HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

ZITTO, WAITARA WALILIA FEDHA ZA BUNGE SERIKALINI

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT –Wazalendo), Zitto Kabwe amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, taasisi za uwajibikaji ikiwamo Bunge zinashindwa kufanya kazi kutokana na kutopewa fedha za kutosha. “Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) amenyimwa fedha. 
Hii inaonyesha kuwa Serikali haina dhamira ya kweli ya kuwezesha Bunge kufanya kazi yake kinyume kabisa na hotuba ya Rais John Magufuli wakati akifungua Bunge Novembea 2015,” amesema Zitto ambaye ni kiongozi wa chama hicho. 
Zitto alikuwa akizungumzia taarifa kwamba, chombo hicho cha kutunga sheria kimekumbwa na ukata, kiasi kwamba kina fedha za muda mfupi ujao. Mbuge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara ameunga mkono kauli ya mbunge wa Mtwara vijijini, Hawa Ghasia akisema shughuli za Bunge zimedorora.
 “Ni kweli kama alivyosema Ghasia kuwa Serikali imeshindwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo kwa wizara mbalimbali. Hata kwenye Bunge imeathiri utendaji,” amesema Waitara. “Kwa mfano katika kamati wabunge wanakwenda kwenye ziara, lakini hawalipwi posho. Wabunge wanakwenda kwenye ziara hawalipwi posho, mwisho kazi zinashindikana kufanyika. ‘Kamati za Bunge zilitakiwa kukaa kwa wiki tatu, lakini zimeishia kukaa wiki moja kwa sababu ya ukata.
 Wabunge wanashinda mchana kutwa bila kula. Tumemuuliza Spika akasema hakuna hela.” Juzi, Ghasia ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, alisema wakati ikiwasilisha maoni kuhusu bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kuwa kumeonekana changamoto kubwa ya Bunge kupewa fedha kwa wakati na hivyo kuathiri utekelezaji wa baadhi ya majukumu.

Chanzo: Mwananchi

Zitto Kabwe Agonga Mwamba Ubunge ELA, Spika Ndugai Agomea Maombi Yake

Mbunge  wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo),  amegonga mwamba baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kutoa msimamo wake kuhusu uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Hatua hiyo inatokana na Zitto kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Machi 28, mwaka huu akitaka kamati hiyo kutoa ufafanuzi wa mgombe wa kundi C ili kila chama kiweze kushiriki uchaguzi, badala ya kupewa kwa vyama vilivyokuwa na idadi kubwa ya wabunge.

Kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, Zitto, alisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na si uchaguzi.

Alisema pia mwongozo huo, mbali na kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotaka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo, lakini pia inavinyima vyama vingine vyenye uwakilishi bungeni haki ya kuchaguliwa.

Chanzo cha kuaminika kimeema  kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Kanuni, kilichokutana juzi mjini Dodoma chini ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, huku Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akihudhuria.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe pamoja na wajumbe kadhaa, ambapo baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho kilichomalizika usiku wa juzi, Spika Ndugai, alihoji uhalali wa Zitto kuandika barua ya kuhoji mgawanyo huo wa wabunge wa EALA.

“Kifupi ni kwamba Zitto amekwama na hana tena namna maana Spika alimsema sana kutokana na mgawanyo lakini kabla ya kuendelea zaidi kwamba alimuuliza Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Kabudi kama kuna tatizo naye akasema hakuna na Spika hajakosea.

“… ila ni kikao ambacho Spika kwa kweli amesimamia sheria na ni kiongozi asiyeyumba katika kusimamia sheria, sasa tunakwenda kwenye uchaguzi huku ukweli ukiwa umeshajulikana, CCM watakuwa na viti sita, Chadema viwili na CUF kimoja,” alisema mtoa habari huyo

Baaada ya majadiliano ya kina na ufafanuzi wa kisheria kuhusu mgawanyo huo wajumbe wa Kamati ya Kanuni walikubaliana na Spika Ndugai kwa kauli moja, huku hoja ya Zitto ikitupwa na uchaguzi huo wa EALA  utafanyika kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya wabunge wa vyama vyenye uwakilishi bungeni.

Hata hivyo kanuni ya 5(5) ya nyongeza ya tatu ya kanuni za Bunge inaeleza “Chama  chochote cha siasa chenye haki ya kusimamisha mgombea wa EALA kinaweza kuweka wagombea watatu katika  ya wagombea ubunge”.

Kutokana na hilo msingi huo wa kikanuni inaonesha kuwa vyama vingine tofauti na Chadema , CUF na CCM, haviwezi kusimamisha wagombea kwa sababu havikidhi kigezo cha kanuni ya 12 za Kudumu za Bunge.

