HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Wema Sepetu atoa jibu juu ya shepu yake

Ikiwa ni wiki imepita tangu malkia wa filamu Bongo Wema Sepetu, kuposti picha kadhaa katika mtandao wa kijamii wa Instagram kuonesha umbo lake, mwana dada huyo ameamua kuwajibu wale wanaodhania shepu hiyo sio yake.

Wema ambaye kwa sasa hataki kujihusisha na skendo yoyote ameandika “Shepu ya mwendokasi… Ndo niliojaliwa nayo… Kama imeanzia kiunoni kwenda magotini ndo niliojaliwa nayo… Kama wewe hauna basi mshukuru Allah… Ndo nilivyoumbwa jamani… Sio mimi bali ni Maulana ndo alionibariki nayo… Hata ingekuwa kwanzia kichwa hadi Vidole vya miguuni ni sawa pia… Ndo niliojaliwa nayo.”
“Sometimes najiangalia kwenye kioo sijimalizi… Ndo majaliwa yangu… Ndo yangu basi… Imenizidia… Allah Subhanah wataallah ndo amenipa… Aaaah….!? Sio shepu ya kawaida… Niacheni na Shepu yangu jamani… Ndo nishaimiliki mie… Siwezi kuitoa…. 🙄🙄🙄🙄,” ameandika mrembo huyo.

Jackline Wolper – Nataka nirudi shule

 Muigiza wa Filamu Bongo, Jackline Wolper amedai anataka kurudi shule mara baada ya kuona picha za Jux alizopiga katika mahafali yake ya kumaliza elimu ya juu nchini China.

Wolper kupitia instagram ameandika, “nimekumbuka mbali kweli nilivyoiona hii picha, nakumbuka siku hizo mwenyewe ndo nakupeleka airport unaenda kuanza kusoma mpaka na mimi nilitamani kuwa mwanafunzi ili twende wote yaani naandika hii caption huku nasmile nikikumbuka hiyo siku ndo unaenda kusoma mwenyewe…am very happy for you mwanafunzi wangu! yani verrrrry happy…!
Ameongeza, “hongera sana siku hizi vijana wanafanya yote na shule ipooo ndo unazidi kuwa mnyamweezi, mimi mwenyewe hapa nataka nirudi shule ya kutafuta hela manake maisha magumu sana… Hongera sana kwa kuhitimu..!!nisaidieni kumtag mwanafunzi wangu,” amemaliza kwa kuandika.

Rose Muhando Atiwa Mbaroni mkoani Singida kwa Utapeli

Jeshi  la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mwimbaji huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake ambao ni Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo wilayani humo.

Inadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na Mwenyekiti wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh 800,000 ambapo zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa angekwenda kwenye uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo hakutokea.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike Novemba 13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida.

Novemba 8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa ajili ya nauli ya kutoka Dodoma kwenda Singida yeye na wasaidizi wake, fedha ambayo ilitumwa na mawasiliano yakaendelea kufanyika ili kuakikisha kuwa siku ya tukio anakuwepo.

Chakushangaza, siku ya tukio msanii huyo hakujitokeza na walipata taarifa kuwa yupo Kahama anatoa huduma, walipofanya mahojiano walithibitisha kuwa ni kweli.

Alipofanyiwa mahojiano na Polisi, Rose Muhando alikiri kutenda kosa hilo kwa kutotoa taarifa kwamba hawezi kuja na alieleza si kweli kwamba alikuwa kahama, bali alikuwa na mgonjwa nyumbani hivyo hakuweza kutoka. Muhando amesema kuwa yupo tayari kurejesha fedha hizo alizotumiwa.

Vanessa Mdee adai kuna msanii mkongwe anamchafua

Vanessa Mdee ameshindwa kuyavumilia yanayomtoka kinywani mmoja kati ya vigogo anaowaheshimu kwenye sanaa ya muziki nchini, hali iliyomsukuma kuanika ya moyoni. 

Vee Money ambaye anafanya vizuri na wimbo wa ‘Duasi’ alioshirikishwa na Legendary Beatz ametumia mtandao wa Twitter kuyatoa ya moyoni dhidi ya kigogo huyo, ingawa hakuweka wazi jina lake.

“Inasikitisha kwamba mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa kila kukicha jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka,” inasomeka tweet ya kwanza ya Vee Money.

Hata hivyo, mwimbaji huyo ameamua kuweka heshima yake mbele na kujiepusha na majibishano kwani kufanya hivyo anaamini kutakuwa utovu wa nidhamu.


Mwaka huu umeendelea kuwa mwaka wa mafanikio ya kupanda zaidi katika ngazi za kimataifa kwa Vee Money, ingawa amekuwa akikumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutajwa kwenye orodha ya wasanii waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

Msanii huyo ameendelea kukubalika ndani na nje ya nchi ambapo amekuwa akipewa mashavu kadhaa kung’arisha nyimbo za wasanii wa nchi za Afrika Kusini na Afrika Magharibi.

Sipendi maisha ya Ustaa - Madam Flora

Madam Flora (zamani Flora Mbasha) amesema hayo hivi karibuni ikiwa ni siku chache kuelekea ndoa yake ambapo amefunguka na kudai kuwa baada ya kumpata mwanaume ambaye siyo maarufu anafurahi kwani hata mfumo wa maisha yake utaenda kubadilika na kuishi kama watu wengine ambao siyo maarufu.

"Mume wangu mtarajiwa siyo mtu anayejulikana bali naamini kwenye ulimwengu wa kiroho anajulikana. Namshukuru Mungu maisha mapya ambayo naenda kuyaishi siyo ya umaarufu. Mimi nimemwambia pamoja na ustaa nilionao napenda tuishi maisha ya kawaida ambayo hayahusiani na umaarufu wangu. Unajua kuna wakati natamani kushuka kwenda kula chakula kwa mama n'tilie lakini watu watashangaa hata wewe? sasa najiuliza who is Flora? kumbe mimi pia ni mtu wa kawaida kabisa. Sitamani maisha ya Ustaa yananinyima uhuru"- Madam Flora.

Aidha Flora amefunguka kuhusu mahusiano yake na kwamba kabla ya kukubali kuolewa kwa mara ya pili ilimchukua zaidi ya mwaka mmoja kutafakari ikiwa ni pamoja na kushirikisha familia kwa ajili ya maombi. "Mimi na David tuna miaka miwili na nusu ya urafiki wa kawaida lakini aliponiambia kuhusu suala la ndoa nilikaa mwaka mzima kutafakari kwa sababu nilikuwa natamani mwanaume atakayeniheshimu, kunijali na kunipenda na yeye vyote anavifanya. Hata hivyo namshukuru Mungu kwa kurudi nyumbani ingawa sikuwa nawaza kama nitapata mume Mwanza lakini ndo imetokea.

Katika hatua nyingine Flora amezungumzia ugumu wa kubadilisha jina lake la awali (Flora Mbasha) hadi kufikia kulikubali jina la Madam Flora huku akishukuru kwa kuwa limeshaanza kuzoeleka kwa baadhi ya watu na hata watumishi wa Mungu. Flora anatarajiwa kufunga ndoa na Mwanaume aliyemtaja kwa jina moja la David kesho mkoani Mwanza baada ya ndoa yake na Muimbaji wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha kupeana talaka.

MSANII WA BONGO FLEVA 'NILLAN' AMPONDA SHILOLE KWA KUHARIBU SHOW SIKUKUU YA PASAKA


Na Mwandishi Wetu
MSANII wa Bongofleva anayetamba na kibao cha ‘Njenje’ Gilbert Paul maarufu kama ‘NILLAN’ (pichani kulia) ameponda kitendo kilichofanywa na msanii  mkubwa katika  tasnia hiyo Zuwena Yusufu ‘Shilole’ cha  kuharibu Show iliyotarajiwa kufanyika mkesha wa siku ya mkesha wa Pasaka na hivyo kusababisha hasara kwa promota.

Nillan aliyetarajiwa kufanya show siku pamoja na msanii mwingine Nuhu Mziwanda alisema kitendo kilichofanywa na Shilole siyo cha kiungwana kutokana na heshima kubwa aliyonayo msanii huyo kwa Taifa hili.


“Ukweli kitendo hicho mimi kama msanii chipukizi kimeniumiza sana, sikutaraji kingeweza kufanywa na msanii mkubwa na maarufu kama Shishi, namuheshimu kama dada yangu lakini kwa hili amejishushia heshima” alisema Nillan.


