HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

SAMIA ATAKA KASI KUONGEZA UWEKEZAJI

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi.

Alisema mwaka wa kwanza wa serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya kukuza uchumi. 

Alisema serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa kati. 

Makamu wa rais ambaye katika hotuba yake alikuwa anazungumzia changamoto zinazoikumba sekta binafsi katika kutekeleza wajibu wake, amesema kwamba serikali ya awamu ya tano inatambua changamoto hizo na imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba zinamalizwa.

Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama bandari na reli na pia kuwapo kwa kamati inayoangalia kero zinazosumgua sekta ili serikali ifanye maamuzi.

Kwa sasa kuna kamati inayoangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara inayofanyakazi Wizara ya Viwanda na inakaribia kumaliza kazi yake na kuikabidhi serikalini. 

Akizungumza kumkaribisha Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji ili amkaribishe Makamu wa Rais kuzungumza na washiriki katika hafla hiyo,Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Shabbir Zavery alitaja changamoto tisa zinazotia msukosuko ukuaji wa viwanda nchini. 

Moja ya changamoto hizo ni mabadiliko ya mara kwa mara na ya ghafla ya sera au sheria za kibiashara ambayo huondoa utulivu kwa wazalishaji. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akirejea kwenye meza kuu baada ya kuhutubia wageni waalikwa kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Zavery alisema kwamba ufanisi na utuilivu wa kufanya biashara unategemea sana kutobadilika mara kwa mara kwa sheria na sera za biashara na mwaka uliopita serikali ilichukua maamuzi kadhaa bila kuhusisha sekta binafsi na hivyo kudhoofisha ushirikiano baina ya serikali na wafanyabiashara. 

Pia alisema kwamba utitiri wa mamlaka za udhibiti na tozo zao mbalimbali pia kufanyakazi zinazofanana na kutembelea viwanda kwa kila mamlaka kwa wakati wake kunachangia gharama za kufanyabiashara. 

Akizungumzia tatizo sugu la wenye viwanda na wafanyabiashara kutorejeshewa malipo stahiki (Vat na nyinginezo) wanazodai kutoka Mamlaka ya Kodi, na kodi zinazoua ushindani,Makamu wa Rais Samia amesema kwamba serikali kwa sasa imeshatulia na kwamba itaendelea kufanya marejesho kwa mujibu wa sheria na suala la kodi limeshafanyiwa maelekezo na kwamba wahusika wanatakiwa kukutana kushughulikia tatizo hilo. 

Aidha ameiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha kwamba utekelezaji wa mikakati ya kupunguza kero kwa wawekezaji na wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo. 

“Nafahamu kuwa sekta ya viwanda imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali. Serikali tunaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha viwanda vyetu vinakuwa katika mazingira rafiki na wezeshi ili kuwaongezea ufanisi na ushindani katika masoko ya kimataifa” alifafanua Makamu wa Rais. 
Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa CTI, Shabbir Zavery akisoma risala ya Mwenyekiti wa CTI kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Rais alikumbushia maneno aliyotoa katika ziara zake mikoani kwa taasisi za serikali na sekta binafsi kukaa, kujadili na kuona namna ya kuondoa adha katika uwekezaji na ufanyaji biashara bila kuipotezea mapato serikali. 

Aidha alisema kwamba wakati serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuondoa changamoto zinazoathiri ukuaji wa sekta ya viwanda, ni muhimi pia kwa wawekezaji na wazalishaji kutambua majukumu yao katika kuchangia juhudi hizo. 

Alisema majukumu hayo ni pamoja na kuzalisha bidhaa nyingi, zenye ubora na zenye bei rafiki kwa mlaji. 

“Tusisahau kuwa sekta ya viwanda ina jumkumu kubwa sio tu la kuipatia serikali mapato; bali pia kutoa ajira kupunguza umaskini pamoja na kuijengea nchi heshima kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani wa kimataifa” alisema Makamu wa Rais. 

Aliiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuratibu na kukutana na wizara au taasisi za serikali na za umma nchini ili kuwahamasisha kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kama ilivyoanza kwa vikosi vya usalama ambapo wanatakiwa kununua bidhaa zao hapa nchini. 

Pia amewataka wafanyabiashara kuingia ubia na mifuko ya jamii ili kuwa na mitaji itakayowezesha kuanzisha viwanda kwa pamoja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga alipokuwa akiwatambulisha wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan kuzungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Nalo shirikisho hilo la viwanda limepongeza uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano kwa kufanya uwekezeji mkubwa katika sekta za kiuchumi zinazotengeneza njia kuelekea katika uchumi wa viwanda. Wametaja uwekezaji huo kuwa katika umeme, barabara,reli, maji na bandari. 

Katika risala ya CTI kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya utoaji Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016, wamesema uwekezaji huo utasaidia kushuka kwa gharama za uzalishaji na hivyo kuongeza ushindani wa wazalishaji wa Tanzania katika soko la ndani na la nje. 

