HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

LEO NI LEO MISS ILALA 2016 JIJINI DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Washiriki wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha baada ya mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. warembo hao wanataraji kupanda jukwaani Septemba 9, 2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro 

Warembo wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.

SHINDANO la Kumsaka Miss Ilala 2016 linafanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Mbali na kufanyika kwa shindano hilo pia litatumika kuadhimisha miaka 20 ya shindano la Miss Ilala tangu kuanza kufanyika kwake na warembo mbalimbali waliowahi kushiriki na kushinda taji hilo watahudhuria.

Mratibu wa shindano hilo, Erick Othman kutoka Kampuni ya Gogetime Enterprises ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa warembo 14 watapanda jukwaani kuwania taji hilo pamoja na tiketi ya kushiriki shindano la Kitaifa la Miss Tanzania 2016 linalotaraji kufanyika baadae mwaka huu. 

Othman alisema mgeni rasmi katika shindano hilo leo hii ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, huku burudani ikitolewa na wasanii mbalimbali akiwepo Rubby. 

Amewataja warembo wanaoshindana kuwania taji hilo kuwa ni Osmunda Mbeyela, Mercy Zephania, Melody Tryphone, Dalena David, Nuru Kondo, Julitha Kabete, Sporah Luhende, Queen Nazil, Lilian Omolo, Mariam Maabad, Brenda Allan, Sabrina Halifa, Agriphina Nathaniel na Grace Malikita.

Kwa upande wa zawadi za washindi, Kitundu alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh milioni moja pamoja na portable TV kutoka Startimes, huku mshindi wa pili akipata sh 700,000 na kingamuzi, na mshindi wa tatu akipata sh 300,000 na kingamuzi pia.

Alisema kuwa mshindi wan ne atapata sh 200,000 na watano atapata sh 150,000 pamoja na kingamuzi huku warembo wengine watapata kifuta jasho cha sh 50,000. 

Kiingilio katika shindano hilo ni Sh 50,000 kawaida na Sh 100,000 kwa viti maalum (VIP).

MISS ILALA TALENT SHOW 2016 ILIVYOBAMBA NDANI YA HIGH SPIRIT DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

 Warembo 15 wanaowania taji la Miss Ilala 2016, usiku wa kuamkia leo walichuana vikali katika kutafuta mrembo mwenye kipaji ambapo warembo wote walishindana kwa kuonesha vipaji vyao vya ubunifu, uchezaji muziki na uimbaji wa nyimbo mbalimbali.
 Hii ndio tano bora ya Warembo wenye Vijapaji kutoka Miss Ilala 2016.
 Washiriki mbalimbali wakionesha ujuzi wao kulingana na vipaji walivyo jaaliwa.

 mashabiki wakishangilia
Wapenzi na Mashabiki wa sanaa ya Urembo nchini wakifuatilia shindano hilo.

SHINDANO LA MISS ILALA 2016 LAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo. Shindano hilo limezinduliwa sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya Miss Ilala tangu ianze mwaka 1996. 
 Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo.
 Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo. Source: Father Kidevu Blog.
 Mwandaaji wa shindano la Miss Ilala 2016, Teddy Kitundu ambaye pia ni diwani wa viti Maalum Ilala, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa shindano hilo Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia kulia ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania , Bossco Majaliwa (kulia) na Mkuu wa Itifaki wa Kamati hiyo, Albert Makoye. Miss Ilala inafanyika ikiwa ni mwaka wa 20 tangu lianze shindano hilo mwaka 1996.
 Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akizungumza kwaniaba ya Kamati katika uzinduzi huo.
 Mmoja wa wadhamini akizungumza katika uzinduzi huo. 
 Mratibu wa shindano hilo la Miss Ilala 2016, Eric akizungumza
 Warembo waliowahi kushirikishindano la Miss Ilala wakifungua shampein katika uzinduzi huo.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa akigonganisha glasi na warembo wanaowania taji la Miss Ilala 2016.
 Warembo wakigonganisha glasi na wadau wa urembo waliohudhuria hafla hiyo.
 Warembo wakigonganisha glasi na wadau wa urembo waliohudhuria hafla hiyo.
 Mdau akilamba unikoni na mlimbwende wa zamani wa Miss Tanzania
 Warembo wakijiselfisha wakati wa hafla hiyo
 Wadau wa urembo wakiwa katika hafla hiyo.
 Mwandishi wa habari za michezo na sanaa ya urembo, Michael Mauruce (kushoto)  akimsikiliza Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.