Zitto Kabwe, CHADEMA Watofautiana Tena

Ikiwa ni takribani miaka mitano tangu Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, avurugane na Chadema ambacho kilikuwa chama chake, sasa hali hiyo inaonekana kurudi tena kupitia uchaguzi wa ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

Tofauti na awali ambapo alikosana na Chadema na kufukuzwa uanachama kutokana na kile kilichodaiwa ni kuandaa waraka wa mabadiliko ya 2013, sasa hivi ubunge wa EALA unaonekana kumvuruga tena mwanasiasa huyo na Chadema, baada ya kuandika barua kwa Spika wa Bunge akitaka utaratibu uliotangazwa wa namna ya kupata wabunge ubadilishwe.

Utaratibu huo mpya uliotangazwa, unatoa nafasi kwa wabunge wa EALA kwa mwaka 2017 kulingana na idadi ya wabunge wa kila chama kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa Mwongozo huo, kutokana na idadi ya wabunge wa vyama kwa kila chama, CCM imepata nafasi za wabunge sita kwenda EALA, Chadema mbili, CUF moja, huku ACT Wazalendo  pamoja na NCCR Mageuzi, vikiwa havina nafasi hata moja kwenye Bunge hilo la Afrika Mashariki, kutokana na kuwa na mbunge mmoja kila kimoja, hivyo kutokidhi vigezo.

Kutokana na hali hiyo, Zitto ameliandikia Bunge barua kutaka Kamati ya Kanuni za Bunge ikutane kujadili uchaguzi wa wajumbe wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

Barua hiyo, ambayo baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai inalenga kutaka utaratibu wa awali ubadilishwe ili chama cha Zitto (ACT Wazalendo), kimwingize mwanachama wake, Profesa Kitila Mkumbo kugombea ubunge huo, inasema mwongozo uliotolewa na Bunge umekwenda kinyume cha Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wanasema endapo hoja ya Zitto ikikubaliwa, ni rahisi zaidi wagombea wa Chadema wakakosa nafasi hizo na badala yake nafasi za upinzani kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki zikachukuliwa na wagombea wa ACT na wale wa CUF.

Hali hiyo inaelezwa kuchangiwa na wabunge wengi kwenye Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ni wa CCM, hivyo ni rahisi kuweka msimamo wa kuwapigia kura wale wagombea wa ACT Wazalendo na wale wa CUF, badala ya wale wa Chadema kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini kwa sasa.

Barua ya Zitto ya Machi 28 iliyoandikwa kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, ilisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na siyo uchaguzi.

Alisema pia mwongozo huo, mbali na kuvunja Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unataka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo.

Baada ya Zitto kuandika malalamiko hayo, Mwanasheria wa Chadema, John Malya, naye aliyajibu akirejea hukumu mbili za kesi ya Anthon Komu (kwenye Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani).

Malya aliandika kwamba, mwongozo wa Ofisi ya Spika wa Bunge wa kugawa idadi ya viti kwa vyama ni sahihi, kwa sababu Divisheni zote mbili za Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ziliamua.

Katika sehemu ya barua yake, alisema: “Mwenye kupaswa kubeba mzigo wa makundi ya Zanzibar, Bara na Wanawake (ukiachilia mbali kundi la vyama vya upinzani) ni chama chenye wabunge wengi (CCM)”.

Hoja hiyo ya Malya inachambuliwa na Ado Shaibu, ambaye aliandika ujumbe unaogusa hoja za kisheria ambazo alitumia Malya kukosoa malalamiko ya Zitto.

Shaibu alisema ni kosa kutumia kesi ya Antony Komu ambayo iliamuliwa na Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama ya Afrika Mashariki, lakini baadaye Divisheni ya Rufani ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ikatengua hukumu hiyo kwa hoja ya kwamba Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama haikuwa na mamlaka ya kuamua suala husika.

Hakuna tatizo la njaa nchini – Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ametoa wito kwa Watanzania kupuuza baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotoa taarifa kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la njaa huku akisema kuwa anayejua njaa ni Rais.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi mkoani Simiyu Rais Magufuli amesema kuwa taarifa hizo ni uzushi huku akisema kuwa kama yeye Rais wa Tanzania yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za njaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
“Wapo wafanyabiashara wengine wachache waliokuwa wamezoea panapotokea matatizo kidogo tu ya ukame wanatumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na magazeti wanayoyaamini wao sio magazeti yote, pamoja na baadhi ya wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa, anayejua njaa ni Rais na sio gazeti fulani mimi ndiyo niliyepewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania,” alisema.
Hivi karibuni kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita aliitaka serikali kutangaza balaa la njaa.

ZITTO KABWE ATOA TAMKO KUHUSU RASILIMALI NA MADENI YA TAIFA

Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya Viongozi.

Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ni matumaini yangu kwamba itafikia wakati Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.

Mfumo wa kuweka wazi Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu na muhimu kwenye vita vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa kadhaa duniani hutumia mfumo huu ( public disclosure of leaders' assets and liabilities) kuwezesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini Uingereza na Kanada kwa mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi lipo wazi kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye duka la vitabu la Bunge.

Namsihi Sana Rais John Pombe Magufuli kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria ya maadili ya Viongozi ili kurejesha na kuboresha Miiko ya Viongozi katika kuimarisha vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais aliahidi kuweka wazi Mshahara wake alipokuwa anazungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV. Ninamkumbusha afanye hivyo na pia aweke wazi Mali, Madeni na Maslahi yake ya Kibiashara ili awe mfano kwa Viongozi wengine Nchini.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini
30/12/2016

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE BAADA YA KUPATA MTOTO WA KIKE LEO

Ameandika ''Mimi na Mke wangu mpendwa tumebarikiwa na Allah kupata mtoto wa kike. Mtoto na mama yake wana afya njema kabisa, Mashaallah. Mtoto amezaliwa saa moja na dakika 45 asubuhi leo Disemba 27, 2016''''.

''Binti yetu ataitwa Josina - Umm Kulthum. Josina kwa heshima ya mwanamama mpigania Uhuru wa Kusini mwa Afrika, Josina Muthembi Machel wa FRELIMO. Umm Kulthum kwa heshima ya mama yangu mdogo na pia jina la binti wa Mtume Muhammad (SAW)''
''Tunamshukuru mungu kwa Baraka hizi za mtoto Josina - Umm Kulthum Zitto'' Kabwe Z. Ruyagwa Zitto

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Disemba 27, 2016
Dar Es Salaam

ZITTO KABWE AMTEMBELEA LEMA MAHABUSU, ATOA NENO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Jana  Ijumaa desemba 2/2016 nilipata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza Kuvu la Arusha. Nilimtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati Za kutafuta na kulinda Haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa Sana na ukiukwaji mkubwa wa Haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona Ni bora akae ndani Mpaka hapo Dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka Mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.

Amemshukuru Mungu Kwa kumpa Mke jasiri anayempa moyo na Ndio ngome yake Kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka Haki kutendeka Katika uendeshaji wa Nchi yetu. Siku zote Haki hushinda

Majibu ya ACT Wazalendo kwa Ole Sendeka baada ya kutaka Zitto achunguzwe

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya kiongozi wake wa chama, Zitto Kabwe kwamba ana miliki mali za kifisadi pamoja na kuhusishwa na ununuzi wa ardhi maeneo ya Kigamboni uliofanywa na NSSF kwa bei ya milioni 800 kwa ekari moja, wakati bei halisi ni milioni 25 na kwamba kitendo hicho kimeitia hasara serikali .

Tuhuma hizo zilitolewa jana na Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Christopher Ole Sendeka, ambapo alivitaka vyombo vya uchunguzi kufanya uchunguzi katika shirika hilo ili kubaini waliohusika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria, huku akimhusisha Zitto katika uchunguzi huo.

Ole Sendeka alitaka akaunti za benki za Zitto pamoja na maisha yake binafsi kuchunguzwa kama yana uhalisia na kipato chake halali.

Tuhuma hizo zimekiibua chama cha ACT, ambapo leo Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa ACT, Habibu Mchange amevitaka vyombo vya uchunguzi haraka iwezekanavyo kuchunguza mali, madeni, akaunti zote za benki pamoja na mfumo wa maisha ya Zitto.

“ACT imeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa jana na Ole sendeka dhidi ya kiongozi wa chama chetu,” amesema.

Amesema kuwa, katiba ya chama hicho huwataka viongozi wote kuweka hadharani matamko ya mali zao na madeni na kwamba Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria hivyo mali na madeni yake yako hadharani na mtandaoni.

“Tunaamini kama kuna kiongozi ambaye mali, madeni, maslahi, na akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto,” amesema.

Aidha, Mchange amedai kuwa, kilichomsukuma Sendeka kutoa tuhuma hizo kwa Zitto ni harakati zake za kuupinga muswada mpya wa habari.

“Tuhuma za ole sendeka kuna kitu nyuma yake, jitihada za zito za kupambana na mswada wa habari ndizo zilizomuibua, sababu wanataka upitishwe ili kuviua vyombo vya habari,” amesema.

Amesema ACT itaendelea kuisimamia serikali katika mambo ya bungeni kama anavyofanya mbunge na kiongozi wao wa chama.