Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph warioba (katikati)
akiongea katika mkutano na Waandishi wa Habari hivi karibuni. Kulia ni
Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid na Bw. Casmir Kyuki (kushoto)
Kwa
kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote
wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume
ambayo ni www.katiba.go.tzKusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba
ya sasa ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti
yanayoainishwa kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba
Mpya.1.
1.
MAMBO YA KUZINGATIAKwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa
na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
2.
(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa
uraia wake anayo haki ya kushiriki katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa
asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza
kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.
(b)Utaratibu wa Utoaji Maoni:Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika.
3. Njia hizo ni kama zifuatazo:
4. (i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti www.katiba.go.tz barua pepe ya Tume, katibu@katiba.go.tz (This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ),
nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769 (ii)Utoaji wa maoni
kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya Tume,
ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi
ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
Endapo
Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa
ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama
Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya
maoni iliyoandaliwa na Tume.
5. (c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina yake matatu;
(ii) (ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) (iii) nchi na mji anaoishi;
(iv)
(iv) endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi
yake (ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).Tume inapenda
kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la uhuru na
hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu raia wa
Tanzania pekee. Kwa maelezo zaidi bofya: http://www.katiba.go.tz/index.php/maoni-nje-ya-nchi



No comments:
Post a Comment