Mabaki
ya Helikopta mbili za Uganda ambazo ziliripotiwa kutoweka siku ya Jumapili
zimepatikana mashambani nchini kenya.
Kanali Cyrus Oguna ambae ni
msemaji wa jeshi la Kenya amesema hatma ya watu 14 waliokuwemo ndani ya chombo
hicho haijulikani.
Ndege hizo mbili zilikuwa
ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikipelekwa nchini Somalia kuongezea nguvu kikosi
cha umoja wa Afrika kilichoko huko.
Helikopta ya tatu ambayo
pia ilikuwa katika msafari huo ilitua kwa ghafla katika eneo la mlima Kenya siku
ya Jumapili.
Kanali Oguna amesema wote
waliokuwa katika helikopta hiyo ya tatu waliokolewa.
Ni helikopta moja peke yake
ndio faulu kutua vizuri na kuongeza mafuta katika mji wa Garissa ulioiko
kaskazini mwa Kenya.
Helikopta hizo nne ambazo
zimetengezezwa Urusi ziliondoka siku ya Jumapili Uganda zikelekea Somalia kabla
ya kukumbwa na mkasa huo.
Masalia ya helikopta hizo
mbili ambazo awali ziliripotiwa kutoweka zilionekana juu ya mlima Kenya na
maafisa wa Shirika la Wanyama pori, limeripoti gazeti la Daily Nation la
Kenya.
Msemaji wa jeshi Kanali
Oguna ameimbia BBC kwamba kikosi cha jeshi la Kenya linaelekea katika eneo hilo
la Mlima Kenya , ambao ndio mlima wapili kwa urefu ,afrika.
Afisa huyo amefafanua
kwamba moja ya helikopta hizo imeharibika kabisa ilhali ya pili imeharibika
kiasi.
Helikpta hizo zilikuwa
zinaelekea nchini Somalia kuongezea nguvu vikosi vya Umoja wa Afrika ambavyo
vinajitayarisha kuvamia mji wa Kismayo na kuwafurusha wapiganaji wa Al Shabaab
toka mji huo ambyo ndio ngome yao kuu.
Chanzo - BBC
Swahili



No comments:
Post a Comment