Magari
yaliyotumika kuwafikisha washitakiwa waliofanya vurugu, uaribifu na
wizi wa mali za makanisa Mbagala, wakiwasili katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kujibu mashitaka yanayowakabili.
Washitakiwa wa kike katika kesi hiyo wakielekezwa kuingia kwenye ukumbi wa mahakama.
Washitakiwa hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuingizwa kwenye ukunmbi wa mahakama. Picha na Francis Dande
---
DAR ES SALAAM, Tanzania
WATU
37 wakiwamo wanawake wawili wanaotuhumiwa kuchoma makanisa, kufanya
uharibu wa mali na kuiba kwa kutumia nguvu huko Mbagala Zakhem jijini
Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu chini ya ulinzi mkali.
Washitakiwa
hao waliofikishwa mahakamani hapo wakiwa kwenye magari matatu ya polisi
aina ya Defender majira ya saa 6:26 mchana chini ya ulinzi mkali wa
askari waliokuwa wamevalia mabomu viunoni, kutokana na kufanya matukio
hayo kama sehemu ya malipizi yao kutokana na madai ya kunajisiwa kwa
mkojo kwa Msahafu kulikofanywa na kijana wa Kikristo.
Baada
ya kushushwa, watuhumiwa hao waliamriwa kuchutama kabla ya kuanza
kuingizwa kwenye chumba namba moja cha mahakamani hapo, huku kukiwa na
tahadhari kubwa ya kiusalama ndani na nje ya mahakama hiyo.
Kwa
upande wa mashtaka, watuhumiwa hao wamefunguliwa kesi nne tofauti za
jinai kwa mpigo, kesi ya kwanza ni jinai Namba. 240/2012, namba
241/2012, namba 242/2012 na 243/2012.
Watuhumiwa
hao walisomewa mashtaka hayo mbele ya Mahakimu Wakazi wawili Sundi
Fimbo anayesikiliza kesi tatu huku moja ikisikilizwa na Hakimu Mkazi
Bingi Mashabara.
Upande wa Jamhuri kwenye keshi hiyo uliwakilishwa na Wakili Mwandamizi Tumaini Kweka, Lasdlaus Komanya na Joseph Maugo.
Wakili
Kweka alidai katika kesi ya jinai namba 243/2012 inayowakabili
washitakiwa 17 ambao ni Maenga Rwenda, Hamad Euli, Shego Sheso,
Ramadhani Mgule, Mashaka Iman, Kassim Juma Kigoni, Ibrahim Himu, Hamza
Fundi Hamza, Mikidadi Sadick, Juma Mbegu na Rahimu Boga.
Wengine
ni Issa Abdallah, Hamis Kmwaga, Ramadhani Mbulu, Hamed Mohamed, Mohamed
Yusuf na Msha Alifa, wanakabiliwa na kosa la kula njama kutenda kosa la
unyang’anyi wa kutumia silaha kinyume na kifungu cha 287A cha sheria
ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2012.
Wakili
Kweka alidai kuwa Oktoba 12, mwaka huu huko Mbagala wajatwa waliiba
vitu mbalimbali ikiwamo 'Laptop', 'Printer Projector', spika, saa za
ukutani na viti vya plastiki vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 20
mali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Usharika wa Mbagala.
Imeelezwa
mahakamani hapo kuwa, kabla ya kuiiba watuhumiwa wamtishia mlinzi
Michael Samwel kwa mashoka na nondo kwa lengo la kujipatia vitu hivyo.
Kweka
alidai shitaka jingini ni la kuchoma kanisa kinyume na kifungu cha
319(a) cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ambapo washitakiwa hao kwania ovu
walichoma kanisa hilo mali na kuongeza kuwa shitaka jingine ni la
kuharibu mali kama madirisha, meza, mfumo wa umeme, milango,
aircondition vyote mali ya kanisa hilo ambavyo vyote vikiwa na thamani
ya sh 500,000,000.



No comments:
Post a Comment