Show hiyo iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya  Merry Merry Entertainment, ilishindwa kufanyika baada ya Shilole kuchelewa kufika ukumbini hali iliyosababaisha mashabiki waliofika mahali hapo kulalamika warudishiwe fedha zao na baadae kuondoka.


Akizungumzia baada ya tukio hilo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Merry Mussa mbali na kulaani kitendo hicho cha Shilole alisema  ni lazima sharia itafuata mkondo wake kwa msanii huyo kulipa hasara yote iliyotokana na kitendo alichokifanya.


“Haiwezekani mtu tukubaliane afike  ukumbini saa  2 usiku, yeye anakuja  muda anaotaka, na hapo hapo hata kushuka kwenye gari hakushuka, hiyo ni dharau na kamwe sikubaliani na kitendo hicho hata kidogo” alisema Merry.


Shilole aliyetarajiwa kutoa burudani  siku hiyo ya mkesha wa Pasaka katika ukumbi wa Heinken uliopo Kijichi, aliwasili ukumbini hapo saa 7 za usiku tofauti na makubaliano na Promota aliyeandaa show hiyo.


Hata hivyo alipotafutwa Shilole kuzungumzia suala hilo alidai kufika ukumbini hapo kama taratibu zilivyo za wasanii kufika kwenye show mbalimbali hivyo haoni kama kuna kosa lolote alilifanya kuhusiana na show hiyo.

Kwa upande wake Nuhu Mziwanda aliyewah kuwa mahusiano na msanii huyo alikwenda mbali na kusema kitendo kilichofanywa na mpenzi wake huyo wa zamani ni ushamba na kumtaka kurudisha fedha alizochukua kutoka kwa promota.
Alisema anashangazwa kwanini Shilole alikubali kupokea fedha hizo na kuahidi kufanya show lakini badala yake akaingia mitini na kuibukia ukumbini muda ambayo show ilipaswa iwe mwishoni.


Akizungumzia suala hilo Meneja wa kampuni ya Ochu Entertainment  inayomsimamia msanii Nillan, Felix Mkuya alisema kitendo kilichofanywa na Shilole ni cha kushangaza na hakipaswi kufanywa na  wasanii wa hapa nchini.


“Imagine watu wametumia gharama kubwa kuandaa ile Show, kila msanii alishapewa hela yake mkononi, sasa kwanini yeye afanye vile, Nuhu Mziwanda alifika ukumbini mapema saa 12 jioni, alikadhalika kwa Nillan…sasa vipi Shilole afanye vile” alihoji Mkuya.

KALA JEREMIAH AWACHANA WANAOJISIFIA

Msanii wa miondoko ya 'HipHop' nchini Tanzania, Kala Jeremiah awachana wasanii wenzake kuwa waache tabia ya kuharibu misingi ya 'HipHop' kwa kutunga nyimbo zenye mashairi ya kujisifia vitu walivyokuwa navyo na kusahau misingi ya muziki huo
Kala Jeremiah amebainisha hayo baada ya kelele za wadau wengi wa muziki wa aina hiyo kudai wasanii wengi wa kizazi hiki wanashindwa kuimba nyimbo zenye kuleta ujumbe wenye uhalisia katika jamii na matokeo yake wengi wanaangukia kwenye mashairi yasiyokuwa na tija.
"Kwangu mimi naamini 'Hip hop' ni kitu kinachotakiwa kije na ujumbe au kiwe na kitu fulani ndani yake, 'actually' ilikuwa hivyo zamani hapa bongo, yaani wimbo unakuta una ujumbe mzuri ambao unalenga jambo moja kwa kulichambua kwa kina, yaani hadi msikilizaji anapata hamu ya kushawishika kurudia na kurudia. 'Hip hop' ni uhalisia". Alisema Kala Jeremiah
Aidha msanii huyo aliendelea kuwachana kwa kusema marapa wengi wa bongo siku hizi hawaeleweki wanaimba nini ?, wanakazi ya kuwachanganyia vitu mashabiki
Kwa upande mwingine msanii huyo amewasisitizia wasanii wote kuzingatia nguzo za muziki wanaofanya na endapo wanataka kufanya biashara basi itakuja baada ya kufanya kazi nzuri.

