HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Tahadhari ya matapeli - wizara ya afya

TAARIFA ZA KUITWA KAZINI KWA MADAKTARI WALIOKUWA WAMEKIDHI VIGEZO KWENDA KUFANYAKAZI NCHINI KENYA.




Rais Maguli Afuta Zaidi ya Ajira Elfu 9 Za Walioghushi Vyeti

Rais  Dk. John Pombe Magufuli, ameiagiza Wizara ya Fedha kufuta mara moja ajira za  watumishi wa umma 9,932 waliobainika kughushi vyeti, kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma.

Akiongea leo mara baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mjini Dodoma, Rais Magufuli pia amewataka watumishi hao kuondoka wenyewe na iwapo watakaidi wakamatwe na vyombo vya dola na kushtakiwa.

Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.

Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema, kwa Mujibu  wa Kanuni na Sheria za nchi zinabainisha wazi kuwa mtu atakaebainika kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha Jela.

Serikali Yatangaza Ajira Mpya 52,436

Serikali inakusudia kuajiri watumishi wapya wa umma 52,436 katika mwaka ujao wa fedha. 

Aidha, madaktari wapya 258 waliokuwa waende kufanya kazi nchini Kenya, lakini wakakwama kutokana na kuwekewa pingamizi la kimahakama na wenzao wao huko na hivyo Rais, Dk John Magufuli kuamuru waajiriwe mara moja nchini, wanatarajiwa kuanza kazi keshokutwa Jumatatu.

Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).

“Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti.

“Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi ya watu 9,700 na tutaendelea kufanya hivyo, na hivi karibuni Rais amebariki kuajiriwa kwa madaktari wapya 258 na Jumatatu (keshokutwa) wanaripoti kazini.

"Tutaendelea kuajiri na wataalamu wa kada nyingine, kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha mwezi Juni tutakuwa tumejiajiri kwa idadi tutakayoipanga kwa awamu, na katika mwaka ujao wa fedha tutaendelea kuajiri watumishi wengine wa umma zaidi ya 52,436,” alisema.

Hata hivyo, alisisitiza Serikali itahakikisha hairudii makosa ya kuajiri watumishi hewa, wasio na sifa na weledi unaohitajika. 

Alisema kwa kiasi kikubwa uhakiki wa watumishi wa umma kwa ujumla umekwisha, lakini kazi hiyo ni endelevu, kwani serikali itaendelea kufanya hivyo mara kwa mara.

Alisema matunda ya uhakiki wa watumishi wa umma umebaini watumishi hewa 19,708 na ambao wameshaondolewa katika orodha ya mishahara ya watumishi wa umma. 

“Hawa wangeachwa, Serikali ingekuwa inapoteza kiasi cha Sh bilioni 19.8 kila mwezi, lakini fedha hizi zimeokolewa kupitia uhakiki wa watumishi wa umma.

"Tunafanya haya kwa nia njema. Mathalani tusingewatoa hawa, si wangeziba nafasi za ajira za wengine na fedha ngapi zingepotea?” alihoji. 

Alisisitiza kuwa, wizara hiyo itaendelea kutimiza majukumu yake kwa vitendo ili kurejesha nidhamu ya serikali na utumishi wa umma kwa kuongeza uwazi na kusimamia sheria, kanuni na taratibu za uwajibikaji wa viongozi wa watumishi wa umma ili wawajibike kwa wananchi ambao ndio wateja na waajiri wakuu wa watumishi wa umma.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akijibu hoja za wabunge, hasa la uhamisho wa watumishi wakiwemo wanandoa wanaotenganishwa, alikemea tabia ya maofisa watumishi kuzuia wenye ndoa kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwa lengo la kuwafuata wenzao.

Alisema kuwazuia ni kuwanyima haki ya msingi, na kuwaagiza wabunge katika maeneo yao wasaidia kusimamia haki za watumishi. 

"Lazima sheria za utumishi zizingatiwe, walimu hawa au watumishi wanayo haki ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini pia kuishi na wenza wao, lakini utadhani mtumishi anapoomba ni kama anasaidiwa, hapana ni haki yake ya msingi, waheshimiwa tusimamie haki za watumishi,” alisema Simbachawene

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA AJIRA KWA VIJANA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha hoja katika mkutano wa Tano wa Bunge linaloendelea Mjini Dodoma.


Na mwandishi wetu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia vijana kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo nchini ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na  kutimiza adhma ya kuleta maendeleo hususani kwa vijana.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni Mhe. Maulid Mtulia iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge unaoendelea Mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwa Serikali ina mipango na mikakati madhubuti inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini.

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuweka mikakati ikiwemo uwanzishwaji wa programu mbalimbali zitakazo saidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuangalia matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zimepelekea kuwa na programu zinazolenga kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana” Alisema Waziri

Alisisitiza kuwa programu hizo ni pamoja na; kurasmisha ujuzi usio rasmi kuwa rasmi, mfumo wa mafunzo kwa vitendo, mfumo wa uanangezi pamoja na kukuza mafunzo kwa watanzania kulingana na soko lililopo kwa sasa.

Pamoja na juhudi hizo zinazotarajiwa kuzaa matunda bado Waziri aliwatoa hofu wananchi wote kwa kuwepo kwa fursa hizo za ajira zitakazo jali hali za watu pasipo kuangalia makabila yao, rangi wala dini.

“Katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hatuta angalia kabila, rangi wala dini ya mtu bali kutakuwa na haki na usawa”.Alisisitiza Waziri

Aliongezea kuwa, Serikali pia inajitihada za kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.

“Serikali itatumia sekta zenye uwezo wa kutoa ajira kwa wingi ikiwemo zile za Kilimo, majenzi, Mawasiliano na Utalii ili kuzitumia kuweka mazingira mazuri kwa vijana kupata fursa za ajira”.

Mhe. Mhagama alisisitizia bungeni kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika zitatumika kama chachu ya kuangalia maeneo yanayohitaji kusaidia kwa haraka na kupunguza changamoto hiyo kwa vijana.

“Kwa kuangalia tafiti ya Hali ya Ajira Nchini ya mwaka 2014 imeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014 na ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014”,alisema.

Hata hivyo, Waziri Mhagama alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo Serikali bado ina wajibu wa kuongeza jitihada zaidi ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa ajira na kuboresha maisha ya vijana.


SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUWA ITAANZA KUTOA AJIRA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


1.Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.

2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha

Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.


3.Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.

5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali. 

Imetolewa na:

SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ZA TANGAZO LA AJIRA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.




WASOMI WAIPONGEZA MeTL GROUP KWA KUFANYA CAREERS FAIR, 25 KUPATA AJIRA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


  Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza  vyuo  ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.(Habari picha na Modewjiblog).
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumzia idara yake ya masoko inavyofanya kazi wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
 Mtaalamu wa kilimo wa kampuni ya MeTL Group, Bw. George Mwamakula akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
 Mtaalamu wa masuala ya fedha wa MeTL Group, Bi. Hasina Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
  Mtaalamu wa idara ya uzalishaji wa nyuzi na nguo ya MeTL Group, Bw. Clement Munisi akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
Mtaalamu kutoka kitengo cha mauzo wa MeTL Group, Bw. Yusuf Ali, akizungumza kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
 Mtaalamu wa idara ya uzalishaji na matengenezo wa MeTL Group, Bw. Vijay Raghavan akizungumza kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
 Washiriki wakiuliza maswali juu uendeshaji wa vitengo mbalimbali vya makampuni ya MeTL Group wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
 Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kongamano hilo.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer (katikati) akikabidhi box la zawadi kwa mmoja wa washiriki aliyejishindia kwenye mchezo wa kuokota majina wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji.

Na Mwandishi Wetu
Safari ya Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) kutoa ajira kwa Watanzania 100,000 hadi mwaka 2021 imeanza kufanyika kupitia Job Affairs ambapo limewapa nafasi wasomi mbalimbali nchini kutumia sehemu hiyo kuonyesha uwezo wao, na kati yao wasomi 25 wakipata nafasi ya kujiunga na familia ya zaidi ya wafanyakazi 28,000 wa kampuni ya MeTL Group.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanyika kwa kongamano hilo, wasomi mbalimbali waliipongeza kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kufanya kongamano la Job Affairs kwani licha ya kutoa nafasi za kazi lakini pia limewasaidia kujijengea uwezo mpya ambao hawakuwa nao awali.
Mmoja wa wasomi hao, Dennis Mtani alisema kupata nafasi ya kuhudhuria kumewajengea jambo lipya kuhusu jinsi ya kuomba nafasi za kazi hadi kuwa wafanyakazi bora katika kampuni.

Alisema kutokana na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprises kwa bara la Afrika ni matarajio yao kuwa wamejifunza jambo ambalo hata kama hawatapata nafasi za kazi basi watabaki na uwezo ambao utawasaidia kujua jinsi ya kuomba nafasi katika makampuni mengine ya kimataifa.

“Tumekuja katika kongamano hili wengine hata CV walikuwa hawajui jinsi ya kuandika ili kuomba nafasi na kuajiriwana na kutokana na ukubwa wa hii kampuni kwa nchi za Afrika tumepata elimu ambayo inaweza kutusaidia kwenda kufanya kazi kwa makampuni mengine,” alisema Mtani.

Nae Monica Mziray alisema alijumuika katika kongamano hilo ili kujaribu kutafuta nafasi ya kujiunga na kampuni ya Mohammed Enterprises kwani anaamini ni kampuni kubwa ambayo anaamini ana ndoto za kuifanyia kazi na ambayo inawajali wafanyakazi wake.

“Nimefanya kazi na kampuni zingine lakini niliacha sababu nataka kampuni ambayo inanilia vizuri na inanipa kitu na mimi naipa kitu, nilisoma historia ya Mohammed Enterprises, nimeona ni kampuni kubwa Afrika, nimeona bidhaa zake na naona inaweza niongezea kitu,” alisem Mziray.

Aidha akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji aliwambia washiriki ambao wametoka katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu, kwamba Idara ya Rasilimali Watu ya MeTL imekua ikitoa ajira, mafunzo ya kukuza vipaji kwa watanzania wa kada mbalimbali ili kuchukua nafasi za juu katika Makampuni shiriki ya MeTL.

Kuhusu kongamano hilo la kazi alisema linalengo la kupata wasomi wenye taaluma mbalimbali kutoka kwa vijana wa Kitanzania. Kwamba Idara ya Rasilimali Watu imelenga kupata wahitimu katika nyanja za Uhasibu wa fedha, Rasilimali watu, Masoko, Uhandisi, Kilimo na Viwanda vya nguo lakini pia vijana wasomi watapewa mafunzo kwa kipindi cha wiki 52 huku wakiwa wanalipwa na watakapomaliza mafunzo watapewa ajira na kuingizwa katika mfumo wa uwajibikaji.

“Kundi la Makampuni ya MeTL limepata umadhubuti wake kutokana na kuwa na utamaduni wa kuhakikisha kwamba wanakuwa karibu na wafanyakazi wake na kuwajali. Wafanyakazi wa Idara ya Rasimali Watu wamekua wakiandaa mafunzo kuboresha elimu ya wafanyakazi, maarifa na utaalamu,

“Ushiriki wa wafanyakazi ni sehemu ya maono ya wafanyakazi wa Idara ya Rasilimali Watu katika kundi hili la makampuni. Kampuni hii huhakikisha kwamba wafanyakazi wanapata mapumziko, kujitengeneza upya, wanakuwa na siku ya familia, siku ya michezo na kwamba shughuli hizo zinafanywa kwa mpangilio ili kuwezesha kuwepo kwa utamaduni  wa familia moja  inayofanya kazi kwa kushirikiana kwa kiwango cha juu,” alisema Dewji.

USAJILI WA METL CAREER FAIR (JOB BONANZA) KUFUNGWA LEO JUMAMOSI CHANGAMKIA FURSA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kama wewe ni mhitimu katika Uhandisi au Utawala (Masoko, Mahusiano, Fedha) na una hari ya kujifunza, ukiwa na mtazamo chanya wa mafanikio na mfuatiliaji wa maadili katika kazi, njoo ujiunge nasi katika bonanza hili la uchambuzi wa ajira.
Rasilimali Watu
Mauzo
Uhasibu
Masoko
Uhandisi
Kilimo
Nguo

Kwani unaweza ukawa mmoja kati ya watu 25 tutakaowachagua kwa ajili ya kujiunga kwenye programu ya uendelezaji wa wahitimu wa vyuo vikuu.
Na ukibahatika kuwa mmoja wapo kati ya hao utapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo katika viwanda vyetu vilivyopo maeneo mbalimbali.
Pia utapata nafasi ya kufundishwa mifumo ya uendeshaji wa viwanda vya kisasa.
Utakuwa chini ya wakufunzi waliobobea katika kazi zao duniani ambao watakuwezesha wewe kukua katika kazi na kushika nyadhifa kwenye kazi yako.
Zaidi ya yote hayo utakayofanyiwa pia utalipwa ilikujifunza

Kwa taarifa zaidi tazama vipeperushi vyetu: