Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro,
wakati ofisa huyo alipofika nyumbani kwa Makamu akiwa na Karani wa
Sensa na msimamizi wake kutoka Kituo cha Oysterbay, kwa ajili ya
kukamilisha zoezi la Sensa, leo asubuhi Agosti, 26, 2012. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASHIRIKI ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
leo Agosti 26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa
ya watu na Makazi akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Dkt.
Bilal, ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa
akiulizwa na Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye
alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria
Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley
Mahembe na Radegunda Maro.
Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.
Akizungumza
baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote
kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha
zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Box 5380 Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment