HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI (JWTZ) KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAANZA KWA SIKU YA KWANZA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waandishi wa Habari walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakinyanyua mikono kuashiria kuanza safari hiyo katika lango la Marangu.
Safari ya kupanda ikaanza katika lango la Marangu majira ya saa 5 asubuhi kila mmoja akiwa na nguvu za kutosha na shauku ya kutizama mandhari ya Mlima Kilimanjaro ambao siku ya kwanza safari inaanza kwa kupita katika msitu mnene.
Wapandaji waliokuwa wamevalia nguo za kuzuia baridi mapema wakati safari ya kupanda mlima inaanza baadae kidogo kidogo walilazimika kuzipunguza kwa sababu pindi unapotembea joto la mwili pia huongezeka.
Safari ya kupanda mlima kwa kundi hili la Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,George Waitara lilikuwa pia na ulinzi wa kutosha. 
Safari ya kupanda vilima vidogo ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro iliendelea.
Maeneo mengine yalikuwa ni ya Madaraja na Mito.
Hatimaye safari kafika eneo la Kisambioni ikiwa ni nusu ya safari ya kuelekea katika kituo cha Mandara ,eneo ambalo hutumika kwa ajili ya kupata chakula.
Baadae safari ya kuelekea kituo cha Mnadara ikaendeleo.
Maeneo mengine Washiriki walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata nguvu mpya ya kuendelea na safari.
Majira ya saa 12 jioni hatimaye Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku ya kwanza ikafika katika kituo cha Mandara na washiriki wakapata nafasi ya kupata picha ya pamoja na kupumzika kwa ajili ya siku ya pili kuendelea na safari ya kwenda kituo cha Horombo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.

Tanzania yetu maliasili zetu,Msimu wa sikukuu ndio huu

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Tanzania yetu maliasili zetu Hakuna jambo zuri kama kusherekea Sikukuu ukiwa kwenye mandhari  tulivu ambayo itakufanya ussosike na chakula kizuri  huku ukifanya vitu vipya au kuona vitu tofauti ambavyo huvioni mara kwa mara katika mzunguko wako wa maisha.

Msimu wa Sikukuu ndiyo huu!!! Fanya sikukuu yako kuwa ya kipekee kwa kutembelea HIFADHI ZA TAIFA. Tuendelee kusapoti Utalii wa Ndani kwa kutembelea #HifadhiZetu. More info piga 0784133217| 0765908073. 

HapaKaziTU

WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 55 YA UHURU WAKABIDHIWA VYETI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakiwemo Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Waandishi wa Habari wakishuka baada ya kupanda mlima huo kwa siku sita.Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Witara (Mwenye fimbo mstari wa mbele) na Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ardhini (JWTZ) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba (kushoto). 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipokea Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro walipofika katika lango la Marangu,Kippi akisalimiana na Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba. 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Waitara ,kiongozi wa msafara wa wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru akivishwa shada la maua mara baada ya kufika katika lango la Marangu. 
Meneja wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adeventure,Rahma Adam akisalimiana na Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika lango la Marangu. 
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Washiriki wa zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kufika katika lango la Marangu zilipo ofisi za KINAPA. 
Baadhi ya Washiriki wa changamoto ya upandaji Mlima Kilimanjaro baada ya kushuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Waioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Mstaafu George Waitara. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Naibu Kamnada wa kikosi cha ardhini,Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba aliyefanikiwa kufika kilele cha Gilman's umbali wa mita 5685 kutoka usawa wa Bahari. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Balozi Charles Sanga aliyefanikiwaa kufika kilele cha Stella umbali wa mita 5756. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Star Tv ,Ramadhan Mvungi baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari. .
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwanadishi wa Habari wa Clouds Media Group ,Kilimanjaro na Mwakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini ,Dixon Busagaga baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi ,Arusha ,Zulfa Musa baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari akiwa ni miongoni mwa wasicha wawili waliofika kileleni. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mtanzania ,Arusha,Eliya Mbonea baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru. 
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima,Charles Ndagulla mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Pascal Shelutete mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi makimkabidhi Cheti Askari wa Jeshi la Ulinzi ,Pte,Joyce Kaila baada ya kufanikwa kufika katika kilele cha Uhuru. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi akimkabidhi Cheti Askari wa Jeshi la Ulinzi,Ally Said baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti ,Mwandishi wa Habari ,Idd Uwesso baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Stella. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti ,Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlia Kilimanjaro,Charles Ngendo mara baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru. 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Waitara akiznungumza mara baada ya kushuka Mlima Kilimanjaro ambako timu ya Watu 36 wakiwemo Askari wa jeshi la Wananchi na Waaandishi wa Habari wamepanda mlima huo kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na askari wa jeshi la ulinzi waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro. 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro. 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waongoza watalii walioshiriki kufanikisha safari ya Waandishi wa Habari na Askari wa jeshi la Ulinzi kupanda mlima Kilimanjaro. Na Dixon Busagaga wa Blogu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune
Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .
   Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog, Mbarali, Mbeya .

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI ya Taifa ya Ruaha


Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu linakivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo amewataka wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.

Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .