HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA BAGAMOYO-- MSATA KM 64 PIA AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MATUNDA CHA SAYONA CHALINZE MKOANI PWANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa Kiserikali na Wabunge, akivuta kitambaa kuashiria jiwe la ufunguzi wa  Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya barabara ya Bagamoyo-Makofia –Msata kama inavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Pwani na Dar es Salaam mara baada ya kufungua barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Mama Salama Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akielezea hatua za ujenzi wa Madaraja katika barabara ya Bagamoyo-Msata huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha Viuadudu cha Kibaha mkoani Pwani.
Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akisalimia kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akizungumza kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigala wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi wa barabara hiyo ya Bagamoyo-Msata.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha Matunda cha Sayona Fruits kilichopo Mboga Chalinze mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda hicho cha Matunda cha Sayona Fruits kilichopo Mboga Chalinze mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kiwangwa  wakati akielekea kufungua barabara ya bagamoyo-Msata mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

TPA WASAINI MKATABA WA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa akiongea na wadau wa sekta ya usafirishaji kabla ya zoezi la utiaji saini wa mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Bw. Mkinga Mkinga. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa (katikati) akishuhudia makabidhiano ya mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mtedaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. XU XINPEI. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi Deusdedit Kakoko kulia na Mtedaji Mkuu wa Kampuni ya China Harbour Engineering Bw. XU XINPEI wakionyesha mkataba wa makubaliano ya upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kwa wadau wa sekta ya usafirishaji baada zoezi la utiaji saini wa mkataba huo kukamilika. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).

Benjamin Sawe, Maelezo
Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imesaini mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha bandari utakaowezesha bandari ya Dar es Salaam kupokea meli kubwa za mizigo na kushindana na bandari nyingine katika pwani ya bahari ya hindi.
Upanuzi huo  utakaofanywa na kampuni ya China Harbor Construction  ya China utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 336 na utadumu kwa miezi 36, ambapo  utahusisha uongezaji wa kina cha lango la bandari na uongezaji wa kina cha maji kati ya gati namba 0, 1 hadi 7.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hatua hiyo inalenga kuifufua upya bandari ya Dar es Salaam ili ifanye kazi kwa ushindani na kuhudumia wateja wengi kuliko ilivyo sasa. 
“ Kukamilika kwa upanuzi na uongezaji wa kina cha maji  katika gati namba 1 hadi 7 kutoka mita 8 hadi 15 kutawezesha meli kubwa na za kisasa zenye uwezo wa kubeba hadi makontena  elfu kumi na tisa kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi na kukuza uchumi wa Tanzania”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ya reli na barabara ili kuhakikisha mizigo haikai muda mrefu bandarini.
“Ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge toka Dare s Salaam hadi Kanda ya Ziwa na Kigoma na ufufuaji wa reli ya Tazara kutawezesha bandari ya Dar e s Salaam kufanya kazi kwa ufanisi na kuvutia wafanyabiashara wengi hivyo nawataka  wafanyakazi wote wa bandari kufanyakazi kwa bidii na uadilifu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko amesema kiasi cha dola za Marekani milioni 421, kitapatikana kwaajili ya ujenzi huo ambapo kati ya fedha hizo  Benki ya Dunia itatoa mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 345.
Kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa adha ya baadhi ya meli kusubiri kwa muda mrefu kupata nafasi ya kutia nanga na kutaongeza hadhi ya bandari ya Dar es salaam na kuvutia wasafirishaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

Waziri Nchemba Ataja Sababu Zinazowafanya CHADEMA Wapigwe Marufuku Kufanya Sherehe Vyuoni

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alihoji bungeni sababu za wanafunzi wa CCM kupendelewa kufanya mikutano na sherehe za kumaliza masomo yao huku wanafunzi wa vyama vingine vya upinzani hasa CHADEMA kupigwa marufuku kufanya sherehe hizo.

Akijibu jambo hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema kuwa wanafunzi wa Chama Cha Mapinduzi huwa wanafuata utaratibu ndiyo maana huwa wanapewa ruksa kufanya sherehe hizo pindi wanapomaliza vyuo na kusema hao wengine huwa hawafuati utaratibu ndiyo maana wanakuwa wanazuiliwa.

