HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

SAIDA KAROLI ADAI KUACHANA NA MENEJA WAKE KULIMFANYA APOTEZE MWELEKEO KWENYE MUZIKI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amefunguka kwa kusema kuwa moja ya sababu ambayo ilimfanya apotee kwenye muziki ni kitendo cha kuachana na meneja wake.
Muimbaji huyo ambaye aliachana na meneja wake toka 2007, amedai kitendo hicho kilimfanya ashindwe kujisimamia na kumfanya ashuke kwenye muziki.

“Baada ya kuachana na meneja wangu sikuweza kujisimamia mimi mwenyewe na pia kwa wakati ule ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu muziki una mambo mengi na mimi nimekulia kijijini kwahiyo kujua baadhi ya vitu ilikuwa ngumu sana,” Saida aliiambia BBC.

“Sina nilipo kosea lakini najua kila kitu chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, simaanishi huo ndo mwisho wangu ila kwa kuwa nilianza na mtu, sasa unapomalizana naye ni kama unaanza maisha mapya ndio kitu kilicho nitokea mimi,” aliongeza.
Pia muimbaji huyo amesema kwa sasa anajipanga kuja kwa kishindo na kufanya mapinduzi katika muziki wa asili nchini.

DIAMOND KUMLIPA SAIDA KAROLI ASILIMIA 25 YA USAMBAZAJI WA NYIMBO YA "SALOME"

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Diamond amedai kuwa Saida Karoli atapata asilimia 25 ya mapato ya wimbo wa Salome.

Diamond amerudia baadhi ya vitu kwenye wimbo wake mpya ‘Salome’ aliomshirikisha Raymond kutoka kwenye wimbo wa ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli uliotoka takribani miaka 16 iliyopita.
Akiongea na 255 ya Clouds FM Jumatatu hii, hitmaker huyo wa Kidogo amesema kuwa walizungumza na uongozi wa Saida Karoli na kumpatia kiasi cha fedha pamoja na asilimia 25 ya usambazaji wa wimbo huo.
“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya kuisambaza nyimbo hiyo. Kila income ya usambazaji ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent,” amesema Diamond.
Mpaka sasa video ya ‘Salome’ ya Diamond ina siku mbili tangu ilipoachiwa kwenye mtandao wa YouTube lakini imefanikiwa kutazamwa mara 659k.