HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKAJI KUZINDUA KLABU ZA ELIMU YA UZIMAJI MOTO SHULE ZA SEKONDARI NCHINI

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kueleza mipango mbalimbali ya jeshi hilo ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi, Casmir Ndambalilo.
 Mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa kuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, akiuliza swali kwa Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye(hayupo pichani), wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa kuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye  wakati wa mkutano huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

KAMISHNA JENERALI WA MAMLAKA YA MAPATO (TRA) ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kulia alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Mnazi Mmoja mapema leo asubuhi.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliopo mnazi mmoja katika ziara zake baada ya kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli hapo jana.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoji kutoka kulia ni Naibu Kamishna Billy Mwakatage, Kaimu Kamishana Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla, Mhasibu Mkuu Chakala, Kaimu Kamishna wa Operesheni Christom Manyologa na Kamishana Msaidizi Hamadi Muhando wakimfuatilia kwa karibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere hayupo pichani, alipofanya ziara katika Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 06/04/2017
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimfuatilia kwa karibu huku akiandika, Kamishana MKuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere, Kamishna huyo aliambatana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo (kulia) alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo Asubuhi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimpatia zawadi ya Kalamu ya Jeshi yenye namba ya dharura 114, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) mapema leo asubuhi alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimsindikiza Kamishana MKuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) akiondoka Makao Makuu ya Jeshi hilo alipofanya ziara Mapema leo Asubuhi.
(Picha Na Konstebo Joyceana Benson)

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTEMBELEA KITUO CHA PEDDEREF SOBER HOUSE KIGAMBONI

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akitoa nasaa kwa wanawake na vijana walioathirika na janga la madawa ya kulevya kituoni hapo mapema leo asubuhi.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akimpa mkono wa pongezi mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe kwa jitihada anazoendelea kuzifanya katika kuhakikisha waathirika wote wa madawa ya kulevya waliopo kituoni kwake wanapata elimu ya kutosha na hatimaye kuacha kabisa utumiaji wa madawa hayo.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa kituo People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef), Nuru Salehe wakati wa sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mapema leo asubuhi. Kulia ni Jacqueline Samson na Ashura Diwani.
Moja ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi. Jacqueline Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada waliowapatia.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef) bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo, ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya kupewa elimu na malezi yanayostahili.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo. 

Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni hapo.

UPDATES: MOTO WATEKETEZA JENGO LA MAKAZI YA ASKARI POLISI MJINI MOSHI

Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika, umeteketeza jengo la ghorofa mbili la makazi ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) la mjini Moshi usiku huu.
Vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Kiwanda cha Sukari cha TPC vilikuwa vikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mashuhuda wameliambia gazeti hili kuwa moto huo umeanza saa 2: na hadi kufikia saa 4:00 ulikuwa umeteketeza ghorofa ya pili unakosadikiwa kuanzia.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa familia zote za askari wa kikosi hicho cha FFU wanaoishi katika nyumba hiyo wamefanikiwa kutoka salama isipokuwa baadhi ya mali zimeteketea.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia jitihada kubwa zikifanyika za kuuzima moto huo lakini unaonekana kuzidi kushika kasi baada ya gari la Halmashauri kuishiwa maji.
Hii ni mara ya pili kwa jengo hilo kuungua moto, miaka ya hivi karibuni lililipuka moto na vikosi vya zimamoto vilifanikiwa kuudhibiti.
Sehemu ya Familia za Askari waliokuwa wakikaa katika Jengo hilo pamoja na mashuhuda wakiangalia tukio hilo wakati vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vikiendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo.
Sehemu ya mali zilizoteketea kwa moto huo.
Jitihada za kuuzima moto huo kwa baadhi ya maeneo ndani ya jengi hilo zikiendelea.

