprili 2017.

WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WATINGA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo siku ya Jumatatu April 24, 2017 wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika picha toka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Swahiba Mdeme,Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania na Canada Col. Adolph Mutta, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa A. Ghasia, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi, Mbunge Mhe. Janeth Z. Mbene, Mhe. Josephat S. Kandege, Afisa wa Ubalozi Bwn. Dismas Assenga na Afisa wa Bunge Bwn. Godfrey Godwin. Wabunge hao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania walikuja Washington, DC kuhudhuria mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika picha toka kushoto ni Afisa wa Bunge Bwn. Godfrey Godwin, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa A. Ghasia, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi, Mbunge Mhe. Janeth Z. Mbene, na Mhe. Josephat S. Kandege.

BALOZI WA MSUMBIJI AKUTANA NA TCCIA KUIMARISHA MAHUSIANO YA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI

Balozi wa Msumbiji nchini Bi Monica Patricio Clemente akizungumza na viongozi wa TCCIA walioongozana na Makamu wa Rais-Viwanda Bw. Octavian Mshiu wa kwanza kulia, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Gotfrid Muganda pamoja na viongozi wa TCCIA Mtwara Bw. Swallah S. Swallah-Mwenyekiti na Muhidin Swalehe. 

Mkutano huo ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa TCCIA mwenye dhamana ya Viwanda Bw. Octavian Mshiu akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Bw. Gotfrid Muganda pamoja na viongozi wa TCCIA Mkoa wa Mtwara Bw. Swallah S. Swallah ambaye ni Mwenyekiti na Bw. Muhidin Swalehe- Afisa Mtendaji.Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa TCCIA- Viwanda Bw. Octavian Mshiu amesema mapendekezo ambayo TCCIA imewasilisha kwa Balozi wa Msumbiji nchini yanalenga kutoa ushirikiano wa karibu kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambao utawezesha uanzishwaji wa vituo katika mkoa wa Mtwara ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na misaada ya haraka kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili.
Makamu wa Rais wa TCCIA-Viwanda Bw. Octavian Mshiu akimkabidhi Balozi Monica Clemente nyaraka maalum baada ya mkutano na Balozi huyo ofisini kwake mapema wiki iliyopita.

Balozi Bi. Monica Patricio Clemente amesema amefurahishwa na ugeni alioupata wa uongozi wa TCCIA na kwamba mapendekezo chanya yaliyoletwa na TCCIA yana nafasi sahihi na muhimu katika kuboresha ushirikiano wa wafanyabiashara wa Mtwara na Mikoa jirani ya Msumbiji kwani mahusiano ya aina hiyo yana nafasi kubwa ya kunufaisha jamii ya wafanyabiashara, kuongeza pato la nchi zote mbili na pia kukuza uchumi wa maeneo husika.
Balozi Monica ameahidi kuyafanyia kazi majadiliano na mapendekezo ya TCCIA kwa haraka ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa mikoa inayofanya biashara pamoja ambayo matokeo yake yataleta tija kwa maslahi ya Tanzania na Msumbiji kwa ujumla
Viongozi wa TCCIA wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa Msumbiji nchini baada ya mkutano wa Balozi na uongozi wa TCCIA jijini.

Katika mkutano huo wajumbe kutoka ubalozini humo wamesema moja ya changamoto kubwa inayowakumba wafanyabiashara wengi ni lugha ambapo wamependekeza pia kuwepo kwa vituo maalum ambavyo vitakuwa vikitoa elimu ya lugha kwa wafanyabiashara hao ili kuondoa changamoto hiyo.Mwenyekiti wa TCCIA Mtwara Bw. Swallah S. Swallah ameshukuru ubalozi wa Msumbiji kwa ukarimu na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya wafanyabiashara wa Cape Delgado nchini Msumbiji na Mtwara nchini Tanzania. Pia alieleza juhudi za Chemba ya Mtwara katika kukabiliana na changamoto ya lugha na kwamba mjini Mtwara tayari kuna kituo kikubwa cha lugha kinachofundisha watanzania lugha mbalimbali ikiwemo Kireno ambacho sasa kinatiliwa mkazo zaidi.
Viongozi wa TCCIA wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa Msumbiji nchini baada ya mkutano wa Balozi na uongozi wa TCCIA jijini.

