HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

UPDATES: MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU IMEFUTA KESI YA UCHOCHEZI ILIYOKUWA INAMKABILI MBUNGE WA UBUNGO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyaondoa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (46). Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, leo ameyaondoa mashtaka hayo mahakamani hapo kwa sababu hati ya mashtaka ilikuwa na utata na aiendani na kifungu cha 132 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema kifungu hicho cha sheria kinataka kosa lielezwe kwa uwazi ' kinaga ubaga'.

Alisema katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Kubenea ya kusambaza habari ya uongo yenye kichwa cha habari 'yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar' ambayo ingeweza kuleta uvunjifu wa amani, Hakimu Mashauri alisema maneno hayo pekee kisheria siyo kosa.

Akiendelea kutoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema upande wa mashtaka ulishindwa kueleza maneno yenyewe hasa ya uchochezi yenye lengo la uvunjifu wa amani.

Hivyo, Hakimu Mashauri aliiondoa kesi hiyo mahakamani hapo na mshtakiwa akaachiwa huru na kwamba upande wa mashtaka unaweza kumshtaki upya.

Hata hivyo baada ya Kubenea kuachiwa huru alikamatwa na kupelekwa polisi kati na baadaye akaachiwa kwa dhamana.

HIZI NI SABABU ZA EDWARD LOWASSA KUKAMATWA NA POLISI JANA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana alikamatwa na polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkutano bila kibali. 

Lowassa, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alikuwa njiani akitokea mkoani Kagera, ikiwa ni mwendelezo wa ziara za viongozi wa chama hicho katika kanda zake kutekeleza Operesheni Kata Funua inayohusisha mikutano ya ndani. Hata hivyo, aliachiwa jana jioni. 

Akiwa ameongozana na viongozi na makada wa Chadema, Lowassa aliingia Geita saa 9:30 alasiri na kupokewa na umati wa wananchi waliojitokeza eneo la Nyankumbu, tayari kwa safari ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Nkome. 

Viongozi wengine waliokuwamo kwenye msafara huo ni Profesa Mwesiga Baregu, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Hamis Mgeja, ambaye ni kada wa chama hicho. 

Msafara huo uliokuwa wa magari matano, ukisindikizwa na pikipiki na wafuasi kadhaa wa chama hicho, ulipitia makutano ya barabara mjini Geita na kukutana na magari ya polisi yaliyosheheni askari wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD), Ally Kitumbo. 

Bila kuingilia msafara huo, magari ya polisi yaliufuatilia kwa nyuma ulipokuwa ukielekea Kata ya Nkome. 

Hali ya hewa ilichafuka baada ya msafara kufika eneo la Soko Kuu wakati wananchi walipouzuia wakitaka kumsalimia Lowassa, ambaye aligombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita. 

Kiongozi huyo alilazimika kujitokeza juu ya gari lake kuwapungia na baada ya kelele za ‘njaa, njaa, njaa’ kusikika eneo hilo, Lowassa alitumia kipaza sauti kuwaomba wananchi wawe watulivu na wawaruhusu waendelee na safari yao kuwahi mkutano wa kampeni. 

“Ndugu zangu wana-Geita, natamani kuzungumza nanyi lakini sheria inanibana. Naomba muwe watulivu na mturuhusu tuendelee na msafara kuwahi mkutano wa kampeni Nkome,” alisema Lowassa. 

Askari hao wakiongozwa na OCD, walimfuata Lowassa na kumuamuru yeye na msafara wake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano. Wakati wa kuelekea kituoni, gari lake lilitanguliwa mbele na la polisi na nyuma kulikuwa na jingine la jeshi hilo. 

Kitendo hicho kiliwafanya wananchi waliokuwa na hamu ya kumsikiliza kiongozi huyo kuongozana kwenda kituoni, jambo lililoibua taharuki na polisi kuwatawanya kwa kufyatua mabomu ya machozi.

Waandishi wapigwa
Pamoja na kuwatawanya wananchi kwa mabomu, askari hao pia waliwapiga kwa mikanda na fimbo waandishi wa habari waliokuwa wakifanya kazi yao eneo hilo. 

Hali ilivyokuwa kituoni 
Baada ya kuwasili kituoni huku polisi wakiendelea kuwazuia wananchi, Lowassa alisalia ndani ya gari lake hadi hali ilipotulia na kutakiwa kuingia kituoni. 

Ni magari mawili pekee; la Lowassa na la Profesa Baregu, yaliyoruhusiwa kuingia eneo la polisi huku viongozi wengine kama Singo Benson ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, na Upendo Peneza (Mbunge wa Viti Maalumu), wakitakiwa kusubiri nje. 

Kitendo cha wananchi kuzidi kufurika kituoni hapo, kiliwafanya polisi kuimarisha ulinzi, wakizuia mtu yeyote kukatiza wala kusogelea eneo hilo. Licha ya kuzingira kituo cha polisi, askari walitanda barabara inayoelekea ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambako pia wananchi walizuiwa kukatiza. 

Lowassa apitishwa uani
Baada ya kuona wananchi wanazidi kujaa kituoni, polisi waliamua kumtoa Lowassa kupitia mlango wa nyuma na kumhamishia ofisini kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Mponjoli Mwabulambo.

 Kama ilivyokuwa Kituo cha Kikuu cha Polisi, ulinzi pia uliimarishwa eneo lote la ofisi ya RPC baada ya Lowassa kuhamishiwa huko na wananchi kupata taarifa. 

Kiongozi huyo aliyehamia Chadema akitokea CCM mwaka 2015 aliachiwa jana jioni. Kamanda Mwabulambo alisema hawakumkamata bali walizuia msafara huo kwa ajili ya usalama wake. 

Akizungumzia suala hilo, Peneza alisema huo ni muendelezo wa ukandamizaji dhidi ya viongozi wa Chadema unaofanywa na polisi mkoani Geita, akitoa mfano kitendo cha yeye kuhojiwa kwa saa kadhaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa madai ya uchochezi alipohutubia mkutano wa hadhara na kusema nchi inakabiliwa na njaa. 

Lowassa: Mshikamano Ukawa utaing’oa CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa mshikamano wa mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea kuing’oa CCM madarakani.
“Wameanza mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha viongozi wetu maneno,” amesema Lowassa mjini Biharamulo ambaye ameongozana na Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.
“Wanaandika uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji Ematasia... mimi sikwenda huko, lakini mbinu zao hizi wananchi wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko inapotea,” amesema.
Lowassa ambaye ametokea Zanzibar alikoshiriki uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Dimani kwa upande wa CUF amesema viongozi wa vyama vya upinzani wana mshikamano mkubwa na kuwataka wanachama wao kuiga mfano huo.
“Katika ziara zetu hizi za kuimarisha chama chetu pia tunaimarisha mshikamano miongoni mwetu sisi wapinzani... CCM wanapata kiwewe na tunawaambia hata wafanyeje mabadiliko hayaepukiki, watawatia ndani viongozi wetu kwa hila lakini wajue hiyo ndiyo inazidisha vuguvugu. Huu ni upepo unaovuma kote duniani hivi sasa wajifunze yaliyotokea Gambia, Ghana na kwengineko,” amesema Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, aligombea urais na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais John Magufuli.

LOWASSA, MAALIM SEIF KUSHAMBULIA JUKWAA DIMANI

Vigogo wawili wa siasa za upinzani nchini, Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad kesho watapanda jukwaani katika Skuli ya Fuoni, Zanzibar kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Dimani kwa tiketi ya CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhan.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani na Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali iliyopita, waligombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, mtawalia.
Uchaguzi huo wa Dimani, utafanyika Jumapili Januari 22, kujaza nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Hafidh Ally Tahir aliyefariki dunia Novemba 11, mwaka jana katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Chini ya ushirikiano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana Chadema kilitangaza utaratibu jinsi vigogo wake watakavyoshiriki kampeni za uchaguzi huo kwa staili tofauti ili kuhakikisha mshirika wake CUF anaibuka kidedea.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alisema jana kwamba kesho, Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, atakuwa kiongozi wa kwanza wa Chadema kuhudhuria kampeni hizo akishirikiana na Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF.

KUELEKEA KRISMASI: BARAZA LA VIJANA CHADEMA ARUSHA MJINI WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA MKOA MT MERU KUOKOA WENYE UHITAJI

VIJANA kutoka Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Arusha Mjini wakiungwa mkonoba baadhiya wananchi wengine wamefanya zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia hospitali yaMt Meru inayokabiliwa na upungufu mkubwa wa damu hali inayochangia ongezeko la vifo hasa akina mama wakati wa kujifungua. 

