HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MAMA JANETH MAGUFULI ATOA VYAKULA KWA VITUO NANE VYA KULELEA WATOTO YATIMA

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Hajat Mwanaisha Magambo mkuu wa kituo cha New Life Orphanage cha Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa  vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopewa vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  Ikulu  jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017. Vituo vilivyopkea vyakula hivyo ni pamoja na New Life kilichopo Boko Dawasco chanye watoto 121, Charambe Islamic kilichopo Charambe (watoto 54), Mwandaliwa Centre kilichopo Mbweni (watoto 94) Al Madina Children Home cha Tandale ( watoto 65), Ijangozaidia Orphanage Centre kilichopo Sinza (watoto 1030, Azam Orphanage kilichopo Mbagala (watoto 51), Hiari Orphanage kilichopo Chang'ombe (watoto41) na CHAKUWAMA (watoto 64) kilichipo Sinza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsabahi mmoja wa yatima maaba ya kumkabidhi vyakula Hajat Mwanaisha Magambo kutoka kituo cha New Life Orphanage cha Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa  vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopewa vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  Ikulu  jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kabla ya kuwakabidhi vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr Ikulu  jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimtakia heri mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Mama yake Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini

MAMA JANETH MAGUFULI AMKARIBISHA MAMA SIZAKELE ZUMA OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa ameongozana na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, wakati  wakielekea kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  wakiwa kwenye mazungumzo na wasaidizi wao kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akifurahia jambo na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  alipomkaribisha kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia)  na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  wakipata picha ya kumbukumbu alipomkaribisha kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia)  na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  wakipata picha ya kumbukumbu na wasaidizi wao alipomkaribisha kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia)  akimsindikiza  Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, alipomkaribisha kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia)  akipeana mikono na  Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, alipomkaribisha kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii
Kikundi cha matarumbeta cha Usambara kikiwatumbuiza Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) na  Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma alipomkaribisha mgeni wake huyo kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii. 

PICHA NA IKULU

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHI VIFAA KWA KITUO CHA AFYA BOGOWA WILAYA YA MKOANI KIJIJI CHA MGANYAGENI PEMBA.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Mhe Hemed Suleiman alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa kwa ajili ya kukabidhi Vifaa kwa ajili ya Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho cha Afya Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya Mkoani Pemba wakati alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa kukabidhi vifaa vya afya katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Balozi wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr. Mbwana Shoka, akitowa maelezo wakati wakitembelea Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr. Mbwana Shoka akitowa maelezo wakati wa ziara ya Mke wa Rais wa Zanzibar kutembelea kituo hicho na kukabidhi vifaa vya Afya kwa Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Harusi Siad Suleiman wakati wa hafla hiyo, katika viwanja vya Kituo hicho Bogowa Mkanyageni Pemba.
Mfanyakazi wa Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba Mwanahawa Mohammed Abdallah akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi na wananchi wa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.  
Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr Mbwana Shoka akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya chumba cha wazazi kwa Kituo hicho cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba. 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pembe Mhe. Omar Khamis akizungumza wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein. wakati wa kukabidgi vifaa vya Afya kwa Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba Wilaya ya Mkoani.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Balozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis wakati wa hafla hiyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya afya kwa Chumba cha Wazazi katika Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakifuatilia hafla hio ya kukabidhi vifaa vya afya kwa ajili ya chumba cha Wazazi katika Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said Suleiman akizungumza kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Wananchi wa Jimbo la Mkanyageni wakati wa kukabidhi Vifaa vya Afya kwa ajili ya Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya Afya katika Kituo cha Bogowa Mkanyageni kwa ajili ya Wazazi wanaofika katika Kituo hicho kuja kujifungua.
Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na wananchi hao na kutowa nasaha zake kabla ya kukabidhi vifaa vya afya kwa chumba cha wazazi katika kituo cha Afya Bogowa Mkanygeni Pemba.



Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashuka kwa Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashine ya kupimia Sukari katika Kituo hicho kwa  Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashine ya kupimia presha wazazi katika kituo hicho kwa Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi pempasi kwa ajili ya watoto wanaozaliwa katika kituo hicho akipkea Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, akitowa shukrani kwa msaada huo kwa kituo hicho. kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.

Viongozi wa meza kuu wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi vifaa vya afya katika kituo cha afya bogowa mkanyageni Wilaya Mkoani Pemba.

Imetayarishwa na Othman Maulid  

Zanzinews.Blog .com

MAMA MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA KUMUAGA PAROKO WA KANISA LA MTAKATIFU PETRO FR. STEPHANO KAOMBWE ANAYEHAMIA CHANG'OMBE

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea machache alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru (kushoto) na Fr. Asis Sylvester Mendoca (wa pili kulia) wakimsikiliza Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke, akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa akiongoza sala wakati wa hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe,, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na waumini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, Fr. Asis Sylvester Mendoca baada ya kuhitimisha hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo April 2, 2017 ameungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.

Kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rigambwa na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mama Magufuli amemtakia kila la heri Fr. Kaombwe katika kituo kipya cha kazi, na pia amempa salamu toka kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amemtakia heri na fanaka kwa uhamisho huo.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa alimpongeza Fr. Kaombwe kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akihudumu katika Paroko hiyo kwa takriban miaka mitatu na nusu, na pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Fr. Asis Sylvester Mendoca ambaye atakaimu nafasi ya Fr. Kaombwe.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, amempongeza Fr. Kaombwe kwa mambo mengi aliyoyafanya kanisani hapo, na kwa niaba ya jumuiya ametoa shukurani nyingi kwa huduma alizokuwa akiwapatia.