-
BONANZA LA MICHEZO NA MAZOEZI KUFANYIKA PEMBA: JULAI 20 - 28, 2024
By: VIJIMAMBO on July 21, 2024 / comment : 0 michezo
Tazama Hapa Ratiba Nzima na Makundi Yote ya Kagame Cup 2018
By: VIJIMAMBO on June 05, 2018 / comment : 0 michezo
Wakongwe wa soka Tanzania, Simba SC na Yanga SC wamepangwa Kundi C katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Akitaja makundi ya michuano hiyo, Katibu wa kudumu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye alisema kwamba pamoja na Simba na Yanga, timu nyingine katika Kundi hilo ni Dakadaha ya Somalia na Saint George ya Ethiopia.
Musonye alisema kwamba Kundi A linaundwa na timu za Azam FC, KCCA ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini, wakati Kundi B linaundwa na timu za Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti. Musonye aliishukuru Tanzania kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo na akasema kwamba anatarajia itafana kwa sababu ya rekodi ya nchi hii kuandaa mashindano yaliyokuwa na msisimko mkubwa miaka ya nyuma.
Musonye ambaye alisema mashindano yatafanyika viwanja vya Taifa na Azam Complex, Chamazi – pia amewapongeza Rwanda na Rais wao, Paul Kagame kwa kuwa wadhamini wa mashindano haya kwa zaidi ya miongo miwili sasa.
Musonye amesema kwamba wamelazimika kufanya mashindano ya mwaka huu sambamba na Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, kwa sababu wasipofanya mwezi huu hayatafanyika tena kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Hata hivyo, Musonye amesema kwamba watatoa ratiba nzuri ambayo haitaruhusu mashindano ya mwaka huu kuingiliana na mechi za Kombe la Dunia.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando alisema kwamba wataitumia michuano hiyo kukizindua kituo chao chao Redio, Uhai FM na akawahakikishia kwamba pamoja na mashindano hayo kufanyika sambamba na Kombe la Dunia, lakini yatafana
FIFA imeridhia Kagame kufanyika mwezi huu tofauti na agizo lake la kutotaka katika mwezi wa Fainali za Kombe la Dunia yasifanyike mashindano mengine yoyote, kwa sababu washiriki watano wa michuano hiyo wapo kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Afrika, ambayo kwa sasa imesimama kupisha Kombe la Dunia itarejea Julai baada ya kumalizika kwa michuano hiyo nchini Urusi.
Hao ni KCCA ya Uganda iliyopo Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Afrika na nyingine nne kwenye Kombe la Shirikisho ambazo ni Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda, Yanga ya Tanzania zilizopoi Kundi D zote na Al-Hilal ya Sudan iliyopo Kundi A.
Na kwa sababu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Afrika itakwenda hadi Agosti, mwezi ambao msimu mpya wa Ligi Kuu nyingi duniani huanza – michuano ya Kagame isipofanyika mwezi huu kuna hatari isifanyike tena na mwaka huu kwa mara ya tatu mfululizo.
Azam FC ndiyo mabingwa wa mwisho wa michuano hiyo ilipofanyika Tanzania, walipowafunga Gor Mahia 2-0 katika fainali Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, mabao ya waliokuwa washambuliaji wake hatari, John Raphael Bocco dakika ya 17 na Muivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 64.
Na hiyo ndiyo ilikuwa michuano iliyomtoa mshambuliaji Mkenya, Michael Olunga ambaye kwa sasa anachezea Girona FC ya Hispania kwa mkopo kutoka Guizhou Zhicheng ya China.
Baada ya kufungha mabao matano akiwa na Gor Mahia na kuibuka mfungaji bora akiwapiku , Osman Bilal Salaheldin wa Al-Khartoum ya Sudan aliyefunga mabao manne sawa na Tchetche wa Azam FC, Olunga akachukuliwa na Djurgardens IF ya Sweden mwaka 2016 iliyomuuza Guizhou Zhicheng mwaka 2017.
Na Tanzania itawakilishwa na Azam FC kama mabingwa watetezi wa mashindano na Yanga SC, kama mabingwa wa nchi.
MSIMAMO WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA LEO JUMAPILI MAY 13, 2018
By: VIJIMAMBO on May 13, 2018 / comment : 0 michezo
Ni rasmi sasa kuwa Mbeya City wamejinasua na kadhia ya kushuka daraja baada ya kufikisha alama 30 kwenye msimamo wa ligi baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons leo.
Mnyukano sasa umebaki kwa timu nne za mwisho ambazo ni Mbao FC, Majimaji FC, Ndanda SC na Njombe Mji.
Kati yao timu mbili zitashuka, mbili zitaendelea na VPL msimu ujao. Nani 'atakatwa' nani atapona?
UZINDUZI WA COPA UMISSETA SINGIDA WAFANA
By: VIJIMAMBO on May 09, 2018 / comment : 0 michezo
Wawakilishi wa shule za sekondari wakipokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Coca-Cola kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahia zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akijiandaa kupiga penati wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo.
Na Mwandishi Wetu- Singida.
Mashindano ya Copa Umisseta ngazi ya mikoa yanaendelea ambapo yamezinduliwa mkoani Singida, katika uwanja wa Namfua ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi, aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo.
Hafla ya uzinduzi huo wa michezo hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya Coca-Cola pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo, wadau wa michezo, walimu na wanafunzi wa shule za sekondari ambao walishiriki kucheza michezo mbalimbali.
Mkuu wa mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi katika hotuba yake ya ufunguzi,aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kutoa udhamini kwa michezo hiyo na amewaasa washiriki ambao ni wanafunzi kuyatumia kuboresha afya na akili ili kuepuka kushiriki katika matendo ya kihalifu kama matumizi ya madawa ya kulevya na kutojihusisha na mapenzi kabla ya wakati.
Alisema mashindano hayo ni jukwaa kubwa la kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo na Ushahidi wa suala hili upo kwa kuwa kuna wanamichezo wengi wanaotokea mkoani Singida ambao vipaji vyao viliibuliwa na Umisseta vilevile mkoa huo katika mashindano ya mwaka jana ulifanya vizuri katika ngazi ya kitaifa kwa kushika nafasi ya tatu.
Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa bidhaa za Coca-Cola mkoani Singida, Joseph Simplis ,amesema Coca-Cola imekuwa ikidhamini mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 na lengo kubwa ni kuhakikisha inawashirikisha wanafunzi wengi zaidi nchini sambamba na kuibua na kukuza vipaji vya michezo.Aliwaasa wanafunzi wa Mtwara kuchangamkia fursa hii.
Katika kufanikisha michezo hii, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikitoa udhamini wa vifaa vya michezo ambapo imelenga kusambaza vifaa kwa shule za sekondari 4,000. Katika uzinduzi huo alikabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni kwa wawakilishi wa shule mbalimbali mkoani humo.
Uzinduzi wa Copa Umisseta mkoani Singida ni wa tano kufanyika baada ya kufanyika katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Mtwara na Zanzibar. Mashindano hayo ngazi ya kitaifa yatafanyika mwezi Juni mwaka huu mkoani Mwanza.
AWESO CUP 2018 YAZINDULIWA KWA KISHINDO, SIMBA WAILIZA YANGA PANGANI
By: VIJIMAMBO on May 07, 2018 / comment : 0 michezo
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizindua mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga. Pembeni ni Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mwenye kofia nyeusi) ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja (mwenye traki suti bluu), Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza na msemaji wa Simba, Haji Manara na Jerry Muro.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza na Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mwenye kofia nyeusi) pamoja na viongozi wengine wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja mara baada ya kumaliza kuzindua mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga.
Picha ya pamoja.
Wachezaji wa Simba tawi la Pangani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Wachezaji wa Yanga tawi la Pangani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Wachezaji wa Yanga tawi la Pangani wakiwapasha.
Wachezaji wa Simba tawi la Pangani wakiwapasha.
Wasanii wanaunda kundi la Uzalendo Kwanza wakifuatilia mtanange huo.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana na waamuzi wa mtangane.
Akisalimiana na wachezaji wa Simba tawi la Pangani.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana nawachezaji wa Yanga.
Tambo za watani wa Jadi, Jerry Muro akitoa yake.
Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo akimpa sapoti Msemaji wa Simba, Haji Manara wakati akionyesha vitu vyake. Pembeni ni Mwakibinga.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah Issa akipatiwa hela na Msemaji wa Simba Haji Manara.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana na Msemaji wa Simba Haji Manara.
Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana.
Ilikuwa ni vuta ni kuvute...
Wachezaji wakionyesha umwamba.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza na Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mwenye kofia nyeusi) wakifuatilia ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akiwa na Mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa wakifuatilia ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga.
Asha Boko na Tausi wakionyeshana umwamba huku Msanii Nuh Mziwanda akitoa burudani.
Umatu wa watu waliohudhuria.
Mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa akiongea na wanachi wa Pangani wakati wa zoezi la kugawa zawadi.
mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa
Zawadi ya Jezi zikitolewa.
Wachezaji wa Yanga na Simba wakiwa wamebeba zawadi ya Maziwa ya Asas.
Picha/Habari na Cathbert Kajuna na Oscar Assenga- Pangani.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amefungua mashindano ya kombe la Aweso katika uwanja Kumba wilaya Pangani na kuwataka viongozi wa halmashauri ya Pangani kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vya kuchezea.
Katika kufanikisha ufunguzi wa kombe la Aweso wasanii wa filamu wanaunda kundi la Uzalendo Kwanza walishiriki ili kuhamasisha vijana kupenda michezo na sanaa.
Akifungua mashindano hayo Naibu Waziri Juliana Shonza akatoa agizo kwa viongozi wa halmashauri kukarabati viwanja huku mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa amesema kuanzisha kwa kombe la Aweso kuanarudisha ari ya michezo wilayani humo.
Kwa upande wake Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo amesema katika mashindano hayo watapatika vijana wenye vipaji.
Nae mwenyekiti wa uzalendo kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema ushiriki wao unasaidia vijana kupenda michezo na sanaa.
"Tumekuja kuwaamsha vijana wenzetu ili watambue umuhimu wa kuwa Wazalendo na kujikwamua na watambue vipaji vyao, maana vijana wengi wamepoteza matumaini ya kuishi kutokana na kujiona wametengwa na jamii" amesema.
Jumla ya timu 20 zinashiriki michuano ya kombe la uweso ambapo timu shiriki zikabidhiwa vifaa vya michezo na naibu waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo.
Katika ufunguzi wa kombe hilo uchezwa mchezo wa mashabiki Simba na Yanga ambapo timu ya Simba ikiongozwa na Msemaji Haji Manara waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Yanga na wakapata maziwa ya Asas na fedha laki tano huku Yanga wakipata laki tatu na maziwa ya Asas. Huku zikishuhudiwa na Naibu Waziri wa Habari Michezo, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mkuu wa wilaya Pangani, Zainabu Issa, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja.
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhe. Abdallah Mitawi, ametembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa lengo la kufahamu ...
-
November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Huma...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Septemba 8, 2026, imeendesha Warsha ya Mafunzo kuhusu Uandaaji wa Hesabu kw...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015
November 01, 2015
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014



















.jpeg)


