NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.
Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.
“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez.
Taarifa zaidi zitawajia kadri zitakavyotufikia
TRENI YANUSURIKA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI, 17 WATIWA MBARONI
By: VIJIMAMBO on November 10, 2016 / comment : 0 Matukio, Treni, TRL
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
TRENI ya abiria inayofanya safari zake kati ya Kituo Kikuu cha Reli na maeneo ya Pugu Dar es Salaam maarufu kama ‘Treni ya Mwakyembe’ nusura ichomwe moto juzi, baada ya wananchi kudai kuchoshwa na usumbufu wa shirika hilo.
Wananchi hao walitaka warudishiwe nauli zao kwa kile walichodai Shirika la Reli Tanzania (TRL) limeshindwa kuwa na ratiba inayoeleweka.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la Majumbasita, baada ya treni hiyo kukaa kituoni hapo kwa muda mrefu bila kuambiwa kuambiwa chochote.
Hali hiyo iliwafanya abiria kuvamia kituo kidogo cha mawasiliano kilichopo eneo hilo wakitaka warejeshewe nauli zao vinginevyo wangekichoma moto pamoja na mabehewa ya treni hiyo.
Mwandishi aliwashuhudia abiria wakitaka kuingia ndani ya kituo hicho huku wakiwalazimisha wafanyakazi waliokuwapo wawarudishie fedha zao za nauli.
Purukushani hiyo iliyodumu kwa takribani saa mbili ilimalizika kwa abiria hao kuvunja vioo vya mabahewa ya treni vipatavyo 30.
Wafanyakazi kuona hivyo walijifungia ndani ya kituo hicho huku polisi waliokuwa wakisindikiza treni hiyo wakitimua mbio kunusuru maisha yao.
Baadhi ya abiria walisema tangu Ijumaa iliyopita wamekuwa wakipata usumbufu kwa kukatishiwa tiketi huku treni ikichelewa na wakati mwingine kutoonekana kabisa.
Walisema jambo hilo limekuwa likiwasababishia hasara na kuwalazimu kutafuta usafiri mwingine na kuchelewa kufika kwenye majukumu yao.
Kufuatia kukithiri vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya reli na treni vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji , Masanja Kadogosa imetoa onyo kwa wananchi kutofanya vitendo hivyo.
“Tukio hili si mara ya kwanza kujitokeza, lilijitokeza tarehe 24, 26 na 28 mwezi wa 10 na Novemba 7 Katika matukio hayo kulitokea uharibifu wa miundombonu na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi wa TRL akiwemo Mustapha Omary ambaye ameshonwa nyuzi 8 katika hospitali ya mnazi mmoja,” amesema.
Amesema kutokana na uharibifu huo, watuhumiwa 17 wanashikiliwa na jeshi la polisi na kwamba upepelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kadogosa amedai kuwa, wahusika wa fujo na uharibifu huo ni makondakta wa dalala kwa lengo la kutisha wananchi kutoutumia usafiri wa treni.
“Kuna watu wa daladala wanafikiri wataendelea kufanya fujo ili wananchi waone kuwa usafiri wa treni si salama wapande magari yao, sisi hatulazimishi wananchi kuutumia usafiri wetu ila kutokana na ubora wa huduma zetu wanakuja wenyewe. Pia hatusitishi kutoa huduma kwa sababu ya fujo zao sababu tutawatesa abiria wetu zaidi ya 21,000,”
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Reli, Simon Chillery amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wengine waliohusika.
WANANCHI WAILALAMIKIA TAZARA KWA KUFUNGA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM
By: VIJIMAMBO on September 26, 2016 / comment : 0 Kampuni ya Reli Tanzania, Matukio, TRL, Wananchi
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam jana.
Wananchi wakivusha relini pikipiki yao.
Pikipiki ikivushwa.
Waendesha bodaboda wakivusha pikipiki zao kwenye reli baada ya kufungwa kwa muda barabara katika makutano ya Reli ya Tazara na Barabara ya Mombasa Moshi Baa Dar es Salaam jana wakati mafundi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wakifanya ukarabati katika eneo hilo.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam.
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) imelalamikiwa na wananchi kwa kutozingatia muda muafaka wa kufanyia ukarabati wa reli zake jambo linalowaletea usumbufu.