JESHI LA ZIMAMOTO LAADHIMISHO SIKU YA MTOTO NJITI KWA KUWATEMBELEA WATOTO NJITI HOSPITALI YA RUFAA TEMEKE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi (wapili kushoto) akizungumza na wazazi waliozaa watoto njiti kabla ya Jeshi kuwapa misaada mbalimbali kwa ajili ya kusaidia malezi ya watoto hao waliozaliwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto lilianzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kuitembelea hospitali hiyo ambapo walitoa zawadi mbalimbali kwa watoto njiti, watoto wanaoumwa na watoto waliozaliwa kwa njia ya operesheni. Wapili kulia(aliyebeba zawadi) ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo, Maria Kulaya. Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maria Kulaya (kushoto) na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi wakimkabidhi msaada wa soksi na kofia mzazi aliyejifungua mtoto njiti, Fausta Jison katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto lilianzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kuitembelea hospitali hiyo ambapo walitoa zawadi mbalimbali kwa watoto njiti, watoto wanaoumwa na watoto waliozaliwa kwa njia ya operesheni. Kulia ni Mariam Juma ambaye naye alijifungua mtoto wa aina hiyo katika hospitali hiyo. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maria Kulaya (kushoto) na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi wakimkabidhi msaada wa soksi na kofia mzazi aliyejifungua mtoto njiti, Mariam Juma katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto lilianzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kuitembelea hospitali hiyo ambapo walitoa zawadi mbalimbali kwa watoto njiti, watoto wanaoumwa na watoto waliozaliwa kwa njia ya operesheni. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Rosy Meena akitoa zawadi ya soksi na kofia kwa mtoto aliyezaliwa na matatizo ya kiafya katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto lilianzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kuitembelea hospitali hiyo ambapo walitoa zawadi mbalimbali kwa watoto njiti, watoto wanaoumwa na watoto waliozaliwa kwa njia ya operesheni. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi akitoa zawadi ya soksi na kofia kwa mtoto aliyezaliwa na matatizo ya kiafya katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto lilianzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kuitembelea hospitali hiyo ambapo walitoa zawadi mbalimbali kwa watoto njiti, watoto wanaoumwa na watoto waliozaliwa kwa njia ya operesheni. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Dk Aman Malima, akiwapa elimu Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maria Kulaya (kulia) na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo, Puyo Nzalayaimisi kuhusu watoto njiti wanavyozaliwa, kabla ya Maafisa hao wa Jeshi pamoja na askari mbalimbali waliofika hospitalini hapo kwenda kuwatembelea wodini watoto njiti, watoto waliozaliwa na matatizo mbalimbali pamoja na watoto waliozaliwa salama katika hopsitali hiyo. Jeshi hilo limeanzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kutoa misaada katika hospitali hiyo kwa wazazi waliojifungua watoto hao. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maria Kulaya (watano kushoto mstari wa mbele), Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa na askari wa Jeshi hilo mara baada ya kumaliza kutoa misaada mbalimbali kwa watoto njiti, watoto wanaoumwa na watoto waliozaliwa kwa njia ya operesheni katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto lilianzimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani kwa kuitembelea hospitali hiyo ambapo walitoa. Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

MOTO WATEKETEZA BOHARI LA KAMPUNI YA 7 GENERAL ENTERPRISES MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Hivi ndivyo moto mkubwa ulivyokuwa ukiwaka katika Bohari la 7 General Enterprises ambapo walikuwa wakihifadhia Mataili, mchana eneo la Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Vikosi mbalimbali vya zima moto kutoka Serikali na Makampuni binafsi wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.
Baadhi ya watu mbalimbali wakiendelea kushuhudia tukio hilo la kuteketea kwa Bohari 
Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumzia kwa ufupi tukio hili na kusema kuwa kwa sasa hawezi zungumza chochote mpaka moto utakapozimwa kabisa 

Hapa mpaka Trekta nalo lilihusika katika kuhakikisha moto huo unazimika 
Mmoja wa waandishi wa Habari ambaye hakujulikana anatokea katika chombo gani akiwa anaendelea kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua taarifa.
Baadhi ya wataalam wa kuzima moto wakiwa wanaendelea na juhudi za kutazama maeneo ambayo moto unawaka zaidi ili kuuzima
Moja ya Gari la zima moto likiwa linawahi eneo la Tukio kusaidia kuzima moto
Zima moto wakiendelea na shughuli ya kuhakikisha moto unazimika katika Bohali hilo
Moto ukiendelea kuteketeza Bohari hilo lililokuwa la kuhifadhia mataili
Pamoja na watu kupewa tahadhali ya Moto mkubwa uliokuwa unawaka lakini bado walikuwa wakiongezeka kushuhudia tukio hilo.
Katika juhudi za kuhakikisha moto huo unazimika kabisa magari ya kila aina yanayobeba maji yalichukuliwa kuongeza nguvu za kuzima moto huo.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa kabisa katika eneo ambalo moto ulikuwa unawaka
Mmoja wa wafanyakazi wa Bohari hilo Shaban Salum akielezea kwa ufupi kile alichokiona wakati moto huo unaanza kuwaka mida ya saa sita mchana


Magari ya zimamoto na mengine ambayo ni ya kubebea maji yakiwa katika eneo la Bohali la 7 General kuhakikisha wanashirikiana kumaliza moto huo
Umati wa watu wakiwa katika eneo hilo la Bohari wakiendelea kushuhudia Tukio hilo
Watu wengine wakiwa wamekaa Jirani kabisa na Moto huo bila wasiwasi wakishuhudia tukio hilo la Moto. Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za mikoa

BREAKING NEWS: HOTELI YA KCC KIBAHA MAILI MOJA YASHIKA MOTO MCHANA HUU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Moto Mkali ukiendelea kuteketeza eneo la jiko la hoteli ya KCC iliyopo Kibaha Maili Moja, Mkoani Pwani mchana huu. Askari wa zimamoto bado wanaendelea na uzimaji wa moto huo. haijafahakima bado kama kuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na tukio hilo la moto. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASO BLOG.
Moto ukiendelea kuteketeza Jengo hilo.
Baadhi ya Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na kazi ya uzimaji wa Moto huo, uliozuka ghafla kutokea katika Jiko la Hoteli hiyo, Mchana huu.