HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

ZUBERI SENZOTA NA BI. KHADIJA KHAMIS WAMEREMETA

 Bw. Harusi,Zuberi Senzota Msemo Na Bi.harusi Khadija Khamis Lyoba  wakiyarudi magoma wakati walipokuwa wakiingia ukumbini katika tafrija maalum ya kuwapongeza kwa kuungana kwao, iliyofanyika katika ukumbi wa Tausi uliopo Kiluvya mkoani Pwani.
 Bw. Harusi,Zuberi Senzota Msemo na Bi.harusi Khadija Khamis Lyoba Wakiwa katika pozi
  Bw. Harusi,Zuberi Senzota Msemo Na Bi.harusi Khadija Khamis Lyoba  wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Picha zaidi bofya hapa

BW. RAYMOND MUSHUMBUSI NA BI. SUSAN BARNABAS WAFUNGA NDOA KANISA LA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akiwa pamoja na Mkewe Bi.Susan Barnabas jana wakati walipofunga ndoa takatifu na kuwa mwili mmoja kwenye kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam wakisindikizwa na wasimamizi wao Benedict Mwakasindile na Bi. Leticia Mwakaila , Ndoa hiyo ilifungwa na Padri Padri Haule wa Kanisa hilo Timu nzima ya Fullshangwe inawatakiwa maisha marefu na yenye furaha katika ndoa yenu huku mkijaaliwa kuiongeza dunia.

Bibi harusi Susan Barnabas na msimamizi wake Leticia Mwakaila wakiwa kwenye gari kabla ya kuingia kanisani tayari kwa tukio la kufungwa kwa ndoa hiyo jana.

Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akimvisha pete Mkewe Susan Barnabas wakati walipofunga ndo katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jana jijini Dar es salaa.

Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akiwa pamoja na Mkewe Susan Barnabas wakishiriki sala wakati wa ibada ya kufungwa kwa ndoa yao.

Padri Haule wa kanisa la Mtakatifu Petro akiziombe pete za maharusi huku maharusi hao wakiwa wamezishikilia.

Bibi Harusi Susan Barnabas akipozi kwa picha kwenye gari.

Bibi Harusi Susan Barnabas akimvisha pete mumewe Bw. Raymond Mushumbusi wakati walipofunga ndo kwenye kanisa la Mtakatifu Petro Osterbay jijini Dar es salaa huku Padri Haule akishuhudia tukio hilo kulia ni Bw. Benedict Mwakasindile msimamizi wa maharusi hao.

Maharusi wakisaini vyeti vya ndao mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo.

Maharusi wakiwa kanisani mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo.

Maharusi wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo kwenye kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam.

MWANAHABARI GEORGE BINAGI WA LAKE FM MWANZA AUAGA UKAPELA

Jana March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapela.

Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.

"Ahsanteni nyote mliotusaidia kutimiza ndoto yetu kubwa katika maishani yetu. Familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu. Waumini wote wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Daniel Kulola na kila mmoja kwa nafasi yake, Mungu awabariki. 

Mmenionesha upendo wa ajabu mno. Wazazi wangu hususani mama mpendwa, nimetimiza deni mliloniachia duniani, hakika sasa mtapumzika kwa amani, pahali pema, peponi, Amina. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, Mungu atuongoze vyema". Mr & Mrs George Binagi.
Shukurani za pekee pia ziwaendelee best man na best lady, Mr and Mrs, Joel Maduka kutoka Storm Fm Geita na Maduka Online kwa kufanikisha shughuli hiyo kwenda vyema.

PICHA: WANANDOA WALIOFUNGA NDOA YA SHILINGI 100 YA KENYA WAFUNGA NDOA TENA


Wanandoa nchini Kenya waliofunga ndoa iliyogharimu shilingi 100 tu ya Kenya, wamerejea kiapo chao cha ndoa yao jana katika Siku ya Wapendanao katika sherehe kubwa iliyoandaliwa na wasamaria wema. 
 Habari za wanandoa hao zilisambaa kwenye mitandao ya jamii mwezi uliopita nchini Kenya na watu wengi walioguswa na tukio hilo waliamua kujitolea kuigharamia upya tena harusi yao hiyo ili iwe ya kumbukumbu.


Katika harusi ya kwanza wanandoa hao Wilson na Ann Mutura walifunga ndoa wakiwa wamevalia nguo za kawaida fulana na jinzi, na kuvishana pete za chuma kanisani. Harusi yao ya marejeo iliyofadhiliwa inakasiwa kugharimu dola 35,000.

