HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Forbes yatoa listi ya Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017

Jarida la Forbes limetoa list ya wafanya biashara 25 ambao ndio matajili zaidi barani Afrika mfanyabiashara kutoka
 Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi kwa mujibu wa orodha hiyo ya mabilionea ya mwaka 2017.

Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.
Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.
Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.

 Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.
Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:
1. Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni
3. Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni
4. Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni
5. Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni
7. Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni
8. Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni
9. Isabel dos Santos, Angola

Utajiri: $3.1 bilioni
10. Issad Rebrab, Algeria

Utajiri: $3 bilioni
11. Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni
12. Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni
13. Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni
14. Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni
15. Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni
17. Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni
18. Folorunsho Alakija, Nigeria

Utajiri: $1.61 bilioni
19. Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni
20. Mohammed Dewji, Tanzania

Utajiri: $1.4 bilioni
21. Stephen Saad, Afrika Kusini
Utajiri: $1.21 bilioni
22. Youssef Mansour, Misri
Utajiri: $1.15 bilioni
23. Onsi Sawiris, Misri
Utajiri: $1.14 bilioni
24. Anas Sefrioui, Misri
Utajiri: $1.06 bilioni
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini
Utajiri: $1 bilioni

Source: BBC

MO Dewji Foundation yatoa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka katika Hospitali ya Sekou Toure

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuboresha hudumza za afya kwa mama na mtoto, Taasisi ya MO Dewji imetoa msaada wa vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 100 kwa Hospitali ya SekouToure iliyopo mkoani Mwanza. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amesema msaada huo ni sehemu ya malengo ya taasisi hiyo ya kuhakikisha inasaidia sehemu zenye uhitaji katika sekta ya afya, elimu na ustawi wa jamii. Amesema msaada huo unalenga kusaidia kupunguza vifo vya wanawake na watoto kwani kwa sasa idadi ni kubwa hivyo msaada huo utawezesha mkoa wa Mwanza kuongeza kasi ya mapambano ili kumaliza kabisa vifo vya wanawake na watoto. 
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza kuhusu juhudi ambazo zinafanywa na taasisi hiyo kwa ajili ya kusaidia jamii na malengo ya kutoa msaada katika Hospitali ya Sekou Toure.

"Tunafahamu kwamba asilimia 32 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinatokea katika siku 28 za mwanzo lakini pia tunaelezwa kuwa kila mwaka cha wanawake 8,000 hufariki dunia wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika na sisi kitu cha kwanza tunachotaka ni kusaidia mapambano ya kupunguza vifo vya watoto na wanawake," amesema Barbara. Nae mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameitaja Taasisi ya MO Dewji kuwa mfano wa kuigwa kwa msaada ambao wameutoa kwa hospitali ya mkoa huo na kuwaomba kuendelea kuwasaidia pindi wanapohitaji msaada zaidi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumzia mipango ya Serikali kuboresha huduma za afya lakini pia kuishukuru Taasisi ya MO Dewji kwa msaada ambao wamewapatia.

"Ukimpa mama afya bora, umesaidia jamii nzima, jambo lililofanywa na Taasisi ya MO Dewji ni kubwa sana, hospitali zetu zinamahitaji makubwa sana na kwa hili ambalo wamefanya ni mfano wa kuigwa na watu wengine, tunawashukuru sana na tunawaomba muwe tayari kutusaidia kwa muda mwingine," amesema Mongella. Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota amesema aliomba Taasisi ya MO Dewji kuwasaidia baada ya kuona changaoto nyingi ambazo zinawakabili wanawake ambao wanakwenda kujifungua katika Hospitali ya Sekou Toure na watoto ambao wanazaliwa.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota akieleza sababu ya kuiomba msaada Taasisi ya MO Dewji ili iwasaidie vitanda, magodoro na mashuka kwa ajili ya wodi ya wazazi.

"Rais Magufuli alikuja hapa na hata yeye aliona changamoto ambazo zinatukabili na mimi kama mbunge niliamua kwenda kuzungumza na watu wa MO Dewji Foundation na napenda kuwashukuru kwa kukubali kutusaidia na naamini msaada huu utasaidia kupunguza baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinatukabili," alisema Lwota.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi akitoa taarifa ya Hospitali ya Sekou Toure.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi amesema hospitali hiyo licha ya changamoto ambazo zinawakabili inahudumia wagonjwa 500 kwa siku na kwa wanawake ambao wanafika kujifungua kwa siku wanakadiriwa kuwa kati ya 30 na 40.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipokea msaada wa vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 100 kutoka Taasisi ya MO Dewji.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akimshukuru Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez kwa msaada ambao wamewapatia.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure Dk. Rweyendela Onesmo akitoa neno la shukrani.Mmoja wa wanawake ambao wamejifungua katika Hospitali ya Sekou Toure, Eveline Francis akiishukuru MO Dewji Foundation kwa msaada ambao wametoa kwenye hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota na Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez wakimjulia hali Zuwena Mohammed baada ya hafla ya kukabidhi msaada.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa UWT Mwanza, Ellen Bagohe na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi wakiwa katika picha ya pamoja.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa UWT Mwanza, Ellen Bagohe na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Hospitali ya Sekou Toure.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

MO DEWJI FOUNDATION YAZINDUA MPANGO WA UFADHILI KWA WANAFUNZI WA UDSM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez akielezea jinsi wanafunzi hao 10 watakavyoweza kufaidika na udhamini wa Mo Dewji Foundation.
 Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi akizungumzia mchakato wa kupata wanafunzi 10 ambao watapata udhamini wa Mo Dewji Foundation.
Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi na Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez wakipongezana mara baada ya kufanya uzinduzi.
Baadhi ya watumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa UDSM.

Na Mwandishi wetu
Mo Dewji Foundation kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM Imezindua rasmi mpango wa ufadhili kwa wanafunzi 10 wa elimu ya juu waliomaliza kidato cha sita mwaka huu wa 2016 (MO Scholar Program) kwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Jumatano Septemba, 7 2016.

Mpango huu wa ufadhili kwa wanafunzi umelenga kuwawezesha wanafunzi wenye sifa tatu, wasio na uwezo wa kujilipia ada ya chuo, wanafunzi ambao wameshiriki vyema katika michezo na uongozi wakiwa shuleni na wanafunzi ambao wamefaulu kwa kiwango cha alama 1 na 2 (division 1 & 2)

Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez amesema kuwa wameanzisha mpango huo kwa lengo la kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania kwa kutoa msaada wao wa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.

“Mpango wetu kwa muda wa miaka mitatu hadi minne ni kusaidia zaidi Tanzania lakini hapo baadae kama tukifanikisha malengo yetu Tanzania tutakwenda mbali zaidi,” ameongeza Barbara.

Aidha Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi ameelezea kuwa chuo kikuu cha Dar es salaam kimelenga kusaidia wanafunzi wote wa kitanzania ambao wanasifa za uhitaji wa ufadhili na ameomba vyombo vya habari visaidie kusambaza ujumbe kwa watanzania ili wanafunzi wafaidike na mpango huo.

“Tumeanza na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, tutaangalia namna ambavyo mpango na tutaenda na hapo baadae tutatanua mikono yetu kwenda vyuo mbalimbali,” amesema Barbara.

Na kwa mtahiniwa ambaye anakuwa anahitaji kutuma maombi kwa ajili ya kupata ufadhili wa Mo Dewji Foundation kwa ajili masomo ya chuo kikuu anaweza kuingia tovuti ya modewjifoundation.org

UONGOZI WA SIMBA WATOA TAMKO BAADA YA MO DEWJI KUKUBALIWA KUIENDESHA SIMBA KWA MFUMO WA HISA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

MO DEWJI AAHIDI MAKUBWA SIMBA KAMA AKIPATA NAFASI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kuelekea mkutano mkuu wa Simba unaotaraji kufanyika Jumapili ya Julai, 31, shabiki na mkeleketwa wa Simba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amezungumza mipango yake aliyopanga kuifanyia Simba kama akipata nafasi ya kununua hisa asilimia 51 za klabu hiyo.

MO amesema kuwa mipango yake ni kuwekeza Bilioni 20 na amepanga bajeti ya klabu hiyo kwa mwaka iwe Bilioni 5.5, kiasi ambacho anaamini kuwa kitaweza kubadili mwelekeo wa Simba kutoka ilivyo sasa na kurudisha zama zake za kutwaa mataji ya ndani na kufika hatua nzuri kimataifa.

MO alisema amefikia uamuzi wa kutaka kununua hisa katika klabu ya Simba kutokana na mapenzi aliyonayo katika klabu hiyo na hana nia yoyote ya kiabiashara na klabu hiyo kwani tayari ana biashara anazofanya ambazo zinamuingizia pesa nyingi hivyo jambo hilo ni kuona timu aliyo na mapenzi nayo ikifanikiwa.

"Nipo tayari kuwekeza Bilioni 20 kama watanipa nafasi lakini tukubaliane kuwa hakuna mtu atagusa pesa hizo pesa, tutauza bondi na kwa kila mwaka tutaingiza Bilioni 3.5 na tutatengeneza mapato ya Bilioni 2 kila mwaka ukijumlisha ni Bilioni 5.5 ambayo itakuwa ni bajeti ya mwaka,

"Inaniuma sana kuona klabu imekuja juzi tu leo inatuzidi mafanikio lakini kama Yanga na Azam bajeti zao kwa mwaka ni Bilioni 2.5 hadi Bilioni 3, sisi tukiwa na bajeti ya Bilioni 5.5 tutakuwa tumewazidi na tutaleta wachezaji wazuri na kocha mzuri," alisema na kuongeza.

"Dhamira yangu sio kupata Simba kibiashara, mimi Mungu kanijalia nina pesa nina biashara ziadi ya 100, tumeajiri wafanyakazi wanafika 28,000 , jambo ninalolitaka Simba ni kuwekeza, tubadili mfumo, tushinde mataji na sio Tanzania pekee shabaha yangu ni kushinda mataji ya Afrika"

Aidha MO alisema kuwa kama akipata nafasi atazungumza na viongozi wa Simba ili kila mwanachama wa klabu wa muda mrefu apatiwe hisa bure kutokana na kazi kubwa ambayo wameifanya katika klabu hiyo.

"Nitazungumza na viongozi wa klabu tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwapa bure wanachama wa klabu ambao wamekuwa na timu kwa muda mrefu, wameshatoka jasho sana na Simba hivyo tutawapa hisa za timu bure," alisema MO.

Hata hivyo MO aliongeza kuwa yupo tayari kwa lolote kama katika mkutano mkuu wa Jumapili watamnyima nafasi ya kuwekeza katika klabu ya Simba na kueleza kuwa anachoamini kwa sasa Simba haiitaji mdhamini bali Simba inahitaji mwekezaji.

"Mimi wakininyima kwa moyo mweupe kabisa sina tatizo na hili jambo hata likifanikiwa halitakamilika kesho linaweza kuchukua muda sababu kuna mambo ya kufanyiwa marekebisho na kusaini mikataba ila kama nikiona mambo yanakwenda sawa kwa hicho kipindi nitaangalia jinsi gani nitaisaidia Simba sababu nina mapenzi nayo," aliongeza MO.