Akisoma risala hiyo kwa Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa Shabbir Zavery, alisema, pamoja na mafanikio katika miundombinu uwekezaji uliofanywa katika elimu utasaidia kutoa wataalamu wengi wenye tija katika sekta ya viwanda ambayo inategemea kukua kwa kasi katika kipindi kifupi kijacho. 

Aidha alisema pamoja na changamoto zinazokabili sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji taifa katika awamu ya tano imeshuhudia kukua kwa pato la taifa kwa asilimia 6.75; kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 5.6 mwaka 2015 ukilinganisha na wastani wa asilimia 5.2 mwaka 2016. 
Mafanikio mengine aliyoyaeleza Zavery ni kuongezeka kwa mauzo ya nje ambapo jumla ya dola za Marekani bilioni 9.38 zilipatikana ukilinganisha na dola za Kimarekani bilioni 8.92 zilizopatikana mwaka 2015.Likiwa ni ongezeko la asilimia 5.2. 

Aidha katika Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mazingira Bora ya Biashara ya mwaka 2016 Tanzania ilishika nafasi ya 139 ikilinganishwa na nafasi ya 140 mwaka 2015. 

“Vile vile usimamizi mzuri wa mapato ya serikali umewezesha kuongezeka mapato ya serikali kila mwezi kufikia zaidi ya shilingi trilioni moja ikilinganishwa na shilingi bilioni 900 zilizokusanywa mwaka 2015” alisema. 

Alisema hata hivyo pamoja na mafanikio hayo ambayo yamepatikana katika kipindi kifupi, kuna changamoto ambazo kwa kiasi zinapunguza kasi ya mafanikio. 
Mkurugenzi wa Ishara Consultants Ltd, Isaac Saburi, akitoa maelezo mafupi ya vigezo vilivyotumika kuwapata washindi wa Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 kwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo. 

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na mazingira yasiyo rafiki kwa kufanyabiashara yanayochangiwa na mabadiliko ya ghafla katika sera na sheria zinazohusiana na biashara. 

Changamoto nyingine ni utitiri wa kodi na tozo , kutorejeshewa malipo stahiki ya kodi ya ongezeko la thamani,ushindani unaozuiwa na kodi ya VAT kwa mali ghafi, upungufu wa makaa ya mawe,vibali vya kazi na bomoa bomoa inayofanywa na kampuni ya reli isiyofuata sheria. 

Zavery aliomba serikali kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo ili azma ya kuwa na Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2020 inafanikiwa. 

Katika juhudi za kuhakikisha kwamba kero zinashughulikiwa CTI imeandika waraka ambao umewasilishwa Wizara ya Viwanda ili kurahisisha ukuaji wa sekta ya viwanda nchini. 

Katika hafla hiyo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji , Mh. Charles Mwijage alisema kwamba wataendelea kushirikiana na CTI kuhakikisha kwamba vikwazo hivyo vinaondoka. 

Alisema ipo mikakati ya kukabiliana na hali hiyo hasa utitiri wa mamlaka na kodi ili kuhakikisha kwamba viwanda vipya vinaongezeka na vile vilivyopo vinashamiri. 

Alisema kwa mwaka 2015 hadi 2016 viwanda zaidi ya 2000 vimesajiliwa na mamlaka mbalimbali ikiwamo EPZ, SIDO, NDC na TIC. 

Amesema kwamba kwa sasa wizara yake imeweka mkakati mahsusi wa kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na katika hili wamepanga kukutana wafanyabiashara mjini Dodoma kutafakari changamoto mbalimbali. 
Meza kuu ya kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Katika tuzo hizo mshindi wa kwanza wa jumla alikuwa ni Tanzania Breweries Limited, akifuatiwa na Mufindi Paper Mills Company Limited na mshindi wa tatu alikuwa Kioo Limited. 

Aidha kulikuwa na washindi katika viwanda vidogo vya kati na vikubwa. 
Mshindi katika safu ya viwanda vidogo wa kwanza alikuwa Alliance Life Assurance Limited kwenye masuala ya fedha na bima na mshindi mwingine alikuwa ni Prisons Corporation Sole katika biadhaa za ngozi na viatu. 

Kwa viwanda vya kati katika hafla hiyo ambayo mdhamini wake mkuu ni Bank M, mshindi katika ujenzi alikuwa Dharam Singh Hanspaul and Sons Limited; safu ya kemikali mshindi alikuwa Royal Soap and Detergent Industiries Limited; katika nishati ,umeme na elektroniks mshindi alikuwa Tanalec Limited na katika usindikaji wa chakula mshindi alikuwa Chemi Cotex industries limited. 

Washindi wengine viwanda vya kati walikuwa Ital Shoe Limited katika bidhaa za ngozi na viatu; Chemi Cotex Industries limited katika bidhaa za metali ;Nyanza Mines (T) Limited katika bidhaa za madini; Hanspaul Automechs Limited safu ya magari na vifaa vyake; Tanpack Tissues limited bidhaa za karatasi na makasha na DPI Simba Limited katika safu ya bidhaa za plastiki. 

Kwa viwanda vikubwa washindi katika nafasi mbalimbali ni Tanzania Breweries limited, Petrolube T limited, Petrofuel T Limited, Alliance Insurance Corporation Limited, Said Salim Bakhressa, Alaf Limited, Kioo Limited, Mufindi paper Mills Company Limited, Jambo Plastics na Nida Textile Mills T Limited. 

Washindi wa tuzo hizo walipatikana kwa kuzingatia ufanisi katika uzalishaji, mauzo ya nje, uwekezaji katika teknolojia ya kisasa,matumizi bora ya nishati, utunzaji wa mazingira, afya na usalama wa wafanyakazi, uwiano wa kijinsia katika uongozi, pamoja na mchango katika jamii. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi cheti kwa niaba ya ITV na RADIO One kwa kutambua mchangao wao wa kurusha LIVE matangazo ya hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimakbidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline Woiso cheti kwa kutambua mchango wao kwa kuwa mdhamini mkuu wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Jacqueline Mengi cheti kwa niaba ya magazeti ya The Guardian Limited kwa udhamini wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo hizo, Teddy Mapunda kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (wa tatu kulia) akiwa amejumuika na marafiki zake, Nancy Sumari Neghesti (kushoto), Nasreen Kareem (kulia) pamoja na Fausta Kameja (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali nchini waliohudhuria hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage walipowasili katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ilipofanyika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakielekea katika ukumbi wa Marquee kwenye hoteli ya Serena jana jijini Dar es Salaam ilipofanyika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo kuhusu vifaa mbalimbali vya umeme kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi alipotembelea banda la maonesho la Kilimanjaro Cables linalomilikiwa na kampuni hiyo wakati wa kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly ndani ya banda la kampuni hiyo maarufu kwa utengenezaji wa samani za ndani kwenye kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akimsikiliza Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (aliyeketi) wakati akitoa maoni juu ya ubora wa samani hizo za ndani zinazotengenezwa na Kampuni ya Amorette Ltd inayomilikiwa na Bi. Jacqueline Mengi (hayupo pichani) katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga wakitia baraka kwenye banda la maonesho la Kampuni ya Amorette Ltd katika kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly (kulia) akiwa na wafanyakazi wenzake kwenye banda la maonesho wakati hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Hanspaul, Kamaljit Singh Hanspaul (kushoto) kabla ya kuanza rasmi kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (kulia) akifurahi jambo na rafiki yake Fausta Kameja katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo za CTI, Teddy Mapunda (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kushoto aliyesimama) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kulia) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mshehereshaji wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Bw. Innocent Mungy (wa pili kulia aliyesimama) akifafanua jambo kwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline Woiso (kulia) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi alipotembelea mabanda ya maonyesho katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly (wa pili kushoto) alipotembelea banda ya kampuni hiyo inayojishughulisha na utengeneza wa samani za ndani (Furniture). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (aliyepo pembeni ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi (wa pili kushoto) alipotembelea banda Kilimanjaro Cables wauzaji wa vifaa vya umeme ambao walieleza wako mbioni kufungua kiwanda cha kutengeneza Transfoma za umeme nchini na kuongeza ajira. Kushoto ni Meneja Utawala wa kampuni ya AFRiCAB Group, Kunajal Gina na Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Bodi ya CTI.

DK.MENGI ASISITIZA WATANZANIA KUONDOA UOGA

WATANZANIA wametakiwa kuingia katika ubia kama wajasiriamali badala ya kufikiria kwamba wao ni maskini na hawana fedha za kuingia ubia na makampuni ya nje. kauli hiyo imetolewa katika wiki ya Ufaransa ambapo makampuni 50 yanashiriki kuonesha uwezo wa utayari wa ushiriki wao katika ujenzi wa uchumi wa kati wa Tanzania unaotegemea viwanda.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi ambaye aliwasilisha haja na matamanio ya Watanzania kwenye sekta binafsi katika kushirikiana na wawekezaji kutoka Ufaransa, alisema watanzania wamekuwa waoga kuomba ubia wakidhani kwamba hawana kitu cha kutoa wakati wao wana akili na rasilimali.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akizungumza katika kilele cha wiki ya Ufaransa ambapo wawekezaji kutoka makampuni 50 ya Ufaransa walishiriki katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliombatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wafaransa. (Picha zote Thebeauty.co.tz)

Kauli hiyo ambayo aliisema kwenye mazungumzo na wawekezaji hao wa Ufaransa wakati akielezea utayari wa sekta binafsi kushirikiana na Wafaransa alisema kwamba watanzania wengi hawajiamini na kwamba wakati umefika kwa Watanzania kujitambua kwa kuwa wao (wafaransa) walijaribu wakaweza kwani kama sisi walikuwa na vitu vya ziada katika uthubutu wao. Katika mazungumzo yake Dk. Mengi akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema kwamba sekta binafsi ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi inawezekana kwa watanzania kuthubutu. Aidha alisema uwapo wa Wafaransa utaweza kusaidia kupandisha uwezo, teknolojia na utaalamu hali ambayo inawezekana kupitia uwapo wa shughuli za ubia kati ya wawekezaji wa Kitanzania na Wafaransa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye (kulia) akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

Alisema baada ya sekta ya umma kuweka miundombinu mahala pake, ni kazi ya sekta binafsi kutumia miundombinu hiyo kubuni na kuwekeza katika viwanda na kuzalisha bidhaa mbalimbali. Dk.Mengi alisema kwamba TPSF inaamini kwamba sekta binafsi ni ufunguo katika kuongoza na kuimarisha uchumi wa Tanzania ambao unatakiwa kuwa endelevu kama awamu ya tano inavyotaka. Aliwaambia wafanyabiashara wa Ufaransa kwamba Tanzania ina kila kitu wanachohitaji na kwamba makampuni makubwa ya Ufaransa kama Airbus, Renault, Alstrom, Systra wana mtandao mpana duniani wa kufanyabiashara na wawawekezaji wadogo duniani hivyo wanaweza kufanya hivyo hapa nchini. Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

Alisema changamoto za utaalamu zitaondoka kwa ushirikiano na uwezeshaji. Aliwataka wawekezaji hao wa Kifaransa kwamba Tanzania kwa sasa ndio nchi ya uwekezaji na kusema changamoto zilizopo ni fursa za uwekezaji nchini Tanzania hasa katika nishati ambapo taifa hili litahitaji megawati 10,000 ifikapo mwaka 2040.
Aidha alisema anaamini kwamba wengi wa watanzania wapo tayari kushirikiana na Ufaransa katika kuhakikisha kwamba wanaingia ubia katika biashara halali na yenye kusaidia pande zote. Naye Simbeye alisema anatamani kuona kwamba wafaransa wanawekeza kiwanda cha magari nchini kwani inawezekana kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa uwekezaji kwa sasa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo katika mkutano huo kwenye kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Mmoja kati ya wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa akiuliza swali kwa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) katika kilele cha mkutano wa wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi, Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira katika mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara walioshiriki mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Blevin Claude (wa pili kushoto) akiwa na Ofisa anayeshughulikia masuala ya Uchumi katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Beatrice ALPERTE (kushoto) katika mkutano huo. Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua masomo ya biashara walioshiriki mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wadau na wafanyabiashara kutoka makampuni 50 ya nchini Ufaransa walioshiriki mkutano huo. Mkutano ukiendelea. Sales Executive wa kampuni ya CMC Formula wauzaji wa magari ya Renault, Erica George akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati akitembelea mabanda katika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akipata maelezo katika banda la kampuni ya TOTAL. Meneja Mauzo wa Kampuni ya AIRBUS HELICOPTERS, Jean-Marc Royer (kulia), akitoa maelezo ya shughulli wanazofanya kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea mabanda ya kampuni mbalimbali kutoka nchini Ufarasan zilizoshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Ufaransa yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Kushoto ni Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude. Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude akitoa neno la shukrani kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati Dk. Mengi akijiandaa kuondoka katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yalipofanyika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa jijini Dar es Salaam.

DK. MENGI AKARIMU WAFARANSA SERENA HOTEL

MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini.

Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro.

Akizungumza kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi alisema katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza.

Alisema jioni hii ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hao ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)

“Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili.

Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia.

Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi.

Aliwatakia wageni wake chakula chema.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni aliyoiandaa maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena jijini Dae es Salaam.

Mgeni rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano.

“ …Business and friendship goes Together..” alisema balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si wa kubahatisha unakua.

Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwenye 'cocktail' kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Eng. Raymond Mbilinyi (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika halfa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville (katikati) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga katika hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga (kushoto) akielezea jinsi 'Application' ya ITV Tanzania inavyofanya kazi kupitia simu za viganjani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville.
'Meet and Greet' ikiendelea kwa wenyeji na wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji mkongwe nchini Mzee Zahir Ally Zoro akitumbuiza kwenye hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meza kuu kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi wa ufaransa Bi. Beatrice Alperte, mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi pamoja na Mshehereshaji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akisherehesha wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk Mengi kwenye hoteli Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiteta jambo na mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa wakijumuika na wenyeji wao katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde alikuwa miongoni mwa wageni waaalikwa katika hafla hiyo.