HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Kauli ya Jerry Muro baada ya Haji Manara wa Simba kufungiwa na TFF

Muda mfupi baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya nidhamu ya TFF kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na makosa matatu.
Afisa habari wa zamani wa Yanga ambaye nae alifungiwa mwaka mmoja Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika “Mtuache sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara“

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka pamoja na faini ya Tsh Milioni 9.

Kamati ya nidhamu ya TFF imetoa adhabu hiyo licha ya Haji Manara kushindwa kufika kwa madai ya kupata dharura lakini anayo nafasi ya kukata rufaa.

YANGA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS BAO 3-0 KOMBE LA SHIRIKISHO ASFC

 Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiruka juu sambamba na kipa wa Tanzania Prisons, Andrew Ntala katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda 3-0.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Amis Tambwe.
 Wachezaji wa Tanzania Prisons wakiomba dua kabla ya mchezo.
Godfrey Taita akichuana na mchezaji wa Yanga.
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, akimtoka kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-0. (Picha na Francis Dande).

Yanga waachwa na ndege Algeria

Yanga imepata pigo lingine nchini Algeria baada ya wachezaji wake kuchelewa ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene, jijini Algers.

Wachezaji hao walikuwa wasafiri na ndege ya Uturuki kupitia Istanbul  wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa walichelewa kufika uwanjani hapo.

Wakati benchi la ufundi na wachezaji wachecha wakiondoka leo, wachezaji waliochwa na ndege wanategemea kuondoka Algeria kesho au keshokutwa.

Yanga imeondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa mabao 4-0 na MC Algers katika mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Algeria.

Simba Yaitandika Mabao 2 Yanga Uwanja wa Taifa Leo

Mashabiki wa soka wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo kushuhudia pambano la Simba na Yanga. Simba imeshinda 2-1. (Picha na Francis Dande).
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kulia), akishangilia bao la kufutia machozi alililoifungia timu yake dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzia Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Haruna Niyonzima. Simba ilishinda 2-1. 
Askari wakiwa katika doria uwanja wa Taifa.

 Mashabiki wa Simba.
 Mashabiki wa Simba.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisalimiana na Simon Msuva.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akisalimiana na Simon Msuva.

 Mashabiki wa Simba.
 Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akimtoka beki wa Simba, Novat Lufunga.
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akimtoka beki wa Simba, Novat Lufunga.
 Mashabiki wa Simba.
Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Laudit Mavugo (11), akiwa amembeba Said Ndemla.


Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, akimtoka beki wa Simba, Novat Lufunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 2-1. 
Shabiki wa Yanga akipata huduma ya kwanza baada ya kupoteza fahamu.
Beki wa Simba, Janvier Bukungu akitoa uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu.
Klabu ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika za mwanzo kabisa na kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7 mgongoni kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat Lufunga na kupelekea Yanga kupata penati ndani ya ya dakika 4 za mchezo na kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga.

Yanga iliendelea kuongoza kwa bao hilo la kwanza huku wakiwa na moto wa kutafuta goli la pili, katika dakika ya 23 Yanga walipata kona ya kwanza ambayo ilipigwa na mchezaji Haruna Niyonzima lakini kipa wa Simba aliweza kuicheza vyema na kuondoa hatari ya Yanga kupata goli la pili ndani ya dakika za mwanzo mwanzo.

Kocha wa Simba Omug alipoona kikosi chake hakina mwenendo mzuri ndani ya dakika 27 alimtoa Luizio na kumuingiza Said Ndemla ambapo hapo kidogo mchezo kwa upande wa Simba ulibadilika na kuanza kufanya mashambulizi, huku wakijaribu

Ndani ya dakika 32 Goli kipa wa Yanga Deogratius Munishi alidaka mpira na kukaa nao kwa muda na kupeleka faulo ambayo ilipigwa na Said Ndemla wa Simba lakini Ndemla alikosa na kupoteza nafasi ya kusawazisha goli la kwanza.

Yanga iliendelea kufanya vyema na kujaribu mara kadhaa katika lango la Simba bila mafanikio, ndani ya dakika 43 Simba ilibahatika kupata faulo nyingine tena ambayo ilipigwa na mchezaji Ajib lakini mpira huo ulikwenda nje.

Mchezo uliendelea kwa kasi na mashambulio kwa timu zote mbili, na ilipofika dakika ya 47 mchezaji wa Yanga Thabani Kamusoko alitoka nje baada ya kupata majeraha na kuingia Said Juma Makapu.

Mpaka muda wa mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao moja dhidi ya Simba huku ikiwa imetawala mchezo kwa asilimia 51 na Simba ikitawala mchezo kwa asilimia 41.

Baada ya kurudi kwa kipindi cha pili timu zote mbili zilikuwa na hamasa ya mchezo na ushindi hamasa hizo zilipelekea mchezaji wa Yanga, Endrew Vicenti alipata kadi ya njano ndani ya dakika 56 mchezaji wa Simba alipigwa kadi nyekundu na kutoka nje ya uwanja na kuwaacha Simba wakiwa pungufu uwanjani.

Katika kipindi cha pili baada ya kuingia mchezaji Kichuya Simba ilibadilika na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kuonyesha uwezo katika kucheza mpira jambo lililopelekea mchezaji Mavugo wa Simba ndani ya dakika 66 kupata goli la kwanza kwa Simba na kuweza kusawazisha na kuwa bao moja kwa moja.

Mpka dakika ya themanini ya mchezo Simba kupitia kwa mchezaji wake Shiza Ramadhan Kichuya aliiandikia Simba goli la pili dhidi ya Yanga huku timu hiyo ikiwa pungufu uwanjani.

Mpaka mpira umekwisha Simba 2-1 Yanga (Mavugo 66, Kichuya 81 : Msuva 5)

PICHA: VIONGOZI MBALIMBALI WA KISIASA WASHUHUDIA MECHI YA SIMBA NA YANGA

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.(Picha na Francis Dande)
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 
Freeman Mbowe akiwapungia mashabiki wa soka. 
Mbowe.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto), akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.  
 Lowassa akishuhudia pambano la Simba na Yanga. 
 Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya akizungumza na Edward Lowassa.
 Viongozi wakiwa wamesimama kuamboleza kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Yanga na timu ya taifa, Godfrey Bonny.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, akiwasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 

LWANDAMINA AIPIGA MKWARA SIMBA

JOTO la pambano la watani wa jadi linazidi kuongezeka baada ya wachezaji na uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kuahidi watacheza kwa kiwango cha juu kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mechi dhidi ya Simba.

Mechi hiyo itakayofanyika kesho kutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyofanyika Oktoba Mosi mwaka jana, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, Shiza Kichuya akiisawazishia Simba katika dakika ya 87.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, alisema kuwa kikosi chake kimeiva na wanachosubiri ni kutekeleza maelekezo waliyowapa ya kusaka pointi tatu muhimu.

Lwandamina ambaye mechi yake dhidi ya Simba kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi alikubali kichapo, alisema kuwa anataka kuona wanaibuka na ushindi ili safari yake ya kutwaa ubingwa na Yanga kuweka rekodi ya kushinda taji la Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo wanalitimiza.

"Ni mechi kubwa na muhimu kwa kila upande, ila Yanga tutaingia uwanjani tukifahamu tunachokwenda kukifanya, ushindi ndiyo jambo tunalolitarajia, tunataka pointi tatu muhimu," nahodha msaidizi wa Yanga na kiungo wa kimataifa kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima alisema jana.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Salum Mkemi, alisema kila mchezaji amejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo huo na kuhakikisha timu yake inaondoka na ushindi mnono ili kulinda heshima yao, viongozi, wanachama pamoja na timu yao.

“Tutaifunga Simba magoli mengi sana, na mwaka huu ni lazima ishuke daraja kwa sababu tutawafunga magoli mengi kipindi cha kwanza, hivyo hawatarudi kipindi cha pili na kwa sheria za TFF ( Shirikisho la Soka Tanzania), timu isiporudi uwanjani inashushwa daraja,” alisema.

Kuhusu hali ya straika, Donald Ngoma, kuwa katika hatihati ya kutocheza mechi hiyo, kiongozi huyo alisema hawana wasiwasi wowote kwa sababu kikosi chao kina washambuliaji wengi wenye uwezo wa kuifunga Simba.

Aliongeza kuwa benchi la ufundi la Yanga linamuandaa mshambuliaji huyo kutoka Zimbabwe kwa ajili ya kuwavaa Zanaco katika mechi ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Machi 11 hapa jijini na marudiano wiki moja baadaye huko Lusaka, Zambia.

AFYA YA MANJI YAANZA KUIMALIKA

Taarifa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alikolazwa zinasema hawezi kuruhusiwa kwa sasa.
Msemaji wa JKCI, Anna Nkinda alisema jana kuwa baada ya vipimo, madaktari wameshauri aendelee na mapumziko mpaka watakapoona inafaa kumruhusu.
Mkurugenzi wa Tiba wa JKCI, Dk Peter Kisenge alisema mgonjwa huyo anahitaji vipimo zaidi hivyo ataendelea kubaki katika hospitali hiyo.
Wiki iliyopita, Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kumtaka kuripoti katika idara hiyo kwa madai kwamba kampuni yake imeajiri wageni 25 wasiokuwa na vibali halali vya kuishi nchini.
Katika mkutano huo Msumule alisema, “Tumekamata pasipoti 126, tumechambua pasipoti 25 hawana vibali vya kufanyia kazi, kwa hiyo wanafanya kazi kinyume na taratibu. Wote hawa hatua zitachukuliwa watapelekwa mahakamani.
“Lakini niseme ukweli, hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani, lazima Yusuf Manji ambaye ndiye mwajiri wa watu hawa, ambaye ndiye mmiliki wa kampuni hii lazima afikishwe mahakamani kujibu shtaka la kuajiri wageni wasio na vibali,” alisema.
“Jana ilikuwa tumkamate alale mahabusu na leo tumpeleke mahakamani, bahati mbaya wakati tunafanya zoezi la kwenda kumkamata tukapewa taarifa kwamba amelazwa hospitalini hadi sasa. Mara tu akitoka aripoti haraka ofisi hii ili tumuunganishe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali.”
Hata hivyo, katika tangazo lililotoka katika gazeti la The Citizen, Aprili 13, 2016, Manji aliutangazia umma kwamba atastaafu uongozi katika kundi la kampuni za Quality kuanzia Julai 15, 2016 na kubaki kuwa mwenyekiti na mshauri mkuu mwenye uamuzi wa mwisho katika Baraza la Uongozi na Ofisa Mtendaji Mkuu.
Pia, katika gazeti hili lilitolewa tangazo jingine Desemba 20, 2016 kumpongeza Arif Sheikh kuwa msimamizi wa ofisi za Quality Group katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Manji.
Tangazo hilo lilieleza kwamba Manji atakuwa akizunguka kusimamia kampuni za Quality Group zilizo katika nchi 28 akiendelea na cheo chake cha mwenyekiti na mshauri mkuu mwenye uamuzi wa mwisho katika Baraza la Uongozi na Ofisa Mtendaji Mkuu.
Tofauti na alipofikishwa hospitalini hapo kwa mara ya kwanza Februari 12 ambako kulikuwa na ulinzi mkali wa askari kanzu na waliokuwa wamevaa sare na hata Februari 16 baada kupata dhamana na kuwa chini ya maofisa wa Uhamaji, jana hapakuwa na ulinzi wowote.

HAWA NDIO WAAMUZI WATAKAO CHEZESHA MECHI YA YANGA NA NGAYA YA COMORO UWANJA WA TAIFA

Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.
Nsulumbi atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.