Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mahakama Kuu imewapa siku saba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake kujibu madai ya chama hicho.
Msajili, Lipumba na wenzake walipewa muda huo jana na Jaji Sekieti Kihiyo kutokana na kesi ya madai iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF mahakamani hapo.
Katika kesi hiyo namba 23 ya mwaka 2016, bodi ya wadhamini CUF inaiomba mahakama itoe amri ya kubatilisha barua ya Msajili inayomtambua Profesa Lipumba kuwa ndiye mwenyekiti wa chama hicho.
Pia, wanaiomba mahakama itoe amri ya kumzuia Msajili kufanya kazi nje ya mipaka yake ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yake na pia itoe amri ya kumzuia Msajili kuingilia masuala ya kiutawala ndani ya chama hicho.
Mbali na Msajili na Profesa Lipumba, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wanachama wengine tisa waliosimamishwa uanachama wa chama hicho, akiwamo Naibu Katibu Mkuu Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua (Tabora), Magdalena Sakaya.
Kesi hiyo ilitajwa jana mahakamani hapo kwa mara ya kwanza tangu ilipofunguliwa Oktoba 19, mwaka huu na mahakama ikataka wadaiwa kuwasilisha majibu ya madai hayo ya CUF, Novemba 17, mwaka huu.
Pia, Mahakama ilielekeza upande wa Maalim Seif kuwasilisha majibu ya hoja za wadaiwa Novemba 23 na ikapanga kesi hiyo itajwe tena Novemba 24, kwa ajili ya kuendelea na hatua nyingine.
Wadai katika kesi hiyo wanawakilishwa na mawakili Juma Nassoro na Halfani Daim wakati Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanawakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Obadia Kameya na Lipumba na wenzake wakiwakilishwa na Mashaka Ngole.
Katika hati ya Kiapo kinachounga mkono maombi hayo, Maalim Seif anadai kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia utendaji wa ndani wa Vyama vya Siasa.
Anadai kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya nchi haimpi mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa chombo cha rufaa wala kurejea mambo ya utawala ndani ya chama cha siasa.
Badala yake anadai mamlaka hayo yako kwa vyombo vya juu vya chama na Mahakama na kwamba jukumu la Msajili ni kusajili vyama na kuweka kumbukumbu za vyama hivyo.
CUF kimekuwa na mgogoro wa kiuongozi baada ya Profesa Lipumba kuandika barua ya kutengua uamuzi wake wa awali wa kujiuzulu ambao Msajili alikubaliana naye na alikiandikia barua chama kuendelea kumtambua mwenyekiti huyo. Hata hivyo, CUF ilimfukuza uanachama Lipumba.
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AVIFUTIA USAJILI WA KUDUMU VYAMA VITATU VYA SIASA
By: VIJIMAMBO on November 09, 2016 / comment : 0 Jaji Francis Mutungi, Matukio, Msajili wa Vyama vya Siasa
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Monica Mnanka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habariwakati akimkaribisha msajili wa vyama kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Msaji Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Msajili wa Vyama, Jaji Francis Mutungi.
Msajili wa VVyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kufutwa kwa usajili wa kudumu wa vyama vitatu vya siasa ambavyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) na Chama cha Jahazi Asilia. Kulia ni Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992, amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kuanzia leo hii.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi Jaji Mutungi alivitaja Vyama alivyovifuta kuwa ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), kilichopata usajili wake Novemba 15, 2001 kilichokuwa kikiongozwa na James Mapalala kama Mwenyekiti wa Taifa na Mwaka Lameck Mgimwa kama Katibu Mkuu.
Chama kingine alichokifutia usajili wa kudumu ni Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) kilichopata usajili Machi 4, 2003 kilichokuwa kikiongozwa na Peter Kuga Mziray kama Rais Mtendaji Taifa na Nziamwe Samwel kama Katibu Mkuu.
