HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

UPDATES: SCORPION AFUNGULIWA MASHTAKA UPYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mtuhumiwa Salum Henjewele almaarufu kwa jina la Scopion (mwenye kanzu) akitoka katika viunga vya mahakamani Ilala leo. 

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfungulia mashtaka mapya Salum Njwete (Scorpion).
Amefunguliwa mashtaka mengine yanayofanana na ya awali ya unyang’anyanyi wa kutumia silaha.
Hata hivyo Njwete amekana shtaka na kurudishwa rumande,huku Hakimu Flora Haule anayesimamia kesi hiyo akizuia dhamana.
Awali Mahakama hiyo ilimfutia mashtaka yanayomkabili Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo na Kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore alikubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.
Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki upya mshtakiwa huyo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo.
Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi Mrisho.

SERIKALI YATANGAZA UHAKIKI WA WANAFUNZI WOTE WALIOKO VYUO VIKUU AMBAO WANASOMA SHAHADA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.   

Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo, vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanavyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI ATOA TAMKO JUU YA MATUMIZI YA ALAMA ZA TAIFA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi hao katika kueleza jamii umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya vielelezo vya Taifa walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 27, 2016 kulia kwake ni Afisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Nyamagory Omary.
Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) muonekano sahihi wa Nembo ya Taifa wakati wa mkutano wake na wanahabari Juali 27, 2016, wa kwanza kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Frank Shijja.
Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akionesha baadhi ya Vielelezo muhimu vya Taifa wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi yake Julai 27, 2016.


Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Cassian Chibogoyo amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya vielelezo vya Taifa kama njia ya kuheshimu Taifa na kuonesha uzalendo.

Chibogoyo ameyasema hayo hii leo katika kipindi cha pili cha ‘TUJITAMBUE’ ambacho kimewakutanisha waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari Jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa muendelezo wa elimu sahihi ya vielelezo vya taifa kwa jamii.

Akitaja alama tatu muhimu za Taifa ambazo ni Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa na Ngao ya Taifa, Chibogoyo amesema kila kimoja kinasimamiwa na sheria ili kuhakikisha matumizi yake yanaliletea heshima Taifa la Tanzania hivyo, wananchi ni vyema wakawa sehemu ya kutunza tunu hizo na kujiepusha na matumizi yasiyo sahihi.

Katika ufafanuzi wake ameeleza kuwa, Wimbo wa taifa una Tone Maalum na maneno maalum yaliyowekwa hivyo uimbaji unaoongeza vibwagizo kinyume cha uhalisia wake ni kosa kisheria.

Akielezea matumizi ya Bendera ya Taifa amesema ni kinyume cha sheria kubadili rangi zilizoainishwa kisheria kwani kila rangi ina maana yake na kuwa matumizi ya bendera serikalini yana utaratibu maalum kuanzia Ofisi ya Rais hadi kwa viongozi wa ngazi za chini.

“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pekee ndiye anayeweza kufanya mabadiliko ya Bendera ya Taifa na Ngao ya Taifa kama kinavyoagiza kifungu cha 5 cha sheria ya vielelezo vya Taifa Na. 15 ya mwaka 1971.” Alisema Chibogoyo.

Kuhusu Nembo ya Taifa amesema ziko nembo nyingi feki mtaani ambazo pia zinatumiwa na wananchi katika matangazo au shughuli za kibiashara kinyume na matakwa ya sheria huku akitumia kipindi hicho kuonesha tofauti zilizopo katika alama sahihi na zile ambazo si, sahihi.

Bwana Chibogoyo alihitimisha kikao hicho kwa kuwashukuru wadau wote na kusema kuwa tarehe ya kikao kingine itatolewa kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu.

UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA AWALI YA UJENZI WA RELI YA KATI (STANDARD GAUGE)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akitiliana saini na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying kuhusu makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying mara baada ya kusaini makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetiliana saini na Benki ya Exim ya China makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge).

Makubaliano hayo ya awali yamefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile kwa niaba ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiliaji saini Dkt. Likwelile amesema hatua hiyo inawezesha hatua za upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuanisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.

Zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kati yenye urefu wa Kilometa 2,190 ambapo Benki hiyo itashirikiana na Serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.

Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza na Tabora-Mpanda-Kalemela-Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.