Malalamiko hayo waliyatoa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu kadhia waliopata baada ya kufungwa kwa muda Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa kupisha ukarabati eneo la reli inayokutana na barabara hiyo.
"Kazi ya ukarabati wanayoifanya ni nzuri lakini wangekuwa wakiifanya nyakati za usiku ili kuepusha usumbufu huu tunao upata wa kuvusha pikipiki zetu relini" alisema Gedion Robert.
Robert alisema katika nchi za wenzetu kazi za kusafisha miji na ukarabati wa namna hii hufanyika usiku ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia barabara kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Mkazi mwingine kwa Diwani Stellah Urio alisema amelazimika kulipa sh. 400 kutoka kwa Diwani hadi Relini ambapo pia alilipa sh. 400 baada ya kubadilisha gari ili kufika Ukonga Mombasa na kujikuta akitumia sh.800 badala ya 400.
Jitihada za kumpata msemaji wa Tazara , Conrad Simuchile, ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kufika ofisini kwake na kuambiwa mwandishi arudi baadae alikuwa nje ya ofisi kikazi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KESHO YASOGEZWA MBELE, KUONDOKA JUMATANO SEPTEMBA 14, 2016
By: VIJIMAMBO on September 12, 2016 / comment : 0 Habari, Treni, TRL
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusogeza mbele kwa siku moja safari ya treni ya abiria ya Jumanne kwenda bara kutoka Dar es Salaam. Treni hiyo itaondoka Jumatano Septemba 14, 2016 saa 9 alasiri.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kusogezwa mbele ni kutokana na kipande cha treni kuitoka Kigoma kuchelewa kufika Tabora. Treni hiyo wakati ikienda Kigoma ilicheleweshwa kufika Kigoma baada ya treni ya mizigo kupata ajali kati ya stesheni za Kazuramimba na Luiche..
Uongozi wa TRL unawaomba radhi abiria na wananchi kwa ujumla kwa usumbufu utakaojitokeza
Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,
Septemba 12, 2016
TRL YATANGAZA NAULI MPYA TRENI YA PUGU
By: VIJIMAMBO on August 31, 2016 / comment : 0 Habari, Treni, TRL
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
NAULI ya abiria wa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es Salaam, imepanda kutoka Sh 400 ya awali hadi 600.
Tozo hiyo ya nauli mpya inatarajiwa kuanza rasmi Septemba mosi, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Ng’hwani Kudema, alisema viwango hivyo vya nauli vilivyokokotolewa na Mamlaka ya Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vimepanda kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu.
“Baada ya siku 14 nauli hizi zitaanza kutozwa kwa mujibu wa utaratibu na hili tutabandika matangazo. Hadi kufikia Septemba 13, mwaka huu nauli itakayokuwa inatozwa ni shilingi 600 kwa mtu mzima na shilingi 100 kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,” alisema Kudema
Alisema wakati wa majaribio ya treni hiyo Agosti mosi, mwaka huu, walikuwa na mabehewa 10 lakini kutokana na mahitaji ya usafiri huo kuwa mkubwa, walilazimika kuongeza mabehewa ambayo kwa sasa yamefika 18.
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mmoja wa abiria akipanda ndani ya Behewa Dar es Salaam jana akielekea Kigoma kwa kutumia usafiri wa haraka (EXPRESS), ambaye alifahamika kwa jina la Fatuma Kininga, aliushukuru uongozi mzima wa Shirika la Reli Tanzania, kwa maamuzi yao ya kuanzisha usafiri huo na kuutaja kuwa ni mkombozi kwao.
Amesema kubwa hasa linalowasumbua ni upatikanaji wa tiketi ambao amesemani mgumu kiasi, Anawaomba wanaotumia usafiri huo kutunza mazingira bila shuruti kwa kushirikiana na wafanya kazi kuona ni mali yake, kutokanyaga viti, kula vitu na kutupa ndani ya mabehewa hayo, kuweka sheria kali na kuendelea kupewa elimu kila mara kwa abiria, na kila mmoja kumwelimisha mwenzake na kuwa mlinzi kwa mwenzake. Hayo aliyasema jana wakati alipokuwa ndani ya behewa Dar es Salaama.
(PICHA ZOTE NA KAHMISI MUSSA)
Abiria wakiwa ndani ya Behewa tayari kuelekea Bara.
SAFARI ZA MAJARIBIO ZA TRENI YA PUGU KUANZA LEO JUMATATU NA JUMANNE KUWA BURE
By: VIJIMAMBO on August 01, 2016 / comment : 0 Banana (Njia panda Segerea), FFU Mombasa, Gongo la mboto, Habari, Kamata(Kariakoo), Kampuni ya Reli Tanzania, Karakata, Mwisho wa Lami, Pugu stesheni, SS Bakhressa, TRL, Vingunguti Mbuzi
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Huduma ya 2 ya treni ya Jiji kutoka Pugu kwenda kituo kikuu cha Dar es Salaam kuanza leo Jumatatu Agosti 01, 2016 saa 12 asubuhi.
Aidha taarifa Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL ) inafafanua huduma hiyo ya majaribio ya siku 2 yaani Jumatatu na Jumanne itakuwa bure kwa Wakazi wa vituo husika.
Vituo hivyo ni pamoja na Pugu stesheni, Mwisho wa Lami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana (Njia panda Segerea) na Karakata. Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi, SS Bakhressa, Kamata(Kariakoo) na Kituo kikuu cha reli Dar es Salaam.
Huduma hiyo itakuwa ya awamu 2 ya safari 3 kila awamu. Safari ya kwanza ya awamu ya 2 itaanza saa 9:55 Alasiri kutoka Dar stesheni.
Wito unatolewa kwa Wasafiri wa treni hiyo kuzingatia maelekezo ya Maafisa wa TRL watakaosimamia safari hiyo ya majaribio na kutoa ushirikiano kikamilifu.
TRL YATANGAZA MABADILIKO YA MUDA WA TRENI KUONDOKA DAR KUELEKA BARA
By: VIJIMAMBO on July 29, 2016 / comment : 0 Habari, Treni, TRL
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kampuni ya Reli ya Tanzania (TRL) imefanya mabadiliko ya muda wa Treni ya Abiria kulekea mikoa ya Kigoma na Mwanza ambapo kuanzia tarehe 02 Agosti 2016 Treni itaanza kuondoka saa tisa(9) mchana badala ya saa 11 jioni muda wa sasa.
Mabadiliko hayo yametangazwa na Meneja Uhusiano wa TRL Midladjy Maez wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Maez amesema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya huduma za Jiji kutoka kituo Kikuu cha Reli cha Dar es Salaam kwenda Pugu ambayo itaanza kutoa huduma mapema siku ya Jumatatu ya tarehe 01/08/2016.
Aliongeza kuwa mabadiliko hayo yanahusu treni za abiria za huduma za kawaida zinazoondoka siku za Jumanne na Ijuma na kubainisha kuwa kwa upande wa huduma za treni ya Deluxe zitaendelea na muda wake wa kawaida.
“Uongozi umeamua kufanya mabadiliko haya kwa sababu za kiusalama zaidi kwani mabadiliko haya yataepusha muingiliano unaoweza kupelekea ajali na kuongeza kuwa kwa safari za kutoka Kigoma na Mwanza muda umebaki uleule”. Alisema Maez.
Meneja Uhusiano huyo aliongeza kuwa huduma za treni ya Jiji kwenda Pugu itakuwa na vituo 10 ambavyoa alivitaja kuwa ni pamoja na Pugu Stesheni, Gongo la Mboto,FFU Mombasa, Banana, (njia panda kwenda Stesheni), na karakata.
Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi,SS Bhakressa, Kamata na Kituo Kikuu cha reli Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa huduma hiyo itakuwa na awamu mbili asubuhi na Alasiri ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Pugu saa 12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar es Salaam sa 12:55 asubuhi na kufanya safari tatu zitakazomalizika saa 05:15 asubuhi.
Jioni kutakuwa na safari tatu ambapo treni itaondoka kituo cha Dar es Salaam saa 09:55 alasiri kwenda Pugu na kuwasili saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kuja Kituo Kikuu cha Dar es Salaam saa 03:20 usiku.
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...

Serikali imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kuharakisha maboresho ya mitaala na mafunzo ya Uhasibu ili...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Huma...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015
November 01, 2015
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014