Afya ya mtotoJuliana Mwinuka mkaziwa kijiji Cha Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
HABARI MPYA KUHUSU MTOTO JULIANA LEO
Habari
za leo kutoka Hospitali ya Muhimbili zinadai hali ya mtoto Juliana
Mwinuka kwa jana na leo imekuwa ya kutia matumaini baada ya kuanza
kula na kunywa dawa na hata kuomba chakula anachokitaka ,pia jicho lake
moja limeanza kuonyesha dalili ya kupona huku tatizo kwa sasa miguu
yake hainyoki na yawezekana akaanzishiwa mazoezi zaidi .hizi ndizo
habari mpya juu ya Juliana Mwinuka.
Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa mtandao huu http://francisgodwin.blogspot.com wa Bw. Francis Godwin
Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi
CHAMZO:http://francisgodwin.blogspot.com



No comments:
Post a Comment