Mwanasheria
wa kujitegemea Howard Msechu (25), mkazi wa Mbezi Beach, Dar es Salaam
amefikishwa katika Mahakama ya Kinondoni kwa kukabiliwa na mashitaka
mawili likiwemo la kumiliki bastola aina ya Wallter bila kibali.
Mwendesha
Mashitaka Mratibu wa Polisi Mkimbu Ramadhani, alimsomea mshitakiwa
shitaka la kwaza mbele ya Hakimu Amaria Mushi, kuwa Mei 29, mwaka huu
katika maeneo ya Kimara, mshitakiwa alikutwa na silaha hiyo yenye namba
za siri 141223 bila kuwa na kibali.
Katika
shitaka la pili, alidai kuwa mshitakiwa alikutwa risasi tatu za silaha
hiyo. Mshitakiwa alikiri makosa yote yaliyokuwa yanamkabili.
Hakimu
Mushi alitoa hukumu ya kosa la kwanza kwa mshitakiwa huyo kuwa achague
moja kati ya kufungwa jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh. 150,000.
Katika
kosa la pili, Hakimu Mushi alimtaka mshitakiwa huyo achague kufungwa
miezi sita au kulipa faini ya Sh. 20,000. Hata hivyo, mwanasheria huyo
alikubali kulipa faini za makosa yote mawili.
CHANZO: NIPASHE



No comments:
Post a Comment