Jaji Mutungi alikita chama kingine alichokifuta kuwa ni Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kikiongozwa Kasimu Bakari Ally kama Mwenyekiti wa Taifa na Mtumweni Jabir Seif kama Katibu Mkuu ambacho kilipata usajili wa kudumu Novemba 17, 2004.
Mutungi alisema vyama hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambapo kila chama klipewa taarifa ya nia ya Msajili wa Vyama vya siasa kufuta usajili wake wa kudumu na kutakiwa kueleza kwanini kisifutwe ambapo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha kuwa havikukiuka sheria na bado vinavyo sifa za usajili wa kudumu.
BODI YA WADHAMNI CUF YAWASHITAKI MAHAKAMANI PROFESA IBRAHM LIPUMBA NA MSAJILI WA VYAMA JAJI FRANCIS MUTUNGI
By: VIJIMAMBO on October 06, 2016 / comment : 0 CUF, Habari, Jaji Francis Mutungi, Maalim Seif, Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, UKAWA
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mgogoro ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) umeingia hatua ya pili baada ya Bodi ya Wadhamini kufungua kesi wakimtuhumu Prof. Ibrahim Lipumba, Jaji Francis Mutungi na watu 12 kwambwa, wanahujumu chama hicho.
Bodi hiyo jana imewasilisha maombi ya kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ya kuomba kibali cha kumzuia Jaji Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasas nchini kutofanya shughuli zake kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo, watuhumiwa ni pamoja na Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho aliyerejeshwa kwa barua ya Jaji Mutungi na watu 12 waliokuwa wanachama wa chama hicho.
Akizungumza na vyombo vya habari Juma Nassoro, wakili wa chama hicho alisema kuwa, wamewasilisha maombi hayo yaliyopelekwa kwa Eva Nkya, Msajili wa Mahakama hiyo ambapo ni ombi namba 75.
Wakili Nassoro alieleza kuwa, katika maombi ya awali waliyowasilisha kabla ya kesi ya msingi kuanza kusikilizwa ni pamoja na mahakama kumuamuru Jaji Mutungi kutengua kauli yake ya uteuzi wa Prof. Lipumba.
Alidai kuwa, mahakama hiyo iliwahi kubainisha kazi za msajili wa vyama ambapo sio kuingilia uamuzi wa ndani ya vyama vya siasa.
Wakili Nassoro alidai kuwa, Jaji Mtungi hana mamlaka ya kutengua uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho .
Prof. Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na ujio wa Edward Lowassa ambaye baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hata hivyo, mwaka huu aliaeleza kuandika barua ya kutengua barua yake ya wali ya kujiuzulu kwa madai ya kutaka kujenga chama jambo ambalo limesababisha chama hicho kupasuka.
Wiki iliyopita, Baraza Kuu la Uongozi la CUF, katika kikao cha dharura kilichofanyika Makao Makuu ya CUF, mjini Zanzibar lilimfukuza uanachama wa chama hicho Prof. Lipumba.
“Baraza Kuu linaweka bayana kwa wanachama wa CUF, Watanzania na mamlaka zote nchini kwamba kuanzia leo, Prof. Ibrahim Lipumba hana haki ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na shughuli zozote za chama,” ilieleza taarifa ya CUF.
Aidha taarifa hiyo ilidokeza kuwa, uamuzi huo umechukuliwa baada ya baraza hilo kuridhika na mashtaka dhidi ya Prof. Lipumba kuongoza na kusimamia kikundi cha wahuni kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam tarehe 24 Septemba, 2016 mwaka huu.
“Baraza kuu limetumia uwezo wake, kwa mujibu wa Ibara ya 10 (1) (c) na kwa kura zote 43 za wajumbe wake waliohudhuria kumfukuza uanachama Prof. Ibrahim Lipumba,” ilieleza taarifa hiyo.
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA, JAJI FRANCIS MUTUNGI ATOA ONYO KWA WANAOTUMIA JINA LA CHEO CHAKE VIBAYA
By: VIJIMAMBO on October 05, 2016 / comment : 0 Habari, Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa, Siasa
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Msajili wa Vyama vya Viasa Mhe. Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama: Sikumrudishia Lipumba uenyekiti CUF, Kajirudisha Mwenyewe Kinyemela
By: VIJIMAMBO on September 26, 2016 / comment : 0 CUF, Habari, Jaji Francis Mutungi, Profesa Ibrahim Lipumba, UKAWA
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Wakati wanasiasa na wasomi wakimnyooshea kidole Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (pichani) kwa uamuzi wake wa kumtambua aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyewe ameibuka na kusema kuwa hatua yake hiyo haikulenga kumrudishia msomi huyo nafasi yake ya uenyekiti.
Jaji Mutungi jana alisema kuwa alichofanya ni kukishauri chama hicho kuhusu mgogoro uliokuwa ukikisonga na Lipumba aliamua kutumia ushauri huo kurudi mwenyewe kwenye nafasi yake hiyo kinyemela.
Kauli hiyo ya Jaji Mutungi imekuja siku mbili tangu alipotoa waraka unaoelezwa kumtambua Profesa Lipumba kama kiongozi halali wa CUF licha ya kuandika barua ya kujiuzulu Agosti 6, mwaka jana akipinga vyama vinavyounda Ukawa kumpa fursa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kugombea urais.
“Isome barua yangu…, mimi nimeamua watu waijadili umenielewa? Ni vizuri wanavyoijadili, ila nilitarajia waijadili kwa tija sio kwa hasira,” alisema Jaji Mutungi.
Alipoulizwa kuhusu polisi kumsaidia Profesa Lipumba kuingia katika makao makuu ya CUF kwa mtutu alisema: “Hizo ni taratibu ambazo (polisi) wanatumia kwa kuzingatia sheria nyingine za nchi.”
Juni mwaka huu, Profesa Lipumba alimwandikia barua Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutengua barua yake ya kujiuzulu na kutaka arejee kwenye kiti chake, uamuzi uliozusha mtafaruku huku Mkutano Mkuu wa chama hicho ulioketi Agosti 21 ukiridhia kujiuzulu kwake licha ya kuwa ulivunjika.
“Barua yangu inajieleza sina haja ya kuichambua. Nimekujibu baada ya kuona mjadala huo (katika mitandao) nilitegemea (waliomtukana) wawashauri CUF cha kufanya badala ya kuanza kunitukana,” alisema Jaji Mutungi.
“Sasa huko mahakamani wanakotaka kwenda kama mahakama ikiamua kama Mutungi alivyoshauri huko nako watatukana pia?” alihoji.
Wanasiasa na wasomi
Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Constatine Akitanda alisema alichofanya msajili ni kupandikiza zogo ndani ya CUF jambo ambalo linasikitisha.
Akitanda alisema ndani ya CUF kuna bundi ambaye alikuwa anasumbua watu ila msajili ameongezea mgogoro huo na kuwa alichokifanya si sawa kwa mujibu wa mamlaka yake.
“Unajua hii nchi inachezewa sana hivi mtu anajiuzulu mwenyewe halafu anaamua kurejea mwenyewe bila kufuata taratibu ni aibu, lakini nadhani kuna mkono wa mtu,’ alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira alisema anachokiona ndani ya CUF ni uwepo wa biashara haramu ambayo inaweza kuua chama hicho.
Alisema ni wakati mwafaka kwa wafanyabiashara haramu hao wakajulikana katika pande zote kwani ni aibu kuvumilia kasoro hizo zitawale vyama vya siasa.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Dominata Rwechungura alisema migogoro ndani ya vyama vya siasa ipo, hivyo ni jukumu la CUF kutatua ili kurejesha amani na upendo kati yao.
