HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

15 WAVULIWA MADARAKA KWA KUANDIKISHA WANAFUNZI HEWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, imewavua madaraka walimu wakuu 15 wa shule za msingi wilayani humo, kwa kosa la kuandikisha wanafunzi hewa 883 na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya Sh milioni 3.4.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege, alisema hatua hiyo imetekelezwa baada ya kufanya uchunguzi wa kuhakiki wa wanafunzi hao kwa kipindi cha kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka jana katika shule za msingi.
Berege alisema katika uhakiki wa kwanza uliofanyika Agosti hadi Oktoba, mwaka jana, ilibainika kuwepo kwa wanafunzi hewa 639.
Aliongeza kuwa katika uhakiki mwingine uliofanyika Oktoba mwaka huo kwa kushirikiana Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) walibainika wanafunzi hewa 244.
Alisema kutokana na tatizo hilo, halmashauri hiyo iliwaita walimu hao wakuu na kuwataka warudishe fedha hizo na walikubali kuzirudisha fedha katika Ofisi ya Mkurugenzi kabla ya kuvuliwa madaraka yao rasmi kuanzia Desemba 7, mwaka huu walipokabidhiwa barua zao.
Mkurugenzi huyo aliwataja waliovuliwa madaraka na shule kwenye mabano kuwa ni Emmanuel Nkwabi (Mhama) aliyelipa Sh 56,000 Sita Kasangi (Mwakuzuka) aliyelipa Sh 132,000, Iman Gongo (Nyamigege) amelipa Sh 155,000, Fabian Mchiwa (Mwanyaguli) Sh 21,000 na Omari Masani (Ngaya) Sh 86,000.
Aliwataja wengine kuwa ni Vedastus Masonga (Buganzo) Shilingi 215,5000, Bernard Patroba (Nyamididi) Sh 142,000, Abbas Kirua (Gulla) aliyelipa Sh 26,000, Elisafi Mshana (Shishinulu) Sh 456,500, George Mabambi (Mbizi) Shilingi 68,000 na Hussen Said (Bukwangu) Shilingi 56,000.
Wengine ni Anthonia Peter (Chella) Sh 168,000, Godfrey Niwagira (Buyange) Sh 99,000, Aron Sizya (Kashishi) Sh 198,400 pamoja na Jovinus Katemi (Nyakadoni) aliyelipa Sh 99,000.

RAIS MAGUFURI AWATUMBUA WALIOTAKA KULA PESA ZA MAAFA MKOANI KAGERA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.
Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Waziri Mkuu, Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo
Kadhalika Rais Magufuli leo amepokea msaada wa Shilingi Milioni 545milioni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba, 2016.

KAMOGA MKURUGENZI MTEULE WA WILAYA YA MBULU AAMUA KUANZA NA MUNGU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.
 
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamoga.
 
Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake 

Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo ili awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu. 
Akiongea kwenye ibada ya Jumapili hii ndani ya Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati alipopewa nafasi na mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi ili asalimia Kanisa Mheshimiwa Kamonga alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na viongozi wengine kati halimashauri ya Mbulu.

Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata nafasi hii ya Ukurugenzi bado ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanya kufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya,alisema Kamoga

Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja na watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa! Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi na waumini walifanya maombi kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.

MKURUGENZI WA BUNDA APOKEA MADAWATI 90 KUTOKA KWA MBUNGE ESTER BULAYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jimbo la Bunda, Mkoani Mara Bi. Janeti Mayanja amepokea madawati 90 yalitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi. Ester Bulaya, ambapo hapo awali  madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo walikataa kupokea madawati hayo baadaya ya kuwa yameandikwa  jina la mbunge huyo pamoja na kuwa yamenunuliwa na fedha za Mfuko wa Jimbo.


Akizungumza leo kwa njia ya simu, Mkurugenzi  Mayanja alisema kuwa  amepokea madawati hayo jana  Agosti 12  kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Ester Bulaya baada ya kufutwa jina lake, ambapo madawati hayo tayari yamewasilishwa katika shule tatu zilikuwa na uhaba.

“Tulifanya kikao na Mbunge Bulaya na tukakubaliana kuwa ni vyema majina yake yakafutwa katika madawati hayo kwa vile yalinunuliwa kwa fedha  za Mfuko wa  Jimbo, lakini endapo mbunge atapenda kutupa madawati atakayonunua kwa  fedha zake binafsi  na kuandika majina yake hapo tutapokea kwa vile bado kuna tunauhitaji katika jimbo letu” alisema Mkurugenzi Mayanja

Alifafanua kuwa fedha zilizotumika  kununua  madawati hayo zilikuwa ni  fedha za Mfuko wa  Jimbo zinazotokana na ruzuku ya Serikali ambazo matumizi yake hupangwa na Ofisi ya Mbunge.

Madawati hayo 90 yalisambazwa katika shule tatu za Msingi zilizopo katika Jimbo la Bunda zilizokuwa na uhaba wa madawati  ambazo ni  Nyatwali, Nyerere na Ligamba,  zilizopewa madawati 30 kwa kila moja.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AAHIDI KUKOMESHA UFANYAJI KAZI WA MAZOEA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD),Athuman Juma akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mipango kamambe ya kukomesha wavamizi wa maeneo ya wazi ambayo yametambuliwa kuwa ni viwanja 52.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD), Athuman Juma akizungumza namna jinsi walivyojipana kukusanya mapato kwanjia za kieletroniki na mashine za EFD's kuhakikisha mapato hayapotei.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania,Eliya Mbonea akiuliza swali.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD),Athuman Juma akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Waandishi wa habari wakiwa makini kuchukua taarifa hiyo
Waandishi wa habari wakiwa makini kuchukua taarifa hiyo

Afisa Habari Mwandamizi wa Jiji la Arusha,Nteghenjwa Hoseah akizungumza jambo baada ya mkutano huo.