Akizungumza jana katika katika Hopsitali ya Mt Meru, mratibu wa zoezi hilo kwa upande wa wachagiaji, Katibu wa BAVICHA Wilaya ya Arusha Mjini ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Glory Kaaya alisema zoezi hilo limefanyika maalum kama tukio la kuaga mwaka huu wa 2016 kwa kuwahamsiaha vijana wenzake na wanajamii wengine kujitolea kuchangia na kusaidia kupunguza upungufu wa damu katika hospitali ya Mt Meruwakiamini mchango wao utasaidia kuokoa maisha ya watu wengi.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliojitokeza kuunga mkono zoezi hilo ni pamoja na Mbunge wa Simanjiro Mh James Olemiya, Naibu Meya Jiji la Arusha Viola Likindikoki pamoja na baadhi ya madiwani wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha akiwemo Ddiwani Ephata Nanyaro wa Kata ya Levolosi na Rick Moiro wa Kata ya Moshono.
Wataalamu wa afya wa Hopsitali ya Mt Meru ya Jijini Arusha wakiwa katika maandalizi ya kufanikisha zoezi la kutoa damu kutoka kwa wachangiaji ambao walijitokeza jana kusaidia upungufu uliopo hospitalini hapo. Wengine pichani ni baadhi yaviongozi na wanachama wabaraza la vijana la CHADEMA wilaya ya Arusha Mjini waliojitokeza kuchangia damu kwa hiyari. 
Sehemu ya damu ambayo ilipatikana jana itakayowafaa wahitaji na kusaidia tatizo la upungufu wa damu 
Mwenyekiti waBAVICHA Arusha Mjini ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini Innocent J Kisanyage akijaza fomu maalumu kablaBya kutolewa damu
Mtaalamu wa afya akiendelea nahuduma ya uchangiaji damu
Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Ephata Nanyaro akiendelea kutolewa damu 

PICHA N AMAELEZO: ARUSHA255 BLOG

Lowassa Afunguka Kuhusu Mgogoro Unaoendelea Ndani ya Chama cha CUF

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amevunja ukimya kuhusu mgogoro wa uhalali wa Uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa unaoendelea ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF) ambao umekuwa ukihusishwa naye tangu awali.

Lowassa ambaye alitajwa na Profesa Lipumba kuwa chanzo cha yeye kujiuzulu kabla ya kurejea tena miezi 9 baadae kutengua uamuzi wake, amesema kuwa shida za chama hicho ni shida za vyama vyote vinavyounda Ukawa.

Mwanasiasa huyo mkongwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ametumia ukurasa wake wa Facebook kueleza jinsi ambavyo Ukawa inalibeba tatizo la mgogoro wa CUF.

“CUF ni wenzetu katika Ukawa. Shida zao ni shida zetu, vita vyao ni vita vyetu, kushindwa kwao ni kushindwa kwetu, ushindi wao ni ushindi wetu,” aliandika Lowassa.

Kauli hiyo ya Lowassa imekuja miezi michache baada viongozi wa Ukawa kueleza msimamo wao kuwa hawamtambui Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na kwamba wataendelea kushirikiana na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Naye Profesa Lipumba amekuwa akieleza kuwa hayuko tayari kuona Chadema au Lowassa wanakinunua chama hicho.

Hivi karibuni, Ukawa wameweka msimamo wao kuwa watawasimamisha wagombea wa pamoja katika uchaguzi mdogo utakaofanyika mwakani.

Hata hivyo, kumekuwa na changamoto baada ya pande mbili zinazovutana ndani ya CUF kila mmoja kutangaza kuwasimamisha wagombea wake huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiweka msimamo kuwa ili iwatambue wagombea wa chama hicho ni lazima fomu zao zisainiwe na pande mbili zinazovutana.

Miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Profesa Lipumba alionekana akimtambulisha Lowassa mbele ya waandishi wabari na kujibu maswali mengi yaliyoelekezwa kwake lakini siku chache baadae alitangaza kujiuzulu akida moyo wake unamsuta hawezi kumuunga mkono mwanasiasa huyo.

ZITTO KABWE AMTEMBELEA LEMA MAHABUSU, ATOA NENO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Jana  Ijumaa desemba 2/2016 nilipata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza Kuvu la Arusha. Nilimtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati Za kutafuta na kulinda Haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa Sana na ukiukwaji mkubwa wa Haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona Ni bora akae ndani Mpaka hapo Dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka Mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.

Amemshukuru Mungu Kwa kumpa Mke jasiri anayempa moyo na Ndio ngome yake Kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka Haki kutendeka Katika uendeshaji wa Nchi yetu. Siku zote Haki hushinda

CHADEMA KUKUSANYA BILIONI 13.9 KWA MWAKA KUPITIA KADI MPYA ZA WANACHAMA ZITAKAZOANZA KUTOLEWA MWAKANI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Chadema imetangaza kuwa Januari itaanza kutumia kadi mpya za uanachama za kielektroniki, zitakazoiwezesha kukusanya Sh13.9 bilioni kwa mwaka na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali.

Mkakati huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika mkoani Morogoro. Tofauti na Mbowe, viongozi wengine wa chama hicho walioko mikaoni ni Edward Lowassa aliyeko Dodoma na Frederick Sumaye ambaye yupo Singida.

Mbowe alisema mfumo huo utasaidia pia kudhibiti baadhi ya viongozi wasio waaminifu, wanaotumia mwanya wa kuuza kadi na kushindwa kuwasilisha fedha kwenye hazina ya chama.

Alisema kwa mfumo huo mpya, kama Chadema itakuwa na wastani wa wanachama 100,000 katika wilaya moja na kila mmoja kulipa ada ya Sh1,000 kwa mwaka, maana yake itaingiza Sh100 milioni.

Kwa hoja hiyo ya Mbowe, ikiwa chama hicho kitakuwa na wastani wa wanachama 100,000 katika kila wilaya za Tanzania Bara ambazo ni 139, Chadema itakuwa na uwezo wa kukusanya Sh13.9  bilioni kila mwaka.

Vyama vya siasa vinapata ruzuku kwa mujibu wa sheria na ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilibainisha kuwa jumla ya Sh67.7 bilioni zililipwa na Serikali kwa vyama vya siasa katika mwaka kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka wa fedha 2009/2010 mpaka 2012/2013. Fedha ambazo kwa mujibu wa CAG zilikuwa hazijakaguliwa kisheria.

Ikilinganishwa na mkakati mpya wa Chadema, fedha hizo ni ndogo katika kuhudumia shughuli za chama nchi nzima.

Mbowe alisema Chadema imeamua kuhakiki wanachama wake ili ifikapo Januari iwe tayari imemaliza kazi hiyo na kuingia rasmi katika mfumo mpya, utakaokisaidia kuondokana na dhana ya utegemezi wa ruzuku kutoka serikalini.

Alisema ili chama kipige hatua na kuondokana na utegemezi wa ruzuku serikalini, wamekusudia kuingia katika mfumo wa kupata mapato kutoka ndani ya wanachama kupitia ulipaji wa ada.

Mbowe alizungumza na wanachama hao kutoka ngazi za vitongoji, vijiji, kata na wilaya waliohudhuria mkutano mkuu maalumu wenye lengo la kuwakumbusha mambo mbalimbali ya kuimarisha chama hicho baada ya Serikali ya Rais Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara.

“Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, Chadema itakuwa tayari imefanya utambuzi wa wanachama wake kwa kuwatambua katika kila mtaa, kitongoji, kijiji, kata na jimbo kupitia mfumo mpya wa kadi za eleketroniki ifikapo Januari 2017,” alisema Mbowe.

Alisema katika baadhi ya maeneo ya mikoa hapa nchini, kadi za uanachama za Chadema ni lulu na zimekuwa zikiuzwa hadi Sh5,000 badala ya 500.

Alieleza kuwa mapato ya chama lazima yatokane na ada za wanachama na siyo ruzuku ya Serikali, kwa kuwa utegemezi wa ruzuku ni hatari kwa uhai wake.

“Hii ruzuku inayotolewa na Serikali inatolewa kwa sababu ya CCM na CCM bila ruzuku hakiwezi kujiendesha,” alidai.

Mbowe alisema kila jimbo linapata fedha za ruzuku kulingana na idadi ya kura ilizopata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, akitolea mfano Jimbo la Mlimba kuwa Mbunge Suzan Kiwanga alishinda kwa kura 40,000 wakati urais Chadema ilipata kura 38,000 huku katika udiwani wakipata kata tisa kati 16.

“Kutokana na ruzuku, Mlimba itapata Sh163,688 kila mwezi. Unaweza kuona fedha za ruzuku kutoka ndani ya chama ni ndogo sana ambapo Mkoa wa Morogoro unapokea kiasi cha Sh2.2 milioni kila mwezi.

“Kufikia mwaka 2017 kupitia programu ya Chadema msingi, tumekusudia kukijikita zaidi kusaka wanachama kutoka ngazi ya mitaa, vitongoji na balozi na tutaanza uchaguzi ndani ya chama.

“Tumebaini kuwa baadhi ya maeneo Chadema tumeshindwa kupata wenyeviti wa Serikali ya vitongoji na vijiji, kukosa madiwani na wabunge kutokana na kukosa misingi imara wa wanachama,” alisema Mbowe.