Mwenyekiti wa Chama cha United People Democratic Party (UPDP), Fahimu Dovutwa alisema kinachotokea ni msiba unaoacha pengo ndani ya CUF na vyama vya siasa nchini.
Dovutwa alisema pia pengo la mwasisi wa CUF, marehemu Shaban Mloo linaonekana na kuwataka wazee wa chama hicho kukaa ili kukinusuru chama.
“Huu ni msiba katika siasa za Tanzania, naomba CUF watafute wazee wao ili waweze kusuluhisha hali hiyo kwa maslahi ya chama chao kwani pengo la Mloo linaonekana,” alisema.
Katibu wa Habari na Uenezi wa NCCR Mageuzi, David Kafulila alisema mgogoro wa CUF unaweza kutolewa uamuzi na mahakama pekee kwa kuwa msajili hana mamlaka ya kufanya alichokifanya. Kafulila alisema msajili anapaswa kushauri kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na si kama alivyoelekeza kwani anaongeza mgogoro zaidi.
Mwenyekiti wa ADC, Hamad Rashid alishauri CUF kutumia vikao kumaliza tofauti zao, huku akibainisha kuwa ndani ya chama hicho kuna viashiria vya udikteta na usultani.
Mbunge wa Tandahimba CUF, Katani Katani alisema kwa sasa wamethibitisha jinsi Lipumba anavyotumika kwani pamoja na Jeshi la Polisi kukataza maandamano, wafuasi wa Lipumba waliandamana bila kuzuiwa.
Alisema haiwezekani chama kikaendeshwa kwa ajenda za watu wachache ambao wanatumikia matumbo yao na makundi yao na si chama.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kitivo cha Sheria, Dk. Onesmo Kyauke alisema msajili anakosea na kuwataka CUF wakimbilie mahakamani kupata haki.
CHAMA CHA SIASA CHAFUTIWA USAJILI
By: VIJIMAMBO on August 11, 2016 / comment : 0 Habari, Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini amekifuta katika orodha ya vyama vya siasa vyenye usajili wa muda Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-Tanzania) kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya usajili. Chama cha CM-Tanzania kilipata usajili wa muda tarehe 4 Februari, 2016.
Kwa mujibu wa kifungu cha 8(3) na (4) cha Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992, chama cha siasa chenye usajili wa muda ni lazima kiwasilishe maombi ya usajili wa kudumu ndani ya siku mia moja na themanini tangu tarehe ya kupata usajili wa muda. Aidha, uhai wa chama cha siasa chenye usajili wa muda unaisha baada ya siku mia moja na themanini (180) tangu kipate usajili wa muda .
Hivyo, uhai wa cheti cha usajili wa muda wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-Tanzania) ulikwisha tarehe 2 Agosti, 2016, kwani waanzilishi wake walipaswa kuwasilisha maombi ya usajili wa kudumu siyo zaidi ya tarehe 02 Agosti, 2016.
Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, waanzilishi na wanachama wote wa CM-Tanzania hawapaswi kufanya siasa au shughuli yoyote kwa jina la Chama cha Maadili na uwajibikaji, kwa sababu uhai wa cheti chake cha usajili wa muda umekwisha. Kufanya hivyo ni kukiuka Sheria za nchi.
Kufutwa kwa Chama cha Maadili na Uwajibikaji kunaifanya idadi ya vyama vya siasa vyenye usajili wa muda kuwa kimoja ambacho ni Chama cha Restoration of the Nation Party (RNP). Aidha, idadi ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni ishirini na mbili (22).
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ALAANI TAMKO LA CHADEMA
By: VIJIMAMBO on July 28, 2016 / comment : 0 Habari, Jaji Francis Mutungi, Siasa
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.
“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.
Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.
Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).
Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.
Jaji Mutungi ametoa rai kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.
Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Serikali imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kuharakisha maboresho ya mitaala na mafunzo ya Uhasibu ili...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Huma...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015
November 01, 2015
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014