Baraka - Siwezi kuwa na mtu mwenye kasoro

Msanii Baraka The Prince akiwa na Najma

Msanii Baraka The Prince ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Acha niende' amefunguka na kusema yeye ameridhika na Najma kwa kila kitu na kusema hawezi kuwa katika maisha ya mapenzi na mtu ambaye anakasoro.
Baraka The Prince alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kwa Najma haoni kasoro yoyote ile na ndiyo maana aliamua kuwa naye kwani si utamaduni wake kuwa na mtu ambaye ana kasoro.

Mtazame hapa akifunguka mengi zaidi

P Funk amuonya Master J kuhusu Harmorapa

Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini P Funk Majani amemuonya mkongwe mwenzake katika game, Master J kutomsema vibaya kwa kumsapoti msanii Harmorapa kwa madai kuwa msanii huyo hana kipaji.

P Funk pia amemkumbusha Master J jambo na kumwambia kuwa hata alipoanza kumtengeneza Juma Nature majungu na maneno yalikuwa mengi lakini alitusua na kuwa msanii mkubwa nchini.

Akiongea na eNewz ya EATV, Majani amesema kuwa yeye kama Meneja wa Harmorapa ndiye anajua ni silaha za aina gani amezitengeneza na tayari ameshamtengeneza msanii huyo kwa ajili ya mashambulizi ya kufanya vyema katika soko la muziki hivyo mtu wa nje kama kina Master J wasimuungilie.

"Unajua nilipoanza kumtoa Juma Nature waliniambia siyo msanii ila ni MC cartoon na kwamba hawezi kuwa kama Solo au Prof Jay kwa hiyo nilichekwa sana Nature pia alisemwa sana lakini nachomshukuru Mungu amenipa uwezo wa kumtambua mtu mwenye kipaji na najua huyu ata'hit au la! na kwa Harmorapa nina imani atafika mbali sana kwa hiyo J yeye asizungumze anyamaze tuu". Alisema Majani

Katika hatua nyingine Majani amemuuelezea Harmorapa kama kijana anayestahili kuwapo kwenye sanaa hata kama si mwanamuziki lakini ni mburudishaji ambaye ana kipaji cha kuwafanya watu wafurahi hivyo hatakiwi kuwa nje ya sanaa na kwa sababu yupo tayari kwenye mikono yake anaamini atafika mbali.

"Harmorapa siyo msanii direct, kuna rapa, MC na Entertainer sasa dogo ni Entertainer. Master J kama anakumbuka kuna kipindi alimleta yule Sulukuchu studio anaimba ndugu Sulukuchu, sasa yule msanii gani lakini kuna John Walker (RIP) yule alikuwa mburudishaji kwa style yake ya ulevi kwahiyo Harmorapa anaingia kwa mtu kama Walker, watu wakipenda anachofanya ndiyo burudani yenyewe" Alisisitiza Majani.

Mkongwe huyo amesema yupo tayari kurudi kwenye game na kwa sasa anamalizia kuandaa ujio wake mpya kwa kikundi kipya cha muziki kinachoitwa Bongolos ambao anaamini watafanya vizuri sana kwenye sanaa.

Roma apatikana akiwa amejeruhiwa mkono na mguu

Msanii Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki amepatikana na sasa yupo katika kituo cha Polisi cha Oyesterbay jijini hapa.
Kaka wa Roma,Omar Musa amesema Roma alirudishwa nyumbani saa tisa alfajiri leo, na kwa sasa yupo kituo cha Oyesterbay.
Hata hivyo Omar hakutaka kueleza kwa kina kuhusu kurejea kwa Roma akisema kuwa hadi familia itakapotoa tamko.
Roma na wenzake wanne, walitekwa wakiwa katika studio za Tongwe, zilizopo Masaki, jijini hapa hivi karibuni.

Sakata la Roma: Wema Sepetu na Ray watofautiana mitazamo

Baada ya wasanii Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wenzao kuchukuliwa na watu wasiofahamika tangu usiku wa kuamkia juzi  wasanii mbalimbali wamekuwa wakitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kupost juu ya kusikitshwa na kitendo hicho, Wema Sepetu akiwa moja kati yao.

