HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

SERIKALI YASISITIZWA KUONGEZA MASUALA YA MABADILIKO YA TABIANCHI KATIKA MIPANGO NA BAJETI

   Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akiwasilisha mada kwa wadau kutoka kwenye asasi za kiraia, maafisa mipango wa wizara mbalimbali pamoja na watafiti kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.

FORUMCC imeandaa mkutano na kukutanisha wadau kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya serikali kuu na serikali za mitaa hapa nchini Tanzania. 
Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na serikali ili kuangalia njia nzuri zinazoweza kusadia Tanzania kuwa na mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kupunguza kutegemea zaidi fedha kutoka kwa wafadhili.
Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau kujadili na kuhamasisha jitihada za kuingiza masuala ya mabadiko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya Serikali katika kipindi hiki tunapoelekea katika Bunge la bajeti ya mwaka 2017/18.
Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi  amesema serikali kupitia TAMISEMI iko karibu na wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza kupunguza majanga mbalimbali hapa nchini, na wao TAMISEMI wana jukumu la kubwa kwenye asasi za kiraia kuingia kwenye miradi inayohusu mabadiliko ya Tabianchi.
Pia Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona aliwaomba wadau mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo kushirikiana na FORUMCC ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea kwenye suala la mabadiliko ya Tabianchi linalotishia maendeleo ya jamii za mbalimbali na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) leo uliwakutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, maafisa mipango kutoka wizara mbalimbali, watafiti na waandishi wa habari. 
Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi akitoa mada kuhusu kazi za TAMISEMI pamoja na ushirikiano wake kwenye masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kumbi wa  COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali pamoja na kutoa maoni kwa maofisa wa wizara kuangalia namna ya kushirikiana ili kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Mkutano ukiendelea uliowakutanisha wadau mbalimbali uliowakutanisha ili kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
Mtaalamu wa Masuala ya Nishati, Erneus Kaijage akiwasilisha mada kuhusu uwekezaji wa fedha katika sekta ya nishati kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi leo jijini Dar es Salaam

 Baadhi ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi  wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi  akijibu maswali yaliyokuwa yanaulizwa na wadau mbalimbali wa masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliowakutanisha wadau hao kwenye ukumbi wa Chuo cha Sayansi jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau mbalimbali waliokutana ili kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
Mwezeshaji wa Mkutano wa FORUMCC, Abdallah Henku akizungumza jambo kwenye mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki kutoka asasi za kiraia, maafisa mipango kutoka wizara, watafiti na waandishi wa habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea kwenye ukumbi wa  COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) mkutano ulipofanyika leo ulioandaliwa na FORUMCC.
Picha ya Pamoja

Wadau wajadili upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Wadau wa mazingira wamekutana mjini Bagamoyo kujadili changamoto za upatikanaji wa fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya kilimo nchini. 

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Forumcc, Oxfam, Care-Tanzania, ACSAA, FAO na IUCN ulilenga kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kupata fedha kutoka katika Mfuko wa Fedha za Kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi (GCF).

Tanzania imeshapata kiasi cha dola za kimarekani 300,000 kutoka katika mfuko huo wa GCF kwaajili ya kujiandaa kupata fedha za kuhimili na kukabilana na mabadiliko ya tabianchi lakini changamoto kadhaa zinakwamisha upatikanaji wa fedha hizo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi. 

Wadau waliainisha changamoto mbalimbali ikiwemo uwezo mdogo katika kuandika miradi, uratibu wa pamoja na kukosekana na mfumo mzuri wa kupeana taarifa sahihi juu ya namna bora ya kuomba fedha kutoka katika mfuko huo.

Pamoja na sekta ya Kilimo kuchangia 25% ya pata la ndani la taifa na 24% ya pato la nchi la taifa ambapo zaidi ya 80% ya watanzania wanajihusisha na shughuli za kilimo bado sekta hii inakabiliwa na athari za mabadaliko ya tabianchi.

“Ili kupunguza athari hizo kunahitajika fedha za kukabiliana nazo, lakini upatikanaji wa fedha umekua ni changamoto kubwa. Utafiti wetu katika sekta ya Kilimo, mifugo na Uvuvi unaonyesha sekta hizi hupata fedha kidogo zinazopelekwa katika miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi.” Anasema Mkurugenzi wa Forumcc, Rebecca Muna na kuongeza:

“Fedha kidogo zinapelekwa kwenye halmashuri na kushindwa kuleta mabadiliko chanya katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi” 

Katika mkutano huo Forumcc walishauri serikali kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo kwa kupeleka kiasi kikubwa kwenye miradi ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, kuongeza uelewa na kuingiza masuala hayo katika mipango na bajeti kwa ngazi zote.
Washiriki wa mkutano huo wakiendelea na majadiliano

FORUM CC YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUJADILI MWONGOZO WA KUFANYA USHAWISHI NA UTETEZI KUHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Shakwaanande Natai akifungua kongamano la mabadiliko ya Tabianchi lenye lengo la kujadili mwongozo wa ushawishi na utetezi katika mipango ya Maendeleo ya Serikali iliyandaliwa na ForumCC na kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka serikarini na sekta binafsi iliyofanyika katika ukumbi wa Sayansi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akizungumza jambo wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tabia ya nchi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Sayansi jijini Dar es Salaam.
Afisa Miradi kutoka ForumCC, Fazal Issa akitoa mada kuhusu mwongozo wa ushawishi na utetezi wa kuingiza mabadiliko ya Tabianchi katika mipango ya maendeleo ya Serikali pamoja na kupangiwa bajeti kuliko kusubilia majanga yakitokea.
Mratibu wa ForumCC, Rebecca Muna akichangia mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira kujadili mabadiliko ya Tabianchi.
 Mchumi kutoka Tume ya Mipango, Jordan Matonya akichangia mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za MazingiraTanzania(JET), John Chikomo akichangia mada kuhusu jinsi ya kuripoti habari zinazohusu mabadiliko ya Tabianchi na kuwafunda waandishi wanaoripoti habari za Tabianchi.
Afisa Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Theresia Massoy akichangia mada.
Afisa Msaidizi wa Miradi wa ForumCC, Jonathan Sawaya akichangia mada wakati wa kongamano lilowakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira kujadili mabadiliko ya Tabianchi.
Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifuatilia mada