Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz.
Lowassa akizungumza na Mwananchi leo (Jumatatu), amesema ameitwa kwa DCI lakini hajui anachoitiwa.
Hata hivyo, amesema anahisi ni kauli yake kuhusu mashehe wa kikundi cha Uamsho cha Zanzibar wanaoshtakiwa kwa tuhuma ya ugaidi.
“Ni kweli nimetakiwa niripoti kesho saa 4:00 asubuhi katika ofisi ya DCI. Sijui wananiitia nini, lakini nahisi ni kuhusu nilichosema kuhusu mashehe wa Uamsho,” amesema Lowassa.
Jana katika taarifa kwa vyombo vya habari, Lowassa alikaririwa akimtaka Rais John Magufuli kuwaachia huru mashehe hao wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Taarifa hiyo ilisema Lowassa alitoa ombi hilo alipozungumza katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara.
Sumaye ajiuzulu ujumbe wa bodi CRDB
By: VIJIMAMBO on May 21, 2017 / comment : 0 CHADEMA, Frederick Sumaye, Habari, Waziri Mkuu Mstaafu
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amejitoa katika Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB kwa madai kuwa familia yake inafuatwafuatwa hivyo kuhofia kuwa anaweza kuathiri benki hiyo.
Baada ya kujitoa kama mmoja wa viongozi wa benki hiyo kubwa nchini, Sumaye amesema kuwa ataendelea kuwa mwanahisa wa benki hiyo ya biashara.
“Sitaki msimamo wangu wa kisiasa uhusishwe na benki yetu” alisema Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.
Sumaye alisema kuwa huenda majukumu yake ya kisiasa yakambana na akashindwa kuhudhuria baadhi ya vikao muhimu vya benki hiyo ambavyo ni muhimu kwa ufanisi na ustawi wa benki.
Akiwa nje ya mkutano huo Sumaye alisema kuwa, familia yake imekuwa ikifuatwafuatwa na serikali na kwamba tayari mtoto wake amepokwa shamba.
Serikali pia alimnyang’anya Sumaye shamba lake lililokuwa Mabwepande kwa madai hakuliendeleza, huku yeye akisema uamuzi wa yeye kupokwa shamba ulikuwa ni wa kisiasa. Sumaye alieleza kwamba hakuweza kulima shamba hilo kutokana na serikali kupiga kilimo jijini Dar es Salaam.
Sumaye amesema uamuzi wake aliuchukua ili CRDB iweze kuendeshwa na watu walioko huru mbele ya jamii kuepusha hisa za wafanyabishara wengine kuathiriwa.
Sumaye anamiliki zaidi ya hisa milioni 7.4 za benki hiyo.
SUMAYE AIFUNDA SERIKALI KUHUSU DEMOKRASIA
By: VIJIMAMBO on March 22, 2017 / comment : 0 Frederick Sumaye, Habari, Waziri Mkuu Mstaafu
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani Mhe. Frederick Sumaye ameiomba serikali kusimamia misingi ya demokrasia katika kutatua malalamiko ya wananchi na kusimamia ustawi wa jamii ya Watanzania.
Mhe. Sumaye ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kama serikali itafanyia kazi malalamiko na mapendekezo yanayotolewa na wananchi ni wazi taifa litafikia malengo yake iliyojiwekea ya kupunguza hali ya umasikini na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo Mhe. Sumaye amewaasa watendaji wa serikali kutumia vizuri misaada inayotolewa na nchi wahisani ili kuhakikisha fedha za wananchi zinazotumiwa katika ulipaji wa madeni hayo zinakuwa na manufaa kwa watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kijamii.
Credit:EATV
LOWASSA: WALIOFUKUZWA CCM KARIBUNI CHADEMA
By: VIJIMAMBO on March 13, 2017 / comment : 0 CCM, CHADEMA, Habari, Lowassa, Siasa, Waziri Mkuu Mstaafu
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa amesema anawakaribisha Chadema waliofukuzwa uanachama baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitisha uamuzi wa kuwatimua 12 kati ya 24 walioadhibiwa.
Amesema walioadhibiwa ni mashujaa waliosimama kutetea demokrasia.
Lowassa yuko katikati ya tuhuma zilizosababisha wanachama wengi wa CCM kuchukuliwa hatua baada ya uamuzi wake wa kuhamia Chadema kupinga kuenguliwa kugombea urais, kufuatiwa na viongozi kadhaa na wanachama kujiondoa chama tawala na kujiunga na upinzani.
Katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari jana, Lowassa ambaye pia alikuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM hadi mwaka 2015, amesema viongozi waliotimuliwa na chama hicho tawala walitumia demokrasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria.
“Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki, demokrasia na taratibu na kupinga dhuluma ndani ya chama chao na nchini,” amesema Lowassa, ambaye kabla ya kuenguliwa alikuwa mmoja wa makada waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupitishwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM.
MAKAMU AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA GUINEA CONAKRY
By: VIJIMAMBO on February 23, 2017 / comment : 0 Makamu wa Rais, Matukio, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mstaafu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Conakry Mhe. Kabine Komara ambaye sasa ni Balozi wa Taasisi ya Maendeleo ya Bonde la Mto Senegal, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Conakry Mhe. Kabine Komara ambaye sasa ni Balozi wa Taasisi ya Maendeleo ya Bonde la Mto Senegal, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Conakry Mhe. Kabine Komara ambaye sasa ni Balozi wa Taasisi ya Maendeleo ya Bonde la Mto Senegal, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA NYUMBANI KWAKE UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM
By: VIJIMAMBO on February 18, 2017 / comment : 0 Magufuli, Matukio, Rais, Waziri Mkuu Mstaafu
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo
na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea
nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwake
Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga
jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake Upanga kwa ajili ya kumjulia hali.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga
jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MWAKA MPYA KATIKA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA MONDULI ARUSHA
By: VIJIMAMBO on January 01, 2017 / comment : 0 CHADEMA, Dini, Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa KamatiKuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017 ambapo amewataka watanzania wote bila kujali itikadi zao kufanya kazi kwa bidii.
Mh Lowassa ameshiriki ibada hiyo akiambatana na familia yake pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali Mkoani Arusha na Jimbo la Monduli wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mh Isack Joseph , Wakili John Mallya na viongozi wengine.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa, mama Regina Lowassa akisalimiana na mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha Laison Saning'o katika Ibada maalamu ya mwaka mpya 2017.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akisalimiana na mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha Laison Saning'o katika Ibada maalamu ya mwaka mpya 2017.
Wakili John Mallya (aliyeshika biblia) akisoma neno kwenye biblia katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017
Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha leo.
Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha leo.
MAJALIWA AITEMBELEA FAMILIA YA MAREHEMU SOKOINE MONDULI JUU
By: VIJIMAMBO on December 04, 2016 / comment : 0 Kassim Majaliwa, Matukio, Msiba, Sokoine, waziri mkuu, Waziri Mkuu Mstaafu
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Napono Sokoine (wapili kulia) na Nekiteto Sokoine (kulia) ambao ni wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Sokoine wakati aipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli leo Desemba 4, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli Juu akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli leo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa aktika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 20, 16. Kushoto kwake wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni Nekiteto Sokoine . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa aktika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 20, 16. Kushoto kwake wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni Nekiteto Sokoine . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Serikali imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kuharakisha maboresho ya mitaala na mafunzo ya Uhasibu ili...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Huma...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014
