Lakini post ya Wema Sepetu ambayo aliiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram imeonesha kutokumfurahisha muigizaji mwenzake Ray Kigosi ambaye amepost pia katika ukurasa wake wa instagram na kueleza kutokufurahishwa na namna Wema alivyoandika kuhusu ishu hiyo.

==> Wema Sepetu aliandika hivi;
"This Is Scary… Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla… Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino…. Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni…??? Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake…. 

"Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa…??? Oh God help Us Please… Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu… Tumejawa sana Unafki…!!! All in All namuonea sana huruma Nancy…. 

"Our prayers are with u mama… Inshallah mumeo atapatikana… Tuzidi kumuomba Mungu…..🙏🏼🙏🏼🙏🏼…. Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani….!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino…?? 🙄🙄🙄 SMH.. "
This Is Scary... Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla... Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino.... Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni...??? Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake.... Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa...??? Oh God help Us Please... Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu... Tumejawa sana Unafki...!!! All in All namuonea sana huruma Nancy.... Our prayers are with u mama... Inshallah mumeo atapatikana... Tuzidi kumuomba Mungu.....🙏🏼🙏🏼🙏🏼.... Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani....!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino...?? 🙄🙄🙄 SMH...
A post shared by Wema Sepetu (@wemasepetu) on


==>Ray Kigosi  hakuipenda post hii, hivyo akajibu;
NAFIKIRI NI VEMA MTU KUELEZA HISIA ZAKE JAPO SIO BUSARA KWA MWENYE HISIA HIZO KUZIELEZA BILA WEREDI NAWASIHI WASANII WENZANGU KUPOTEA KWA ROMA ISIWE SABUNI YA KUTAKATISHA UCHAFU WA MTU SOTE TUMESIKITISHWA NA JAMBO HILO NA TUMEONYESHA KWA VITENDO. MIMI NIMEPOST INSHU YA ROMA TANGU JANA USIKU WEMA SEPETU WEWE ULIKUWA HUJAPOST CHOCHOTE TUSEME ULIKUWA HUNA UCHUNGU? ALAFU LEO UNAANDIKA KUWA BONGO MOVIE HAWAPO PAMOJA NA TUKIO LA ROMA HUKU NI KUTUGOMBANISHA NA WANANCHI WANAOTUAMINI. SISI BONGO MOVIE MARA NYINGI SANA TUNAKUWA PAMOJA KWENYE MATUKIO YA BONGE FLEVA TOFAUTI NA WAO. KAMA UNA UGONVI NA MTU HAYO NI MAMBO YAKO BINAFSI ILA USITUFANYE SISI TUONEKANA WABAYA MBELE YA JAMII UTAKUWA KICHAA KAMA USIPOPATA MAUMIVU KWA TUKIO LA ROMA NIMESIKITISHWA SANA POST YAKO @wemasepetu KAMA UNADHANI HUU NI MUDA MUAFAKA WA KUTAFUTIA POINT KATIKA TUKIO LA ROMA MKATOLIKI UMEFELI HILI NI JANGA LETU SOTE. @wemasepetu #(KINA ROMA WAKO WAPI?).

Maagizo Aliyoyatoa Waziri Nchemba Kwa Polisi Kuhusu Kutekwa kwa Msanii Roma

Msanii wa hip hop Roma Mkatolikia alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.

Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.

“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”

Maagizo Aliyoyatoa Waziri Nchemba Kwa Polisi Kuhusu Kutekwa kwa Msanii Roma

Msanii wa hip hop Roma Mkatolikia alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records  na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa  kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.

Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.

“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”

WEMA SEPETU AMJIBU HARMORAPA BAADA YA KUTAKA MAHUSIANO NAYE

Harmorapa na Wema Sepetu

Wema amecharuka katika mtandao wake wa instagram leo ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo anayetamba na ngoma ya 'Kiboko ya mabishoo' kutangaza kuwa anampenda msanii huyo na kwamba anaumizwa na jinsi watu wanavyomuumiza kimapenzi.
Aidha mwanadada huyo amemtaka msanii huyo kupigana jinsi atakavyoweza kulifikisha jina na muziki wake juu pasipo kumtumia yeye kama njia na kuongeza ni kumvunjia heshima mbele ya familia, chama, marafiki pamoja na mpenzi aliyenaye.
"Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi siyo wa aina hiyo". aliandika Wema.
Katika kuonesha kuwa muigizaji huyo amekerwa na kauli ya Harmorapa, ameongeza kwamba "Do u think na mimi ni wa aina hiyo? Usinidharaulishe.... Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one butan not for you and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako lets stop there"