"Taratibu ziko wazi kama CCM walikuwa wamefuata utaratibu na kupewa mikutano, chama kingine chochote kinachotakiwa ni kufuata utaratibu zile zile waweze kupewa mikutano lakini wengine kama hawajafanya utaratibu hawatapewa tu kwa sababu CCM walipewa bali watapewa kwa kufuata utaratibu, kuna sehemu zingine CHASO hao hao wamepewa mikutano kwa hiyo linalotakiwa ni utaratibu tu wa kupewa mikutano hiyo" alisema Mwigulu Nchemba

Mbali na hilo Waziri Mwigulu Nchemba alisema mikutano ya hadhara haijazuiwa bali imewekewa utaratibu na kusema duniani kote sifa za mikutano ya hadhara ni kama ambavyo inafanyika hivi sasa Tanzania na kusema kuwa mtu aliyeshinda ndiye anaendelea na majukumu ya kuongoza na aliyeshindwa hapaswi kushukuru kwa wananchi.

"Marekani mwaka jana walifanya uchaguzi mmemuona Hillary Clinton anashukuru kwa wananchi? Duniani kote aliyeshinda ndiye anaendesha serikali kwa utaratibu wa kiserikali hili liko wazi duniani kote" alisisitiza Mwigulu Nchemba

YALITOJIRI LEO BUNGENI WAKATI WA UWASILISHWAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/2018

Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwaonyesha waandishi wa Habari mkoba wenye hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.
 Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18.
 Wabunge wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 Baadhi ya wageni wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 .Wabunge wakiingia Ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.

Picha zote na MAELEZO, DODOMA.

WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA WAHITIMU CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA HOMBOLO WAPEWE KIPAUMBELE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanachuo Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Hombolo), Bw. Kelvin Mbuta hivi karibuni mjini Dodoma. Pembeni ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Martin Madale.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene akizungumza na Uongoza na Wawakilishi wa Serikali ya Wanachuo ya Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Hombolo)mjini Dodoma hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
 SERIKALI imeziagiza Halmashauri,Miji na Majiji nchini kutoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu wa chuo  Kiongozi cha Mafunzo ya  Serikali za Mitaa(LGTI) ambao mafunzo wanayopata  yanalenga kuongeza  na  kuleta ufanisi katika serikali za mitaa nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema hivi karibuni kuwa  Chuo  Kiongozi cha  Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Hombolo) kipo mahusiusi kwa ajiri ya kutoa mafunzo  kwa ajili ya wafanyakazi  wanaoajiliwa kwenye serikali za mitaaa nchini.

“Naagiza kunapokuwa na nafasi za kazi kwenye halmashauri, miji na hata majiji ni vyema wahitimu wa chuo hiki wakapewa kipaumbele. Ni vizuri wakapata nafasi ya kushindanishwa na wengine kwani hawa ni walengwa,”  alisema Waziri Simbachawene  wakati alipokutana na viongozi na wawakilishi wa chuo hicho mjini Dodoma.

Bila kumung’unya maneno, Waziri Simbachawene alisema wahitimu kutoka chuo Kiongozi cha Serikali za Mitaa ndiyo wabobezi kwenye taaluma za serikali za mitaa na hivyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuleta ufanisi zaidi.

“Ni vizuri tukakumbuka kuwa chuo hiki kilianzishwa na serikali kwa lengo la kuwaandaa wafanyakazi wa kada zote katika serikali za mitaaa,” alisema na kuongeza kuwa serikali itaendelea kukijengea uwezo chuo hicho ili kiweze kutoa wahitimu bora.

Waziri Simbachawene aliuagiza uongozi wa chuo hicho kutosita kutoa taarifa yeyeto endapo chuo kinapokuwa na upungufu wa watumishi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Martin Madale alimshukuru Waziri Simbachawene kwa kuwa karibu na chuo  na pia kufuatilia maendeleo na  ustawi.

“Kwa niaba ya Bodi, Menejimenti, Wafanyakazi na wanachuo wote wana imani kubwa na uongozi wako kwani umekuwa karibu sana nasi na pia umekuwa msaada mkubwa katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo,” alisema Dkt. Madale.

Alimwomba waziri kukisaidia chuo  kupata kompyuta zaidi, viti na vifaa mbalimbali ilikukabiliana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoomba kujiunga na chuo hicho kwa sasa.

Naye Rais wa Serikali ya wanachuo, Bw. Kelvin Mbuta alimwomba waziri kusaidia kufikisha ombi la wanachuo serikalini kuhusu mikopo kama wanachuo wa vyuo vingine wanavyopata.

“Nipo hapa kwa niaba ya wanachuo ambao wameniagiza kilio chao kuhusu mikopo. Tunakuomba Mheshimiwa waziri utusaidie tupate mikopo kwaajili ya kujikimu kwani kuna wachuo wengi wanetoka kwenye familia maskini sana,” alisema.

Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa maarufu kama Chuo cha Hombolo kina wanachuo zaidi ya 3,000 ambao wapo katika Kampasi Kuu ya Hombolo ambayo ipo pembeni kidogo mwa Mji  wa Dodoma na ile Kampasi ya Mjini.

Chuo kinatoa  programu  sita  za Stashahada (Diplomas)  na program sita za Cheti(Certificates) katika Usimamizi wa Raslimali Watu (Human Resource Management), Serikali za Mitaa na Utawala(Local Government and Administration)Uhasibu na Usimamizi wa Fedha Serikali za Mitaa(Local Government Accounting and Finance),Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka(Records and Archive Management),Manunuzi (Procurement)na Maendeleo ya Jamii (Community Development).

CDA Wadaiwa Kuficha Viwanja 34,000

Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amedai kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) wameficha zaidi ya viwanja 34,000.

Lukuvi ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa CDA kwa miaka kadhaa, pia amesimulia jinsi wabunge wanne walivyotapeliwa na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Hivi karibuni, Rais Dk. John Magufuli aliifuta mamlaka hiyo na shughuli zake kuhamishia Manispaa ya Dodoma.

Akizungumza mjini hapa jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST), Lukuvi alisema viwanja vilivyopimwa Manispaa ya Dodoma vilikuwa 60,000, lakini vilivyoonekana ni 26,000 tu huku 34,000 vikiwa vimefichwa na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi, Serikali imegundua wafanyakazi wengi wameiba viwanja na kuviuza kwa watu wengine.

Lukuvi alisema kulikuwa na utaratibu wa wafanyakazi wa CDA kuuza viwanja kwa njia za panya kwa Sh milioni 5, kisha mhusika kupelekewa nyaraka mahali alipo.

Alisema kuna wabunge wanne waliuziwa viwanja kwa kutoa Sh milioni 5, lakini kesho yake rais akaivunja mamlaka hiyo na kujikuta wakitapeliwa.

Lukuvi alisema wabunge hao walikwenda kumlilia wakitaka kurudishiwa fedha hizo, lakini jambo la kushangaza hawakuwa na ‘invoice’ ya aina yoyote.

“Sasa wapo watu ambao wamewalipa hizo milioni tano, halafu kesho yake ikala kwao, Mheshimiwa Rais kaifuta CDA, ndiyo wanakuja kusema kwangu, watalipwaje? Nimewaambia nipeni risiti wanasema hawana. Nitawapa kitu gani? Majina ninayo,” alisema.

Alisema wale wote walioiba viwanja hivyo vitawatokea puani, kwani Serikali tayari inayo ripoti nzima juu ya wizi huo.

 “Serikali inakosa mapato, sasa tunataka viwanja vipimwe vingi ili tuweze kujiingizia mapato,” alisema.

Aidha Lukuvi alimbana aliyekuwa Mpimaji Mkuu wa CDA, Frank Mkomochi ambaye alikuwapo katika mkutano huo, akidai kuwa ni mmoja ya watu waliohuka kusimamia uuzwaji wa viwanja maeneo mengi.

“Viwanja Itega vilikuwa vinauzwa milioni tano, sasa vinauzwa milioni 25, hili hujalisikia wewe mtu wa CDA?” alimuhoji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa IST, Martin Chodota, aliomba Serikali kutoa kipaumbele kwa kampuni za wazawa na kuacha kuwapa nafasi zaidi wapimaji wanaotoka nje.