MHESHIMIWA BALOZI WILSON MASILINGI, AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA MHESHIMIWA ENRIQUE PEÑA NIETO, RAIS WA MEXICO.

Tarehe 11 Aprili, 2017, Mhe. Balozi Wilson Mutaganywa Kajumula Masilingi aliwasilisha hati za utambulisho kwa Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico, Ikulu Katika Jiji la Mexico. Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Mexico na mke wa Mhe. Balozi, Marystella Masilingi. 
Wakati wa kuwasilisha hati hizo, Mhe. Balozi alipata fursa ya kuongea na Mhe. Rais wa Mexico na kumpa salam kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico akimpokea Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mexico. Katikati akitizama ni Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico.
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico na Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, nchini Mexico.
Kutoka kushoto, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi na Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico; Mke wa Balozi Bi. Marystella E. Masilingi na Mhe. Luis Videgaray, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico.
Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi na Mke wake Bi. Marystella Masilingi (kulia) na Bi. Swahiba Mndeme, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi (kushoto)

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. YAHEL VILAN, IKULU, DAR ES SALAAM LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu toka kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu uliowasilishwa kwake na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza baada ya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan baada ya kutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.

PICHA NA IKULU

DK. MENGI AKARIMU WAFARANSA SERENA HOTEL

MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini.

Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro.

Akizungumza kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi alisema katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza.

Alisema jioni hii ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hao ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)

“Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili.

Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia.

Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi.

Aliwatakia wageni wake chakula chema.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni aliyoiandaa maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena jijini Dae es Salaam.

Mgeni rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano.

“ …Business and friendship goes Together..” alisema balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si wa kubahatisha unakua.

Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwenye 'cocktail' kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Eng. Raymond Mbilinyi (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika halfa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville (katikati) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga katika hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga (kushoto) akielezea jinsi 'Application' ya ITV Tanzania inavyofanya kazi kupitia simu za viganjani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville.
'Meet and Greet' ikiendelea kwa wenyeji na wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji mkongwe nchini Mzee Zahir Ally Zoro akitumbuiza kwenye hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meza kuu kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi wa ufaransa Bi. Beatrice Alperte, mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi pamoja na Mshehereshaji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akisherehesha wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk Mengi kwenye hoteli Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiteta jambo na mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa wakijumuika na wenyeji wao katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde alikuwa miongoni mwa wageni waaalikwa katika hafla hiyo.

BALOZI WA ISRAEL MHE. YAHEL VILAN ATEMBELEA IDARA YA URATIBU WA MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU -DODOMA

 Balozi wa Israel Nchini Mhe. Yahel Vilan akiongea jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 4, 2017 Dodoma.
 Mwambata Jeshi wa Israel Barani Afrika Bw. Aviezer Segal akionesha michoro ya muundo wa Ofisi yake wakati wa ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Idara ya Maafa ili kuangalia eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa na Kimataifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Dodoma.
 Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akionesha muundo wa Idara hiyo wakati wa ziara ya ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Aprili 4, 2017.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza mwenye miwani) akifuatilia mada ya muundo wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan Dodoma.
 Wakala wa Maendeleo wa Kimataifa wa MASHAV Bw. Yuval Fuchs akitoa hoja wakati wa Ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan kwa Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Waziri Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi wa wageni walioambatana na Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 4, 2017 Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idaya ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Brig. Jenerali, Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto) akimuonesha Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan ramani ya  eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa na Kimataifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya Watendaji wa Serikali walioshiriki katika ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan mara baada ya kumpokea Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)