Wanandoa Wilson na Ann Mutura wakifunga ndoa yao ya awali iliyogharimu kiasi cha sh 100 za Kenya sawa na sh 1,800 za Tanzania

JOSEPH MWANUKUZI NA MARIAM WAMEREMETA LEO

 Joseph Mwanukuzi akiwa amepozi na mke wake Mariam wakati wa Ibada ya Ndoa yao iliyofanyika katika Kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
Joe na mke wake wakielekea kula kiapo cha ndoa.
Joseph akimvisha pete ya ndoa mke wake Mariam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAPYA YAIBUKA SAKATA LA BWANA HARUSI ALIYEMKIMBIA BI HARUSI SIKU YA NDOA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mapya  yameibuka sakata la kukwama kufungwa kwa ndoa ya Samwel Mwakalobo na Ginen Mgaya, baada ya kubainika kuwa moja ya sababu ni Bibi harusi mtarajiwa kuendeleza uhusiano na mzazi mwenzake.

Bwana harusi, Samuel Mwakalobo alitoweka muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Ginen Mgaya  katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Isanga jijini Mbeya.

Mwakalobo (26) alizua taharuki hiyo  Ijumaa ya Desemba 16, baada ya kutoonekana kanisani kufunga ndoa mbele ya Mchungaji Andagile Mwakijungu.

Habari zimedai kuwa kabla ya mpango wa kufunga ndoa hiyo, Mgaya tayari alishapata mtoto kabla hajaolewa, na Bwana harusi kubaini dakika za mwisho kuwa wawili hao walikuwa bado wana uhusiano wa karibu.

Habari hizo za ndani kutoka familia ya Bibi harusi, zilidai kuwa kilichofanya Bwana harusi amtelekeze Bibi harusi ni wasiwasi aliokuwa nao juu ya uhakika wa ujauzito wa mkewe huyo mtarajiwa, kuwa ni wake kweli au wa mpenzi wake huyo wa zamani.

“Hofu hiyo ilijengeka kutokana na taarifa alizoziamini Bwana harusi kuwa Bibi harusi anaendeleza uhusiano na mzazi mwenziwe. Ni hofu tu ambayo angeifanyia kazi na angegundua kuwa haina ukweli wowote,” kilidai chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kudai: “Unajua muda mwingine binadamu tunahitaji kufanya uamuzi kwa kutafakari … maana shemeji yetu (Bwana harusi) alipigiwa simu na mzazi mwenza wa Bibi harusi na kuelezwa maneno ya ‘shombo’ na yeye bila kufanyia utafiti, akaamua kususa harusi.”

Wakati taarifa hizo zikibainisha hayo, familia ya Bwana harusi imeendelea kufanya jitihada za kuhakikisha suala hilo linamalizika kistaarabu.

Anayeelezwa kufuatilia suala hilo kwa karibuni ni kaka yake, ambaye hadi jana jitihada za kumtafuta mdogo wake zilikuwa zimeshindikana kutokana na kutopokea simu yake ya mkononi mara zote.

“Anayeongoza familia ya Bwana harusi ni kaka yake. Inasemekana pia kuwa wawili hao waliingia kwenye mgogoro dakika za mwisho kabla ya harusi na ndiyo maana baada ya kutoweka hataki hata kupokea simu,” kilieleza chanzo kingine.

Awali, mpambe wa Bibi harusi alieleza kuwa siku mbili kabla ya harusi hiyo, Bwana harusi alikuwa kwenye migogoro ya kifamilia na ndugu zake kuhusu fedha za sherehe na mpaka siku ya sherehe, suala hilo walikuwa hawajalitatua.

“Lakini tunashukuru kaka yake ni mstaarabu, aliamua kuonesha upendo kwa mdogo wake na amekuwa akilifuatilia suala hilo ili limalizike kwa amani, lakini mdogo mtu hapatikani,” alisema mpambe huyo.

Alisema jitihada za Bibi harusi kumtafuta Bwana harusi hazijazaa matunda, kwani hadi juzi alikuwa hapatikani hata nyumbani kwake, ingawa redio ilikuwa inasikika ndani ya chumba hicho kilichofungwa kufuli kwa nje.

Simu ya Bwana harusi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokewa, lakini hatua zingine zilidai kuwa Bwana huyo ambaye ni mfanyabiashara kwenye kituo cha mabasi yaendayo Chunya eneo la Isanga jijini Mbeya hajafungua duka lake.

HARUSI YA BW. LOUIS MUNISHI NA MKEWE BI. INVIOLATA YAFANA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Bwana harusi Louis Munishi akipata picha ya kumbukumbu na mkewe Bi. Inviolata ukumbini. Ibada takatifu ya ndoa yao ilifanyika Kanisa la Bikira Maria mama wa huruma Mbezi Beach Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam. Bwana harusi Louis Munishi akipata picha ya kumbukumbu na mkewe Bi. Inviolata ukumbini. Ibada takatifu ya ndoa yao ilifanyika Kanisa la Bikira Maria mama wa huruma Mbezi Beach Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA