Dear Colleagues,
Naomba niwasimulie yaliyonipata jana ili na ninyi mchukue tahadhari mapema!
Jioni
baada ya kutoka kazini nilielekea nyumbani Tabata Kinyerezi moja kwa
moja na nilipitia njia zifuatazo.Nilipita Fire,Magomeni,Round about ya
Kigogo,Tabata-Dampo, moja kwa moja hadi Tabata Segerea then
Kinyerezi.Nilipofika njia ya kuingia kwangu,pembeni kuna Bar inaitwa
Fantastic na ina Kigorofa,basi nikamkuta jamaa yangu mmoja nilyekuwa na
mazungumzo naye then nikapark gari then nikashuka na kuongea naye nikiwa
nimesimama umbali kidogo kama hatua kumi na tano na nilikopark gari
langu-Noah!Baada ya mazumgumzo ya hardly dk 5 nikarudi kwenye gari ili
niingie home,hamadi nikakuta tayari kioo cha gari cha kulia nyuma ya
kiti cha dreva umeshavunjwa na wamechukua lap top yangu binafsi,
iliyokuwa ndani ya begi na kulikuwa na documents nyingine nyingi na
ziliakuwa original docs-vyeti vya shule na kadi za benki!
Ila
upande wa pili wa barabara kulikuwa na waendesha pikipiki wenge tu sasa
nikaanza kuwauliza je walimwona nani akiingia kwa gari langu,sikupata
majibu hata kidogo!Katika kufutailialia na nikaenda polisi,walinieleza
kuwa kuna wimbi la vijana ambao hutumia magari ya kifahari na pikipiki
ambao kazi yao ndo hiyo tuu!na walijaribu kufutailia zaidi na ikaonekana
kuwa hawa watu wanapenda kufuatilia watu nyuma na hata kama kuanzia
mjini hadi katika vitongoji vyetu!Hii ni story ya kweli na imenitokea
jana jioni ndugu zangu.
Sasa
lengo la kuwasimulieni kisa chote hiki ili nanyi mchukue tahadhari!hata
kama mtu unashuka kwenda kuchimba dawa,shuka na all your belongings
especially your computer na vitu vyote muhimu ndugu zangu.Usipuuzie
kwani yaliyonikuta jana sijalala hata kidogo maana Hasara niliyopata ni
kubwa isiyopimika ndugu zangu.Katika kundelea na uchunguzi wamebaini
kuwa maeneo ya tabata ni hatari sana kwa sasa na hawa wahuni wanatumia
gari aina ya Rav 4 nyeusi,na wakati mwingine wanatembea na Toyota
OPA.Ndugu zangu nawasihi sana ikiwezekana acha laptop nyumbani beba
external disc au flash disc maana kwenye gari sio tena shehemu nzuri ya
kuhifadhia docs zako.
Hayo ndo yaliyonipa jana na sina jinsi nabaki tu mdomo wazi! Samahanini kama nitakuwa nimewaboa but nawaokoa na ninyi ndugu zangu. Mtu yoyote atakayeona karatasi zime tupwa mahali tafadhali jaribu kuangalia maana na kama ni zangu nitashukuru nikizipata.
Asante Cayus



No comments:
Post a Comment