Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, George
Nyatogo
Na Joachim Mushi,
Thehabari.com
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu
nchini pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imewaengua zaidi ya wanafunzi
3074 walioomba vyuo na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka
2012/13.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na taasisi hizo kupitia mitandao yao (website) Agosti 10 na 12, 2012
zaidi ya wanafunzi 3074 wameenguliwa katika maombi yao kwa kuwa na dosari
mbalimbali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pekee imeorodhesha zaidi ya wanafunzi
2,649 ambao imebaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo
ya vyuo.
Miongoni mwa makosa ama dosari
ambazo bodi imezibaini kwa walioenguliwa kwa sasa ni pamoja kukosekana kwa vyeti
vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha
ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa Serikali za
mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa
waombaji.
Kwa upande wake TCU imewaengua
jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali, ambayo imeyabainisha
katika taarifa yake.
Miongoni mwa dosari ambazo
zimetajwa na TCU kwa wanafunzi hao ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za
vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano (O' level na A' level Index number),
miaka ya kumaliza masomo (year of completion), mawasiliano sahihi kwa muombaji
(Contact information e.g. Mobile phone number, email address and postal address)
pamoja na uchaguzi wa masomo (Programme selected).
Waweza kuingia katika linki
hii hapo chini na kuona majina ya waliobainika kuwa na dosari anuai katika
maombi yao kwa TCU http://www.tcu.go.tz/uploads/ file/LIST%20OF%20APPLICANTS% 20FOR%202012-2013% 20ADMISSIONS%20WITH%20MISSING% 20INFORMATION.pdf
Pia waweza kutembelea linki
zifuatazo na kushuhudia majina ya waliobainika kuwa na dosari hizo katika maombi
yao kwa bodi ya mikopo;- http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=365&Itemid=66
http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=366&Itemid=67
http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=367&Itemid=68
Hata hivyo taasisi hizo mbili
zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na
kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa. Kwa
taarifa zaidi pia waweza kutembelea mitandao ya www.heslb.go.tz na www.tcu.go.tz



No comments:
Post a Comment