Timu ya Azania kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Standard Chartered Uingereza

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameikabidhi bendera timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield.


Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria, Waziri Mwakyembe alisema ni fursa ya kipekee ambayo Tanzania imeipata kushiriki mashindano kama hayo na ni muda sasa dunia kujua kuwa Tanzania kuna vipaji vya soka hivyo wahakikishe wanarudi nchini na kikombe.

“Mtuwakilishe vyema huko muendako ni muda sasa wa dunia kuwa Tanzania tuna uwezo wa kisoka, kila mmoja acheze vizuri na kuonyesha uwezo wake, tunaamini mtarudi na kikombe na nawatakia kila la kheri,” alisema Waziri Mwakyembe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria kwa timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar Es Salaam.



Nae Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe amesema benki yao inajivunia kupata wawaklishi kutoka Tanzania na wamesimamia gharama zote za safari kwa muda wote ambao timu itakuwa Uingereza na ni matumaini yao kuwa timu hiyo ya Azania itarejea nchini na kikombe.

“Tupo hapa kuiaga timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki wa kombe la Standard Chartered Safari kwenda Anfield, tunajivunia timu hii sababu imetuletea heshima kubwa, tunawaombe ushindi mkubwa na tunategemea watakuja na ubingwa,” alisema Mpungwe.

Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akitoa pongezi kwa timu ya Azania kupata nafasi ya kwenda Uingereza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo inayokwea pipa kesho 18 Mei. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.


Kwa upande wa Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke aliipongeza timu ya Azania kwa kupata nafasi ya kwenda Uingereza kucheza kwenye moja ya kiwanja maarufu cha Anfield lakini pia kuipongeza benki ya Standard Chartered kwa kufikisha miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma nchini.

“Hii ndiyo nguvu ya michezo inauwezo wa kuwaunganisha watu pamoja, mnakwenda Uingereza tunaijua ni timu kubwa nawapongeza Azania kwa kupata nafasi, hongereni sana nawatakia kila la kheri najua mtafurahi kwa kipindi ambacho mtakuwa kule,

“Mnakwenda kwenye moja ya uwanja maarufu nchini Uingereza, Liverpool ni timu yenye historia na wachezaji wakubwa kama Steven Gerarld, Kenny Dalglish na wengine wengi, pia niwapongeze Standard Chartered kwa kufikisha miaka 100 tangu kuanza kufanya kazi Tanzania,” alisema Cooke.


Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said akizungumzia safari ya timu ya Azania katika hafla ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo inayokwea pipa kesho 18 Mei kuelekea nchini Uingereza.


Nae nahodha wa timu hiyo, Khalid Sultan Said aliahidi kuwa timu hiyo inajiamini kuwa inauwepo wa kupambana na timu zingine na kuahidi kuwa itahakikisha kikombe kinakuja nchini.

Timu hiyo itaondoka nchini Mei, 18 watafika Mei, 19 wakiwa huko watakutana na timu zingine, Mei, 20 watatembelea uwanja wa Anfield, Mei, 21 watashuhudia mchezo wa Liverpool na Middlesbrough na baada ya hapo wataingia uwanjani kwa ajili ya mashindano na watarejea nchini Mei, 22.
Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe (kushoto) akizungumzia wakati wa halfa ya kukabidhi bendera timu ya Azania inayotarajia kukwea pipa kesho Mei 18 kuelekea nchini Uingereza. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiwa bendera kuelekea nchini Uingereza kesho Mei 18.
Kikosi cha Timu ya Azania katika hafla ya kukabidhiwa bendera kuelekea nchini Uingereza kesho Mei 18.
Picha juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiabidhi hati za kusafiria kwa wachezaji wa timu ya Azania wanaotarajia kukwea pipa kesho Mei 18 kuelekea nchini Uingereza.Katikati ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.
Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akikabidhi hati ya kusafiria kwa mwandishi wa TV1 atakayeambatana na msafara wa timu hiyo kuelekea nchini Uingereza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akikabidhi rasmi bendera kwa Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe (suti nyeusi) na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi jezi Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said wakati wa hafla ya kukabidhi bendera timu hiyo. Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe.

