HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

JWTZ yatoa onyo kwa matapeli wa ajira

Jeshi la Wananchi (JWTZ) limetoa tahadhari kwa umma juu ya matapeli wanaowalaghai wananchi kwamba watawapa ajira katika jeshi hilo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Akitoa tahadhari hiyo, Mkuu wa Utumishi wa JWTZ, Meja Jenerali Harrison Masebo amesema wamepokea malalamiko mengi ya wananchi kuhusu utapeli huo na kusisitiza kwamba jeshi lina utaratibu wake wa kuajiri na siyo kuwatumia watu wengine kufanya kazi hiyo.
Masebo amesema wanawatafuta watu hao kwa sababu wanalichafua jeshi kwa kujiita maofisa wa JWTZ na kujenga dhana kwa wananchi kwamba wametapeliwa na jeshi.
"Tunaomba ushirikiano wa wananchi ili tuweze kuwakamata watu hao. Mtu akikwambia anataka kukupa kazi JKT au JWTZ wewe msikilize lakini tuletee taarifa kabla hukampa chochote, sisi tutamkamata,"amesema Masebo.
Mkuu huyo wa utumishi jeshini amesema ajira zote zinazotelewa na JKT lazima zitangazwe kwenye vyombo vya habari na mchakato wake uko wazi.
Amewataka wananchi wasiwape chochote matapeli hao badala yake watoe taarifa jeshini.

BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo baada ya mazungumzo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar (Picha na Ikulu)

PICHA: YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA LEO MAY 16, 2017.

 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Zungu akitafakali jambo wakati akiongoza    kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Mbunge wa Kavuu(CCM) Mhe, Dkt Pudencia Wilfred akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Mbunge wa Busega(CCM) Mhe Dk. Raphael Chegeni akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11 leo Mjini Dodoma Mei.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Josephine Genzabuke akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akifafanua jambo katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angela Mabula katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei.
  Naibu Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Martha Mlata akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11 leo Mjini Dodoma Mei.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Halima Bulembo  akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11 leo.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akisoma hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017.
 Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Florens Turuka na Naibu Katibu Mkuu Imaculate Ngwalle,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo,Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa na Meja Jenerali Michael Isamuhyo wa JKT wakiwa katika kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Michael Isamuhyo katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa wakizungumza jambo na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama leo katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.

Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

Taarifa Kuhusu UTAPELI Ajira za JWTZ



AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JWTZ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Kikundi cha ngoma cha JWTZ kikitumbuiza kwa ngoma ya Chaso ya Pemba wakati Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Waziri wa ulinzi nja Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Juma Kijazi na viongozi wengine katika picha ya pamoja baada ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.PICHA NA IKULU

JENERALI MWAMNYANGE ATAJA KITU AMBACHO HATOKISAHAU

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amesema katika kipindi chake cha utumishi jeshini, hatasahau kamwe tukio la milipuko ya mabomu kwenye vikosi vya Mbagala mwaka 2009 na Gongolamboto mwaka 2011.

Aliyazungumza hayo Ikulu, Dar es Salaam Jumatatu hii wakati akiongea na wanahabari baada ya kuapishwa mkuu mpya wa majeshi, Jenerali Venance Mabeyo. Jenerali mstaafu Mwamunyange alisema tangu aingie jeshini mwaka 1971, wakati wa milipuko hiyo iliyosababisha vifo na uharibufu wa mali, ndiyo ulikuwa mgumu zaidi kwake.
“Wakati wa milipuko ya Mbagala na Gongolamboto nilikuwa kwenye nafasi hii (Mkuu wa Majeshi), huu ndiyo ulikuwa wakati mgumu kwangu kwa sababu ilisababisha vifo, mali za watu na askari ziliteketea, kwangu kipindi kile kilikuwa kigumu sana,” alisema Mwamunyange.
Milipuko ya mabomu ya Mbagala, ilitokea April 2009, kwa upande wa Gongo la Mboto ilitokea Februari 2011.