ROMA MKATOLIKI NA WENZAKE WAKAMATWA

Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usimsahau mchizi' amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.
Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambay pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio.
Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records. 
"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay
EATV tulipojaribu kumtafuta Roma Mkatoliki simu zake zilikuwa zikiita tu bila kupokelewa.
Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Rais Magufuli abariki ngoma ya Ney wa Mitego ipingwe redioni/TV

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.
Mwakyembe amesema Rais John Magufuli ameruhusu wimbo wa Ney wa Mitego"WAPO" upigwe vyombo vyote na pia uongezewe vionjo ikiwemo rushwa na mengine. Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.

MAHAKAMA YAMUONYA AGNESS MASOGANGE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange baada ya kutohudhuria kesi hiyo mahakamani.

Kesi hiyo ambayo imetajwa kwa mara ya kwanza mbele ya hakimu mkazi wa Kisutu Wilbard Mashauri wakili wa serikali Adolf Mkini amesema kuwa mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepham.

Ameeleza kuwa mshitakiwa anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam  alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine) na kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017  alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Mshitakiwa anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015 na kuwa uopelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika licha ya mshtakiwa kutokuwepo mahakamani hapo.

Hata hivyo  wakili wa Masogange, Nictogen Itege aliwasilisha udhuru mahakamani hapo juu ya mteja wake kutokuwepo.

Licha ya maelezo hayo Hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa kuheshimu masharti ya mahakama na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 20, mwaka huu mshitakiwa yupo nje kwa dhamana.

Mh Temba atapeliwa shilingi milioni 100

Rapper kutoka TMK Wanaume Family Mh Temba ameelezea sababu za yeye kuwa kimya ni kutokana na kutapeliwa pesa na mfanyakazi wa bandari jijini Dar es Salaam. Temba amekuwa akimposti tapeli wake kupitia ukurasa wake wa Instagram ishara ya kumwinda tapeli huyo na kutangaza donge nono kwa atakayefanikiwa kumpata.

Kupitia kipindi cha Zero Planet ya Ice Fm temba amesema, “Nilishindwa kutoa kazi kwasababu hapa juzi kati nilikua na matatizo sikuweza kuyazunguma sana kwenye media. Kuna jamaa alifanya wizi kakimbia na pesa, ndio maana project zangu hazikuweza kutoka, alinidhulumu pesa nyingi sana.”
Alipoulizwa juu ya kiwango na biashara waliokuwa wanafanya na huyo jamaa, Temba alisema, “tulikuwa tunafanya kazi ya magari, huyo jamaa alikuwa anafanya kazi bandarini alikuwa anadili na haya magari ambayo watu wameshindwa kuyalipia ushuru kwahiyo si tunatoa pesa tunaenda kuyauza, tulikuwa na chama chetu cha washikaji kama 18 hivi kila mtu akatoa pesa kama milioni mia moja na kitu hivi,” ameongeza.
Amesema kumbe hata safari ya South Africa walivyoenda kushoot video ya ‘Waache Waowane’ ya Chege, Temba naye alikwenda kushoot video ya wimbo wake mpya japo hakufanikiwa na majanga yalipoanzia baada ya kuona jamaa hawatumii mkwanja kutoka kwenye biashara zao. Walivyorudi bongo ndio wakajua kuwa jamaa kawapiga mkwanja.
Temba na Chege kwa sasa wanafanya vizuri na wimbo mpya uitwayo ‘Go Down.’

Vanessa Mdee Kaachiwa Kwa Dhamana

Mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu Vee Money ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kuwa ameshikiliwa kwa takribani wiki moja kufuatia tuhuma ya dawa za kulevya inayomkabili.

Mdee aliachiwa jana jioni ambapo anatuhumiwa kutumia na kusambaza dawa za kulevya. Alishikiliwa na Polisi tangu juma lililopita baada ya kwenda kuripoti kufuatia kutajwa kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa hizo iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam, Paul Makonda.

Madawa ya Kulevya: Vanessa Mdee ajisalimisha Polisi

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita.

Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.

Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa chini ya Lebo B'hitts.