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA 2017/2018


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kushoto ni Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na makamanda wa Jeshi la Polisi muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge la Bajeti ambapo wizara yake iliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akifurahia na baadhi ya wabunge mara baada ya kumaliza kuwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Dkt Mwakyembe - Asimia 90 ya watangazaji si wanataaluma

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harisson Mwakyembe amesema, asilimia 90 ya watangazaji wamebainika kutokuwa na sifa za kitaalamu za uandishi wa habari na utangazaji.

Hayo yamezungumzwa na Waziri Mwakyembe wakati akitoa taarifa hiyo bungeni alipokuwa anawasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ya Shilingi bilioni 28.2.
“Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kusimamia ubora wa huduma za utangazaji kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye vituo vya utangazaji kwa lengo la kuhakiki vitendea kazi na ubora wa huduma zinazotolewa na vituo hivyo,” alisema Mwakyembe.
“Maeneo yaliyohakikiwa ni pamoja na studio, vyumba vya kuandaa habari, maktaba, utaratibu wa ndani wa kuandaa na kutangaza vipindi, sifa za watangazaji na waandishi wa habari na mikataba ya ajira.
“Vituo vyote vilivyokaguliwa vilionyesha ubora katika kutoa huduma kwa wasikilizaji wake katika maeneo husika, ikiwa ni pamoja na ubora wa usikivu ambao hauna miingiliano ya sauti, ubora wa vitendea kazi katika vituo, uelewa wa taratibu na sheria za utangazaji pamoja na uwezo wa kituo katika kutimiza haki na maslahi ya wafanyakazi wake.
“Lakini katika ukaguzi huo, asilimia 90 ya wafanyakazi walibainika hawana sifa stahiki katika taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji, jambo linaloifanya iendelee kuwa changamoto kubwa katika tasnia ya habari na utangazaji nchini,” alisema Dk. Mwakyembe.

WAZIRI MAHIGA AFUNGUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA 69 YA UHURU WA ISRAELI, DODOMA.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 69 ya uhuru wa Taifa la Israel iliyofanyika kwenye Hoteli Morena Mjini Dodoma 
Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo ya Taifa unakipigwa kweye maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel 
Balozi wa Israeli nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Yahel Vilan akizunguza kwenye hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel iliyofanyika mjini Dodoma 
Mhe. Balozi Vilan akisisitiza jambo 
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akihutubia hadhira iliyo shiriki hafla hiyo 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani (Mwinyi kulia) akifuatilia jambo, kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima 
Picha ya pamoja 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga jana alifungua hafla ya maadhimisho ya 69ya uhuru wa Taifa la Israeli yaliyo fanyika mjini Dodoma katika Hoteli ya Morena.

Hafla hiyo ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Taifa hilo na uhusiono mzuri wa kidiplomasia  baina ya Tanzania na Israeli yaliratibiwa na Ubalozi wa Israel wenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya.  Waziri Mahiga akizungumza katika hafla hiyo aliupongeza Ubalozi wa Israel kwa uamuzi wake wa kufanyia hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wao, Makao Mkuu ya Serikali mjini Dodoma.

 Waziri Mahiga aliongeza kusema Mataifa haya mawili Tanzania na Israel yana mahusiano mazuri ya kidiplomasia, ikidhihirishwa wazi na idadi kubwa ya raia wa nchi hizi mbili kutembeleana na kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo utalii. Aidha Mahiga aliipongeza Serikali ya Israel kwa hatua kubwa ya maendeleo waliyofikia katika maeneo mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia na kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali.  

Balozi wa Israeli nchini Mhe. Yahel Vilan mwenye makazi yake Jijini Nairobi, Kenya akitoa hotuba yake alisema Ubalozi wa Israeli umechukua maamuzi ya kufanyia hafla hiyo Mjini Dodoma ikiwa nikuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma. Aliongeza kusema kuwa hafla hiyo ni ishara ya Israel kuanziasha Ubalozi wake nchini Tanzania. 

Balozi Vilan ameihakikishia serikali ya Tanzania kuwa Israel itaendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Taifa katika maeneo ya kilimo, afya, elimu, sayansi na teknolojia na usalama.Israeli ilifungua kituo cha kushughulikia masuala ya viza nchini Tanzania tarehe 3 Novemba, 2016.