HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

WAZIRI MKUU MAJALIWA - WATANZANIA WATAKIWA KUDUMISHA MUUNGANO

 Waziri Mkuu   Kassim  Majaliwa  akisalimiana na Rais Mstaafu  wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi, Baada ya Duwa ya Siku  ya Karume  iliyofanyika April 7, 2017 katika Viwanja  vya Afisi za CCM Kisiwandui  Unguja  Zanzibar  Katikati ni Makamu wa  Rais Mstaafu  Dk. Gharibu Bilali.
Waziri Mkuu   Kassim  Majaliwa  akisalimiana na Mama Fatma  Karume Mke wa Hayati Rais wa kwanza  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Zanzibar  Shekh  Amani Abeid Karume, Baada ya Duwa ya Siku  ya Karume  iliyofanyika April 7, 2017 katika Viwanja  vya Afisi za CCM Kisiwandui  Unguja  Zanzibar  katikati ni Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la Mauwa katika Kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume baada ya Dua ya Khitma iliyofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar jana. (Picha na Ikulu).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi na wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani kushirikiana kwa pamoja katika kuimarisha na kuulinda Muungano ulioachwa na waasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Aprili 7, 2017) mara baada ya kushiriki hitma na kuzuru kaburi la Sheikh Karume lililoko Afisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja wakati wa maadhimisho ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Sheikh Abeid Karume sambamba na siku ya Mashujaa Zanzibar

Amesema ni muhimu kwa wananchi kutenga muda wao na kuwaombea viongozi wetu waliotangulia mbele ya haki, lengo likiwa ni kukumbuka na kuenzi mchango mkubwa waliotoa katika kujenga msingi wa maendeleo ya Taifa.

Waziri Mkuu amesema Watanzania wote Bara na Visiwani ni wamoja kiasili, hivyo wanapaswa kushirikiana katika kudumisha misingi iliyoachwa na waasisi wa Taifa ili kuweza kujiletea maendeleo

Pia amewaomba Watanzania wote kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja kuulinda na kuudumisha Muungano ulioachwa na waasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Karume.

“Tuhakikishe Muungano huu tulioachiwa na wasisi wa Taifa letu unadumu ili tuendelee kuwa wamoja na kuzungumza lugha moja ya kuboresha maendeleo na kulinda amani na utulivu wa nchi yetu,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amesema katika kutambua umuhimu wa viongozi hao Serikali imetenga siku maalumu kwa ajili ya maadhidhimisho ya vifo vya viongozi hao na kutoa fursa kwa wananchi kila mtu kwa imani yake kuwaombea dua na kutafakari namna walivyojitoa kwa taifa letu.

Maadhimisho ya kifo cha Sheikh Karumbe ni Aprili 7 ya kila mwaka na Hayati Mwalimu Nyerere ni Oktoba 14 ya kila mwaka.

Maadhimisho hayo ya kifo cha Sheikh Karume yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.

Wengine ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Sheikh Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, wazee wa CCM pamoja na wananchi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

IJUMAA, APRILI 7, 2017.

RAIS DKT MAGUFULI AZURU KABURI LA MAREHEMU SHEIKH ABEID AMANI KARUME, AWEKA SHADA LA MAUA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoka katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016 baada ya kuweka saini kitabu cha wageni kabla ya kuzuru na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoa heshima zake baada ya akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Septemba, 2016 ameendelea na ziara yake Visiwani Zanzibar ambapo majira ya Asubuhi amezuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume lililopo kando ya Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) eneo la Kisiwandui Zanzibar.

Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi hilo na baadaye wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume na kuombea amani.

Viongozi mbalimbali wa Dini na Siasa akiwemo Rais Mstaafu wa Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume ikiongozwa na Mjane wa Marehemu Mama Fatma Karume wamehudhuria.

Baada ya kuzuru kaburi la Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume, Rais Magufuli amezuru kaburi la Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi lililopo nyumbani kwake Migombani Zanzibar.

Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika kaburi la Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi na pia wametoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu.

Wakizungumza katika Dua ya kuwaombea Marehemu wote wawili Viongozi wa Dini kutoka madhehebu ya Kiislamu na Kikristo wameomba kuwepo kwa amani na upendo kwa watanzania wote kama ambavyo waasisi wa Taifa walipigania.

Baadaye leo Rais Magufuli atazungumza na Wananchi wa Zanzibar katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Demokrasia wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Unguja
03 Septemba, 2016
 Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiwa na Mama Fatma Karume baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiwa na Mama Fatma Karume baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiwa na Mama Fatma Karume baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.

PICHA NA IKULU