MBUNGE wa jimbo la Ismani wilaya ya Iringa mkoani Iringa Wiliam Lukuvi amesema kuwa mbinu ya wafanyabiashara wakubwa wa mpunga kuendelea kuwaibia wakulima wa Pawaga na Idodi dawa yake ipo jikoni baada ya kuanzisha mpango kabambe wa kufunga mashine kukoboa mpunga na kuuuza mchele badala ya mpunga.
Lukuvi
ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu ( sera na uratibu wa
bunge) alitoa kauli hiyo Leo Mara baada ya kukagua mfereji wa mradi wa
umwagiliaji katika kijiji cha Magozi kata ya Ilolompya ambao utajengwa
kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.
Alisema kuwa
wakulima wa mpunga katika eneo hilo wamekuwa wakilanguliwa mazao Yao ya
mpunga na wafanyabiashara hao wakubwa ambao wamekuwa wakinunua mpunga
kwa bei ambazo wanapenda wao na sio bei inayomkomboa mkulima .
Lukuvi
alisema mfereji huo ambao unajenga unataraji kumwagilia 600 hivyo
katika tarafa hiyo ya Pawaga ambayo wananchi wake wanategemea kilimo cha
umwagiliaji watapiga hatua kubwa katika kilimo hicho.
Alisema
kwa kipindi kirefu kata hiyo ya Pawaga ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la
njaa ila baada ya serikali kuanzisha mradi huo wa kilimo cha
umwagiliaji wananchi wameanza kuondokana na tatizo hilo la njaa na sasa
hata maisha Yao kiuchumi yameanza kuboresheka kwa kuongeza ujenzi wa
nyumba za bati tofauti na a wali ambapo nyumba za bati hazikuwepo.
Aidha
alisema kuwa mbali ya mradi kujengwa kwa kipindi tofauti tofauti
serikali kwa bajeti yake ya mwaka 2012/2013 serikali imetenga zaidi ya
shilingi milioni 600 kwa ajili ya mradi huo.
Lukuvi
alisema kuwa katika tarafa hiyo ya Pawaga kuna mfereji miwili mikubwa
ya umwagiliaji ukiwemo mfereji wa Mlenga na huo wa kijiji cha Magozi
unaoendelea kujengwa.
Hata hivyo alisema ujenzi
huo wa mifereji ya umwagiliaji katika tarafa hiyo imesababisha
mapinduzi makubwa ya uchumi kwa wananchi na hivyo kuwataka wananchi
kuongeza kasi ya uzalishaji.
Lukuvi alisema
katika miaka miwili hii kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 anatarajia
kuona tarafa hiyo inakuwa na umeme wa uhakika na kuwa njia hiyo
itawawezesha kujikomboa kiuchumi zaidi.
Pia
alisema upo mkakati wa kujenga Maghara ya kuhifadhia chakula katika
tarafa hiyo pamoja na mashine za kukoboa mpunga na kuwataka
wafanyabiashara wa mashine za mpunga waliopo mjini Iringa kufika
kuwekeza katika tarafa hiyo kwa kujenga mashine .
wakati
huo huo Mbunge Lukuvi ametangaza ofa maalum kwa wapiga kura wake ambao
wanataka kujenga nyumba za kisasa kuwa ofisi yake itajitolea kununua
bati Kiwandani na kuzifikisha hadi mjini Iringa na huko watanunua bati
hizo kwa bei ya Kiwandani kwa kuanzia bati 10 na kuendelea.
MWISHO



No comments:
Post a Comment