HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

TWIGA WAMO HATARINI YA KUANGAMIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Idadi ya twiga imepungua sana maeneo mengi Afrika
Twiga wamepungua sana duniani katika kipindi cha miaka 30 iliyopita na kwa sasa wanakabiliwa na hatari ya kuangamia.
Idadi ya twiga duniani imeshuka kutoka 155,000 mwaka 1985 hadi 97,000 mwaka 2015 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi wa mambo asilia (IUCN).
Idadi ya wanyama hao imepungua sana kutokana na kuharibiwa kwa maeneo wanamoishi, uwindaji haramu na migogoro ya kisiasa katika maeneo mengi Afrika.

Baadhi ya aina wa twiga, sana maeneo ya kusini ya Afrika, wanaongezeka hata hivyo.
Hadi kufikia sasa, IUCN hawakuwa wameorodhesha twiga kuwa miongoni mwa wanyama walio hatarini.
Hata hivyo, kwenye orodha yao mpya ya wanyama walio hatarini, mnyama huyo ameorodheshwa kuwa "hatarini", baada ya idadi ya wanyama hao kushuka kwa zaidi ya asilimia 30

Kwa mujibu wa Dkt Julian Fennessy, mwenyekiti wa kundi la IUCN linaloshughulikia twiga, wanyama hao "wanaangamia kimya kimya."
"Ukienda kwenye safari, twiga wapo kila mahali," aliambia BBC News.

"Ingawa kumekuwepo na wasiwasi kuhusu ndovu na vifaru, twiga wamesahaulika. Ni jambo la kusikitisha kwamba idadi yao imeshuka sana na ni jambo la kushangaza, kwamba wamepungua hivyo katika kipindi kifupi."
Twiga hupenda sana kupeleleza na hili huwafanya kuwindwa kwa urahisi na majangili na wapiganaji
Ongezeko kubwa la idadi ya watu limesababisha maeneo mengi ya misitu kuharibiwa kwa ajili ya kilimo, jambo ambalo limepunguza maeneo wanamoishi twiga.

Vita katika baadhi ya maeneo Afrika pia vimeathiri idadi yao.
"Katika maeneo haya yenye vita na migogoro, hasa kaskazini mwa Kenya, Somalia na Ethiopia katika mpaka wake na Sudan Kusini, twiga ambao ni wanyama wakubwa wanaliwa."

OFISI YA MAKAO MAKUU HIFADHI YA SERENGETI YATEKETEA KWA MOTO.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

MWENYEKITI WA BODI YA UTALII (TTB) AWAAGA WATALII NA WAANDISHI WA HABARI WANAOKWENDA RUJEWA KUSHUHUDIA KUPATWA KWA JUA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akiagana na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena Kiongozi wa Msafara wa Watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaotoka Dar es salaam kwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua ambapo wageni mbalimbali pamoja na wanahabari kutoka vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa wako mkoani humo kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo nadra kutokea duniani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi wakiagana na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena pamoja na Antonio Nugas Mtembezi kutoka Clouds Media Viongozi wa Msafara wa Watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Baadhi ya wapiga picha wa vyombo vya habari hapa nchini wakiendelea na kazi yao wakati msafara huo ukiondoka jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devotha Mdachi wakielekea kwenye gari kwa ajili ya kuwaaga baadhi ya watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua wakitokea jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari na kuwapa maneno kadhaa wakati akiwaaga baadhi ya watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua wakitokea jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari, kulia ni Bi. Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB na kutoka kushoto ni Mtangazaji wa Clouds Baby Kabaya na Mkurugenzi wa Masoko TTB Bw. Philip Chitaunga,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akiasalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Utalii TTB.
Kulia ni Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena na kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Geofrey Tengeneza na Mkurugenzi wa Masoko TTB Bw. Philip Chitaunga.

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA - PWANI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. --- Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA. Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo. Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi.
Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.  Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
 Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu, Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za kupata elimu ya juu. --- Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu. "Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu," alisema Kingi. Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
 Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi. Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa elimu akiwa na  katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).

Shule ya msingi ya Chole iliyojengwa na Mwekezaji wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development. 


Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu. Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo. 

Picha zikionyesha jinsi majengo ya kale yalivyoonekana kabla hayajakarabatiwa na kufanyiwa usafi. 
Katibu wa Harambee wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia Mkoa wa Pwani, Mohammed Kingi akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Chole. Shule hiyo pamoja na masomo hayo yanafadhiliwa na kampuni ya Chole Conservation and Development 
Kituo cha elimu ya watu wazima, hapa ndipo hujifunza kingereza
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza. Alisema kuwa aliwatafuta baada ya kubaini kwamba wakazi wa kijiji hicho hawana mwamko wa elimu na wamekuwa wakifadhili hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu na mambo mengine ya muhimu kwa ajili ya elimu.
"Mbali na hilo kwa sasa tuna shule ya chekechea, kituo cha wanawake cha kujufunza kusoma, kituo cha kujifunza kompyuta na kituo cha wanafunzi na watu wengine kujifunza lugha ya Kiingereza na maktaba," alisema mkurugenzi huyo na kuendelea: 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmad alisema kuwa serikali imekuwa ikifaidika kwa kupata dola 10 kwa kila mgeni anayeingia na kulala katika hoteli ya Chole mjini inayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development sambamba na dola 5 kwa kila mgeni anayetembelea majengo ya kale ya mapango ya Chole ambayo yakikuwa yakitumika katika biashara ya watumwa. 
Nae Bi. Riziki Hassan Selenge alisema kuwa hapo mwanzo mambo yalikuwa magumu tokea kuingia kwa mwekezaji huyo ndiye amekuwa mwasisi wa maendeleo kijijini kwao kwa vile asilimia 99 wakazi wa Chole hali zao ni masikini na hawakuweza kupeleka shule watoto wao. 
Upande wake Mwenyekiti mstaafu, 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. 
Akitoa historia fupi Bw. Sadiki alisema mchakato wa kumpokea mwekezaji huyo ulifanyika Desemba 4, 1993 kwa kueleza dhamila yake na tulimkubalia kwa kufuata sheria zote na makubaliano tuliwekeana nae tokea kipindi hicho ambapo tokea ameingia mwekezaji huyo amekuwa akitekeleza mkataba aliyopewa na kijiji.

TANAPA YAIONGEZEA NGUVU TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA MASHINDANO YA OLIMIPIKI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho kwa wanahabari na wageni wengine katika hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa, inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki yatakayoafanyika mwezi Agosti  nchini Brazil.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi Milioni tano kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki.

Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki. 
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi "Track Suit "maalumu zenye maandishi na nembo yanayotangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wanaojiandaa na mashindano ya Olimpiki
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi pamoja na mavazi maalumu kwa ajili ya wanariadha hao .
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) waliohudhuria hafla hiyo.kutoka kushoto Mkurugenzi wa Utalii na Masoko,Ibtahim Musa,Meneja Utalii Johnson Manase na Mhifadhi Vitalis Uruka.
Wanariadha watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Olimpiki katika jiji la Reo De Jeneiro nchini Brazil wakiwa katika mavazi maalumu yanaotangaza vivutio vilivyoko nchini.
Mkufunzi wa Wanariadha wanaojiandaa na mashindano ya Olyimpiki ,Francis John akizungumzia matarajio yake juu ya vijana hao.
Mmoja wa Wanariadha hao,Alphonce Felix Simbu akizungumza mara baada ya kupoke msaada kutoka  TANAPA.
Baadhi ya Wanahabari na wageni wengine waliofika katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kushuhudia makabidhiano hayo.
Mwanariadha Said Makuka atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Sara Ramadhan ,mwanadada pekee atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Alphonce Felix atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Fabian Joseph atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Wanariadha wanne watakao iwakilisha Tanzania katika Michuano ya Olyimpiki nchini Brazil wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Antony Mtaka ,wengine kutoka kulia ni Mkufunzi wa wanariadha hao,Francis John na anyefuatia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masokowa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza  kutumia fursa ya mashindano ya Olyimpiki yanayotarajia kuanza mwezi ujao katika jiji la Rio de Janeiro nchini Brazili kutangaza vivutio vya utalii kupitia wanariadha wa Tanzania.

Hadi sasa ni wanariadha wanne ,wakiume watatu na wa kike mmoja ndio waliofuzu kushiriki mashindano hayo na tayari wako kambini katika hosteli za Chuo cha Misitu cha FITI zilizoko West Kilimanjaro wilayani Siha.

Akiongea mjini Arusha wakati akikabidhi msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya wanariadha hao Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi amesema wameamua kutumia fursa hiyo pia kusaidia wanariadha hao wanaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo ili waweze kurejea na medali.

Akishukuru kwa msaada huo Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu AnthonY Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwakatia bima ya Afya mwaka mmoja wanariadha hao pamoja na familia zao ili wanapokua nchini Brazili wasiwe na mawazo mengi kuhusiana na familia zao walizoziacha hapa nchini.

Naye mmoja wa wanariadha waliofuzu kushiriki mashindano hayo Alphonce Felix pamoja na mkufunzi wa timu hiyo ya Riadha Francis John wameushukuru uongozi wa Riadha kwa kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini kwa miezi saba na kuahidi safari hii timu hiyo haiendi kushiriki bali kupambania medali.

Wanariadha waliopo katika timu hiyo ya taifa wanaotarajiwa kwenda Brazili ni mwanamke pekee Sara Ramadhani, Fabiani Joseph, Saidi Makuka na Alfonce Felix.