HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MANENO OSWALD AMDUNDA RASHID MATUMLA, NATURE, MAUNDA, MWASITI, LINAH, JAHAZI WAFUNIKA NDANI YA DAR LIVE SIKU YA EID MOSI

Matumla akisulubiwa jukwaani wakati wa mpambano huo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Juma Kassim ‘Juma Nature’, akionyesha ukongwe wake.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki zake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Estelinah Sanga ‘Linah’, akiwa jukwaani.
Mwasiti Almasi akikamua na wacheza shoo wake.
Maunda Zorro akionyesha umaarufu wake.
Sadick Momba (kushoto), akipambana na Venance Mponji katika mpambano wa utangulizi ambapo Sadick aliibuka mshindi.
Julius Thomas (kushoto), akizidunda na Jumanne Kirumbe kabla ya Maneno Oswald na Matumla kupanda ulingoni. Julius alishinda mpambano huo.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mabaga Fresh ambaye sasa yuko katika kundi la Wanaume Halisi, JB Mkuu wa Maadui akiwajibika.
Mwimbaji wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Khadija Yusuf akitumbiza jukwaani.
Malkia wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid akiwajibika.
Watoto wakicheza muziki ndani ya bwawa la kuogelea.
Baadhi ya umati uliokuwa ndani ya ukumbi huo.
Pichani ni Linah, Mwasiti na Maunda Zorro wakiwa Backstage ya Dar Live wakisubiri kuanza kwa show

Maunda Zorro akiwa juu ya jukwaa la Dar Live

 Mwasiti juu ya staji la Dar Live

Linah juu ya jukwaa akifanya vitu vyake kwa wakazi wa Mbagala waliofika Dar Live
 
Bondia Maneno Oswald akitangazwa baada ya kumdunda Rashid Matumla.
..............................................
MPAMBANO wa ndondi baina ya mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla ambao ulifanyika ukumbi wa maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, ulishuhudia Oswald akimchakaza Matumla kwa pointi.

Mbali na mpambano huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kulikuwa pia na burudani za aina mbalimbali, likiwemo disko la watoto ambao pia walifurahia kuogelea katika bwawa maalum na michezo mingine mingi. Kwa upande wa muziki kulikuwa na shoo kali zilizofanywa na wanamuziki Juma Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi zima la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf.  
Picha: Musa Mateja, Richard Bukos/GPL na DJ Choka

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: