Askari
wa Kikosi Cha kutuliza Ghasia FFU wakiweka ulinzi mkali eneo la
Kariakoo baada ya kufunga mitaa ya Kongo na ile ya jirani kutokana na
kuibuka vurugu zilizotokana na ugonvi wa nyumba ambayo kwa maelezo ya
watu wa karibu nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka 20 kati
ya wamiliki na wapangaji kutokana na kutengeneza hati feki.
Mmoja
wa majeruhi kwenye vurugu hizo akiondolewa eneo la soko la Kariakoo
baada ya kuanguka chini kutokana na milipuko ya mabomu ya machozi
yaliyokuwa yakitumiwa na askari polisi waliofika kutuliza ghasia katika
eneo hilo, ambayo iliambatana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na vijana
waliokua wakitetea upande mmoja wa ugomvi huo.
Wananchi wakizungumza na waandishi wa habari kutoa maoni yao juu ya mgogoro huo.
Kikosi
cha kampuni ya Yono Auction Mart iliyopewa tenda ya kusimamia ubomoaji
wa nyumba hiyo chini ya ulinzi mkali wa polisi wakiendelea na kazi
kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Kongo.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) akifyatua bomu la machozi.
Vijana wakirusha mawe.
Vijana wakirusha mawe.
Soko kuu la Kariakoo likiwa limefungwa kufuatia machafuko hayo.
MAENEO ya Kariakoo jijini Dar es Salaam leo yalikuwa hayakaliki kufuatia vijana waliokuwa wakipambana na polisi wakipinga uvunjwaji wa nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na swahiba wao aliyetajwa kwa jina la Shaban Hassan. Nyumba hiyo imekabidhiwa kwa Samir Sadiq baada ya kushinda kesi Mahakama ya Ilala jijini.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

No comments:
Post a Comment