HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

WAZIRI MWAKYEMBE AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI NAHODHA WA SERENGETI BOYS

VIDEO – MBUNGE WA VITI MAALUM MKOANI RUVUMA, AZUNGUMZIA MAMBO MANNE ANAYOPAMBANA NAYO

Dakika mbili za Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma kupitia chama cha mapinduzi (CCM ) Mhe. Sikudhani Chikambo, akizungumzia mambo manne anayopambana nayo katika mkoa wa Ruvuma.

PROF TIBAIJUKA AONYA UPOTOSHAJI WA MITANDAONI NA KUTOA UFAFANUZI KUHUSU MCHANGO WAKE BUNGENI

Tazama nyimbo mpya ya Snura ft Yamoto band "Nionee wivu"

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI SUALA LA VYETI FEKI

VIDEO – WAZAZI WALAZIMISHWA KUCHIMBA KABULI, WANANCHI WAKATAA KUZIKA MWILI WA MAREHEMU.

Wakazi wa mtaa wa NAMANYINGU kata ya MSHANGANO Manispaa ya Songea Mkoani RUVUMA, wamewalazimisha mume na mke kuchimba kabuli la mtoto wao aitwaye DANROAD MAHUNDI mwenye umri wa miaka 36 ambaye inasemekana wazazi wake wamemua kwa njia za kishirikina.

VIDEO: Ajira ya uoshaji magari yamtakatisha Dar

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


The Beauty TV katika pitapita yake mjini Posta ilikutana na kijana muosha magari Khumudi Juma almaarufu kama Muddy wa Muzungu na kuzungumza nae juu ya ajira yake hiyo inayomfanya aheshimike mjini, mtazame kupitia Youtube ya The Beauty TV na usisahau ku-subscribe kwa ajili ya kupata updates zaidi.

TAZAMA HAPA HOTUBA YA MWISHO YA RAIS BARACK OBAMA ILIYOMTOA MACHOZI



Rais Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa kama rais wa Marekani, huko Chicago hotuba ambayo ilijaa hisia kali na kupelekea kutokwa na machozi yeye pamoja na baadhi ya watu.

Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, kwenye hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.
"Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka, amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mjini humo.
Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani".

Amewaomba Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba "lazima tuwategee sikio wengine na kusikia".
Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza mabadiliko.


Mrithi wake Donald Trump ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama, 55.
Michelle Obama akimliwaza binti yake Milia ambaye alijikuta akitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba ya baba yake Rais Barack Obama
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye alijikuta akishindwa kujizuia na kutokwa na machozi
 Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden baada ya kumaliza hotuba yake.
Michelle Obama akimkumbatia mumewe rais Barack Obama baada ya kumaliza hotuba yake. 
Rais wa Marekani Barack Obama akimkumbatia binti yake Milia baada ya kumaliza hotuba yake.